Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
soma rasimu ya katiba vizuri hususan maoni ya ccm utaelewa. kila kitu kimewekwa wazi
 
hatutaki miserikali miiingi, yote ya nini? mbili ndio mpango mzima
 
Sisi tunaogelea kwenye bwawa wachimbalo wazenji. Bara tumekufa kabisa na tunaendeshwa na wachache wa zenji
 
Napendekeza tuwe na serikali moja tu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Marekebisho yafuatayo yafanywe katika Muungano huu.

Zanzibar ipewe hadhi ya "Special Administrative Region" na Kiongozi mkuu wa Zanzibar aitwe "Chief Executive Officer" na iendeshe mambo yake kwa kuwa na autonomy kwa mambo yote isipokuwa mambo yafuatatayo: 1. Mambo ya nje, 2. Ulinzi na 3. Uhamiaji. hii ni model ya jinsi China inavyoendesha serikali yake na visiwa vya Hong Kong na Macau.
 
Hata Mimi naamini katika serikali moja

Tanganyika ilishafeli na haina sifa ya kuifanya zanzibar ikubali serikali moja.
Mtihani wa dini.
Zanzibar ni nchi ya waislamu na utamaduni wakr ni wa kiislam . Hili Tanganyika huwa hawataki kulitambua.
Tukiwa nchi moja maana yake zanzibar kukubali kuondoa shughuli zote za maendeleo ya uislam na kuivunja ofisi ya mufti na mahakkama ya kadhi.
Tanganyika wajifunze kustahamiliana na kutofharau uislam na waislam ndo tuzungumze serikali moja
 
Chadema ndo wanadharau waislam
 
Kama tuna upenda muungano na ni waumini wakubwa wa Muungano nadhani Serikali 1 ni suluhu katika kuulinda muungano, tukisema muundo wa serikali 2 ni wazi mpaka sasa umeshindikana kwasasababu kwa miaka karibia 50 sasa umeshindwa kutatua kitu kinachoitwa kero za muungano na kwa upande mwingine serikali tatu naona kama ni njia ya kuelekea mwisho wa muungano kwasababu ni wazi kuwa kwa wazanzibari ambao kwa miaka mingi wamekuwa wakilalamika kuwa muungano kwao ni kero sasa misingi hiyo utakapopatikana mfumo wa serikali 2 huru (yaan Zanzibar na Tanganyika) ni wazi kuwa baada ya hapo watataka zanzibar yao isimame yenyewe kama yenyewe.
 
Tanganyika ilishafeli na haina sifa ya kuifanya zanzibar ikubali serikali moja.
Mtihani wa dini.
Zanzibar ni nchi ya waislamu na utamaduni wakr ni wa kiislam . Hili Tanganyika huwa hawataki kulitambua.
Tukiwa nchi moja maana yake zanzibar kukubali kuondoa shughuli zote za maendeleo ya uislam na kuivunja ofisi ya mufti na mahakkama ya kadhi.
Tanganyika wajifunze kustahamiliana na kutofharau uislam na waislam ndo tuzungumze serikali moja

Automatically unapendekeza serikali tatu ili zanzibar iwe huru zaidi na tanganyika kadhalika ili zisiingiliane ktk jambo uliloeleza; au sio?
 
Kwa kuwa ni nchi mbili zimeungana hapakwepeki kuwa ma serekali tatu au moja nikiwa na maana moja itavunja uzanzibar na utanganyika jambo ambalo ni zuri lkn pia tatu kutakuwa na serekali za nchi husika na ya muungano. nadhani mtakubaliana nami.
 
Habari zenu watanzania kuhusu hii rasmi mpya juu ya mkakati wa kutengua katiba mpya mimi sioni kama kuna haja ya kuwa na serikali 3 kwa sababu tukiangalia serikal ya mapinduz zanzibar Bara kwanza kuna v2 vingi vinashare kwa kuwa na serikali ya 3 tayari tunataka kuwa na nchi mbili tofauti .
 
Hivi kwani ni lazima tu kila mtu aandike hapa, jamaa sielewi hata umeandika nini hueleweki kabisa.
 
Back
Top Bottom