Huyu hawajui wa znz.
Wa znz hawataki kuvunja muungano . Wanachotaka ni uhuru zaidi ili nchi yao ifaidike na mahusiano na wengine bila kubanwa na masharti ya mungano.
Wawe huru katika katika mambo kiuchumi sarafu mikopo na misaada bila ya kubanwa na masharti ya muungano.
Tumeona miaka 50 namna gani uchumi wa znz ulivo poromoka kutokana na muundo wa muungano. Mfumo wa muungano ndio sababu kubwa ya kuanguka uchumi wa znz ma bila kupata msaada wa maana kutika serikali ya mungano kujikwamua.
Wakati tanganyika ikisaidiwa kujikwamua kiuchumi toka wakati wa mwinyi mkapa na sasa kikwete mazungumzo yote na mashirika ya fedha nje kama world bank IFC au IMF
Tanzania imefanya mazungumzo na mashirika haya kwa niaba ya tanganyika na wamesaidia sana kukwamua uchumi wao kwa kupewa ushauri na fedha . Katika masharti yale tanganyika ilikubali masharti magumu ili kupata kupata misaada hio kutoka mashirika ya fedha.
masharti hayo ni kubinafsisha makampuni na mashirika ya umma,
Kufungulia njia makampuni ya nje kuwekeza
Kubinafsisha ma benki
Na kubwa zaidi ambalo ulikua ni mwiba mkali ni lazima wakubali kushusha thamani ya fedha ya Tanzania.
Kutokana na hali ngumu walokua nayo serikali ya tanganyika ndani ya muungano walikubali kuumeza mwiba huo na kukubali kushusha thamani ya shilingi .
Kabla ya masharti haya USD $ 1 =Tshs 20 tu. Hii imekwenda mpaka sasa ni shs 1630.
Na hali ya uchumi na uwezo wa SMZ wakati huo haikua mbaya ulikua mzuri tu wa kujiweza.
Serikali ya mungano kwa niaba ya mambo ya tanganyika wakapokea misaada mikubwa na mikopo baada ya kukubali masharti ya IMF na World Bank.
Nini kilitokea ? Wakati tanganyika ikifaidika na misaada hio, Zanzibar ndio mwanzo wa kuanza kuporomoka uchumi wake .wao hawakupata fidia yoyote kutokana na Tanganyika kukubali kushuka kwa Shilingi.
Bajeti yake ilianza kuharibika mfumuko wa bei ukuwa juu bei ya mafuta ukawa juu . Wakati tanganyika ikipata misaada kujikwamua zanzibar ikaachwa kufa kabisa kiuchumi.
Muundo wa sasa wa muungano hauruhusu znz kuingia katika mikataba mashauriano au kupata misada kuwa na mahusiano yoyote na mashirika ya fedha au mashirika ya kimataifa kama FAo ,Unicef,UNdp,IMF au hata Comminwealth,OIC au hata mashirika ya mahusiano na umoja wa visiwa vya Indian Ocean !!
Hivyo mfumo uliopo haufai kabisa. Utakua unafaa kama kuna nia ya kuimaliza zanzibar kiuchumi na kuifanya wawe mafukara wa kutupwa.
Nadhani sote nia yetu tunapenda kuona Tanzania bara inaendelea na kusonga mbele na pia tunapenda kuona Zanzibar nao wanaendelea kiuchumi na sio tegemezi.
Kutaka serikali 3 sio kuvunja muungano ni njia nzuri ya kuumarisha kukiwa na njia njema .
Kuwa na serikali tatu sio sababu ya kuanza kuchochea chuki, sio sababu ya Tanganyika kuwabana wazanzibari na kadhalika.
Haubadili mahusiano yetu bali kuleta mfumo mzuri zaidi utaoboresha mahusiano na uchumi wetu.
Huyu mheshimiwa ametaja kuhusu ardhi na wafanyabiashara wa znz walioko walioko bara ni kweli wa znz wapo Bara na wanafanya kazi na biashara lakini wanasaidia kujenga uchumi wa bara na sio znz. Kiserikali znz haifaidiki chochote hakuna hata anaeweka akiba yake katika benki ya znz
Na pia huyu mheshimiwa ni katika watu wa kuogopwa kama ukimwi ni mbaguzi,mchochezi ndio maana maoni yake ameleta upemba na uunguja.
Hasemi kuwa Tanzania bara walotaka serikali 3 ni 66% ila yeye ameona wapemba tu. Ni Racist mkubwa.na hawa ni katika wale ambao serikali ya muungano inapoteza fedha nyingi kuwaweka madarakani ikadhaniwa kuwa wataendelea kuulinda muungano kwa porojo na propaganda.ukweli tanganyika haihitaji kupoteza fedha kuwa na mamluki kutoka znz eti waunge mkono muungano hata kama unaizika znz na kuwafanya omba omba.vibaraka hawa wanazidisha tu ari na morari ya wa znz kuuchukia muungano.
tuufanye muungano huu uwe wa wananchi na wananchi wataupenda na wataulinda , hakutakua na sababu kwa serikali ya bara kuwalinda na kuweka vubaraka kama hawa huku ikigharamika bure.hawa wanapigania matumbo yao na ndio walio influence CCM kuweka msimamo wa serikali 2 japo kwa gharama ya 66% ya watanzania bara waliotaka serikali 3.
Serikali tatu ndio suluhisho la kupata muungano wenye nguvu zaidi.
Hata wakati wa apartheid kule afrika ya kusini walikuwapo waafrika na waliojifanya wazalendo sana lakini walikubali mfumo ule wa kibaguzi .wakakubali kuwa viongozi wa zile bantustans. Na walikubali kupewa uhuru wa hizo bantustan na kupewa "urais" mimi namfananisha huyu seif khatib na buthelezi aliepewa kaji urais wa wazuli !!!