Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Kura ya Maoni: Muundo upi wa Muungano unafaa?

Muundo upi wa Muungano unafaa?

  • Serikali 1

    Votes: 81 23.3%
  • Serikali 2

    Votes: 22 6.3%
  • Serikali 3

    Votes: 241 69.5%
  • Sijui

    Votes: 3 0.9%

  • Total voters
    347
  • Poll closed .
Mi nataka muundo ubadilishwe....i mean...nikinunua gari zanzbar kwa m4....nilifikishe bongo kwa m4 labda na ela usafiri labda 50000 ivi.

So serekali 3 ndo itakua poa sana
 
serikali 3 inafaida ya kuirudisha Tanganyika,kuhusu gharama hata serikali ya sasa inaendeshwa na kodi za watanganyika.
 
Serikali moja inatosha 2/3 hizo ni za wasaka tonge
 
Serikali tatu! serikali ya Tanganyika, ya Zanzbar, na shirikisho la Tanganyika na Zanzibar
 
Waasisi wa Muungano Waliasisi Serikali lengo lilikuwa ni kuelekea Serikali moja Serikali moja ndio dawa ya muungano
 
Mimi pia ningependekeza hiki kipindi ambapo bunge la katiba litakuwa likizo ingeitishwa kura ya maoni nchi nzima wananchi waulizwe wanataka Serikali 1,2 au 3
 
Waasisi wa Muungano Waliasisi Serikali lengo lilikuwa ni kuelekea Serikali moja Serikali moja ndio dawa ya muungano

Uko sahihi mkuu...kwanini wanasiasa wanataka serikal mbil au Tatu??hapa serikal moja ndio mpango mzma
 
Mi nataka moja!hizi gharama tunazoingia watanganyika kuwabeba hawa wazenj sioni tija yake...Kama ulifuatilia Bunge la katiba baada ya UKAWA kuondoka na kuwasikiliza kwa makini wajumbe kutoka Zanzibar unaweza kuelewa namaanisha nini
 
Eleza Faida Ya Serikali 3 Na Hasara Ya Serikali Mbili,au Eleza Faida Ya Serikali 2 Na Hasara Ya Serikali Tatu,karibuni

Serikali Mbili ni Hasara kuliko Serikali hata 1 au 3 , ebu fikiria kuna Marais wawili,Makamu wa Rais watatu,waziri mkuu , wizara ya Muungano,na Wizara ya waziri asiye na Wizara maalumu, Huu ni Uongozi mkubwa na ni Ghari Hakuna mfano ! Pia kuna Mianya mingi ya Ulaji wa Pesa inayotoka Hazina Tanganyika kuelekea Zanzibar ,huku Pesa zinazotengwa kwa ajili ya kumaliza Kero kupitia Wizara ya muungano nazo zinaliwa na Wajanja ndio Maana Kero hazimaliziki , kero zimegeuzwa Mladi wa Wajanja na wanaombea kero zizidi ili na Fungu liongezeke wapate kuneemeka maradufu ,sasa Zanzibar wamevunja katiba wanajiita Nchi kinyemela wamelundika watumishi wa umma na Utitiri wa wabunge kwa kutegemea pesa za Tanganyika , endapo Rais angelikuwa mmoja tu na ZNZ akatawala Gavana na Tanganyika akatawala Gavana , muungano usingekuwa na Hasara Kama hizi zilizopo sasa, hasa ukizingatia muungano wa sasa umechakachuliwa si sawa na muungano ule wa Nyerere na Karume ambao haukuwa kero Kama hizi za sasa.
 
Mi naona bora serikali moja tu ikishindikana bora kuwe na serikali ya majimbo
 
Back
Top Bottom