Kura ya Siri: Maoni ya Mheshimiwa Zitto Kabwe

Kura ya Siri: Maoni ya Mheshimiwa Zitto Kabwe

chademaistheway

Senior Member
Joined
Aug 18, 2010
Posts
100
Reaction score
86
Haya ndio aliyoaandika Mheshimiwa Zitto Kabwe kwenye FACEBOOK PAGE yake:






Siri? Wazi?


Wabunge wamegawanyika, wananchi wamegawanyika. Wachambuzi kama Mimi Mwanakijiji na wengine wanashauri kura ya wazi. Mgawanyiko pia umekaa kivyama ambapo wengi wa wabunge wa CCM wanataka iwe wazi na wengi wa wabunge wa upinzani wanataka iwe siri. Wajumbe wa BMK (Bunge Maalum la Katiba) kama Maria Sarungi-Tsehai na wanataka kura ya Siri. Siri au Wazi imekuwa habari kubwa na imesheheni vyombo vya habari. Mwafaka umekosekana.

Kwa nini Siri?


Kura ya siri humlinda mpiga kura asijulikane chaguo lake na hivyo kama kuna madhara ya chaguo lake huepukwa. Hii ni pamoja na kuadhibiwa kwa kunyimwa fursa fulani fulani au hata kuondolewa kwenye chama cha siasa alichomo. Wanaotaka kura ya siri wanataka ulinzi dhidi ya madhara hayo na pia kuwapa uhuru zaidi wabunge kuamua bila ya woga. Chaguzi zote kuu duniani kote hufanyika kwa kura ya siri.

Kwanini Wazi?


Kwenye mabunge takribani yote duniani kura huwa wazi. Lengo ni kuweka wazi misimamo ya vyama/makundi kwani mabunge hupata wabunge kutoka kwenye vyama/makundi. Hivyo inakuwa ni vema wawakilishi hao wajulikane kwa makundi yao kama wamepiga kura kwa matakwa ya makundi na sio matakwa binafsi.
Kura ya Wazi pia huweka rekodi ya mbunge/mwakilishi binafsi na hivyo kujua misimamo yake kutokana na rekodi yake ya kura. Kwa mfano mgombea Urais nchini Marekani anajulikana sera zake kwa kuangalia historia yake ya kura kama alikuwa Seneta au Mwakilishi (Congressman/woman).

Wabunge wafanyaje?


Siku ya Jumatatu wabunge wataamua kama wapige kura ya siri au ya wazi kwa kupiga kura ya siri. Nasikia kampeni zinaendelea Dodoma kuhusu uamuzi huo. Siasa zetu tunazifanya ni 'zero-sum game' kwamba anayepata anapata vyote na anayekosa anakosa vyote. Haipaswi kuwa hivyo hata kidogo.

Tufanye hivi;


- Kwa kuwa vifungu vya Katiba ni masuala (issues) basi ni vema kifungu kwa kifungu kura ziwe za wazi ili wawakilishi wa makundi wenye maslahi na masuala yao wajue misimamo ya kila mjumbe na rekodi ziwe wazi. Kama mtu anaunga mkono ndoa ya mashoga ajulikane, anayeunga mkono haki ya kupata elimu bila vikwazo ajulikane nk.
- Upitishaji wa Katiba nzima ufanywe kwa kura Siri ili kutunza uhuru wa Mjumbe kuamua kuhusu katiba kama ilivyo kwa wananchi watakapopiga kura kwenye 'referendum' kwa siri.
Ni vema vyama vya siasa vitambue kuwa Katiba inayotakiwa ni ya wananchi na sio katiba ya vyama. Hivyo kuweka misimamo ya kivyama kunaondoa kabisa dhana nzima ya kuandika Katiba na kupata mwafaka. Ni vema kwa chama kama CCM kuacha kabisa kutumia wingi wake kuburuza mchakato wa Katiba. Bila mwafaka Katiba haiwezi kupatikana.


It must not be a Zero-Sum Game.......

Absalom Kibanda Mwananchi Communications Ltd Ismail Jussa January Y. Makamba David Kafulila William J. Malecela John MnyikaDennis Msacky Bunge la Katiba
 
Kwa mazingira ambapo vyama vimeshaweka misimamo kuhusu masuala
kadhaa kama muungano..katika mazingira ya Tanzania ambapo vyama
bado ni Mungu mtu...na katika kiwango cha uchanga wa demokrasia yetu
naitamani kura ya wazi kwa maana ya principles& practices. .lakn
mazingira tuliyonayo hapa yananisukuma kuamini kuwa uhuru wa
wajumbe ushatekwa na misimamo ya vyama na mbinu pekee ya kuwafanya
wawe huru ni kura ya siri kifungu kwa kifungu ili kuongeza uhuru wa
wajumbe kufanya maamuzi wanayoamini bila hofu wala mashinikizo
 
Zitto waambie wenzako mizigo tumeishindwa. Hili suala SI la chama ni la TAIFA.
Ukoo wa Panya hamridhiki.
 
Last edited by a moderator:
zito ni msoma upepo ... hana lolote ... i have rated him very low.
 
Wabunge wataamua kwa kura ya SIRI kama kura iwe ya UWAZI au USIRI.
Wananchi tusihofu wingi wa CCM bungeni
 
zito ni msoma upepo ... hana lolote ... i have rated him very low.
Sasa ndugu yangu kwenye siasa lazima usome upepo bila hivyo kimbunga kitakubeba ati. One thing I like about Zitto ni mtu anayeamini katika lobbying and advocacy ili kuleta muafaka wa kueleweka, hebu tuchukulie mfano CCM wakaendelea na Msimamo wake hala CDM nao wa kwao, nini kitatokea?
 
Last edited by a moderator:
Wabunge wafanyaje?


Siku ya Jumatatu wabunge wataamua kama wapige kura ya siri au ya wazi kwa.......

kupiga kura ya siri.
[/B]

Kwa nini na hapo wasipige kura ya wazi ili kupata msimamo wa kura ya SIRI au WAZI?

Nimeshangazwa!!!
 
Jamaa kiboko yenu huyu bavicha wote mnatetemeka kila mkisikia kaongea kitu mnajua kawamaliza.
 
Tujikumbushe 13th amendment to abolish slave trade kipindi cha abraham lincoln kule marekani!Wale congressmen walipiga kura ya wazi kupinga utumwa na walishinda kama ingekuwa siri utumwa marekani ungeisha miaka hamsini baada ya lincoln
 
Kwa hiyo yy anawasiliana na facebook na c Bungeni?
 
namchukia sana huyu zito! Tangu niufahamu usnitch wake nataman kumpiga hata mawe.
 
Kwa mazingira ambapo vyama vimeshaweka misimamo kuhusu masuala
kadhaa kama muungano..katika mazingira ya Tanzania ambapo vyama
bado ni Mungu mtu...na katika kiwango cha uchanga wa demokrasia yetu
naitamani kura ya wazi kwa maana ya principles& practices. .lakn
mazingira tuliyonayo hapa yananisukuma kuamini kuwa uhuru wa
wajumbe ushatekwa na misimamo ya vyama na mbinu pekee ya kuwafanya
wawe huru ni kura ya siri kifungu kwa kifungu ili kuongeza uhuru wa
wajumbe kufanya maamuzi wanayoamini bila hofu wala mashinikizo

Umenena Mkuu, Tanzania huwezi kuilinganisha na demokrasia zilizoendelea-Hivi unakukmbuka hata kiongozi mkubwa wa bunge letu ilipotumika kura ya wazi akaulizwa mara mbili na spika aliyumba na kubadili 'msimamo'?
 
Naunga mkono hoja kura za kula ndio ziwe wazi, kura za haki na mustakabala wa taifa ziwe siri!.
Pasco
 
Back
Top Bottom