Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
CROSSING THE RUBICON
Julius Caesar alivuka Mto Rubicon mwezi Januari 49 BC akiwa na jeshi kubwa nyuma yake na baada ya mguu wake kukanyaga upande wa pili wa mto vita ya wenyewe kwa wenyewe baina ya Warumi ikaanza.
Kesho ni tarehe 27 Oktoba 2020 siku ya Kura ya Mapema Zanzibar siku ambayo Maalim Seif leo ametoa tamko kuwa Wazanzibari watoke kwa amani wakapige kura.
Maalim Seif Shariff Hamad ana jeshi kubwa la Wazanzibari nyuma yake wanaomuunga mkono.
Nashindwa kuendelea kuandika.
Mpenzi msomaji wangu unadhani nini kitatokea?
Tumuombe Allah atupe nusra kwani dua inafuta qadar, yaani kile ambacho mwenyewe Allah alishakipitisha kitokee.