Hute
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,537
- 6,472
nimeangalia bunge la katiba mara nyingi. kila mjumbe aliyekuwa anasimama nilimsikia hadi mwisho. nilichoona ni kama ifuatavyo;-
1. kila mbunge wa ccm aliyesimama alisapoti kura ya wazi, hata wale niliowaamini kama wana akili kama prof
tibaijuka,prof magembe na wengine wengi. hakuna hata mbunge mmoja wa ccm aliyesimama kusapoti wazo la kura
ya siri.
2. wabunge wote wa upinzani na wajumbe wale wasio wabunge wa bunge la jamhuri, walitaka kura iwe ya siri.
3. kati ya wachangiaji wote, wabunge wa upinzani na wale walioteuliwa sasa tu ndio walikuwa wanaongea kutoka
moyoni na wakiongea unaona kabisa kuwa wanatoa point zenye maana, waliobaki wanaosapoti kura ya wazi wote
walikuwa wanaonyesha kuwa wanaongea tokea usoni tu wala haitoki moyoni, wanaongea kinafiki kabisa hadi nafsi
zao zinawasuta.
4. Hadi shehe Jongo alisimama na kuweka vifungu vya kuran kusapoti kura ya wazi, akanifanya nimwone kama amenunuliwa vile.
5. Prof. Lipumba, cheyo, na Maria sarungi,na wengine wote waliosapoti kura ya wazi waliongea maneno mazito yenye
akili yanayoweza kumshawishi mtu yeyote kuwa wanaongea kitu cha kweli, na walionyesha ni wakweli na
wanasema kitu cha kweli toka mioyoni mwao, hakuna hata tone la unafiki.
6. Prof. Lipumba alisema kuwa, kunatakiwa kuondolewa doubt, kwamba kuna tetesi kuwa CCM wote wameweka
waangalizi atakayeenda kinyume na walivyokwishapanga watamshughulikia akitoka. na kwamba tayari kati ya
wabunge wale wa ccm wengine ni waratibu wa kuangalia nani anakaidi walichokubaliana. hivyo katiba hii kama
ikipitishwa kwa namna hiyo itakuwa ni ya ccm si ya tz.
7. Kuna dogo mmoja alisimama akamsema sana warioba kuwa amezeeka, na alikuwa anamwogopa mwalimu kumpinga
kuhusu muungano kipindi yupo hai sasa anakuja kumpinga akishakufa..hakutaja jina ila alimsema waziwazi
nikashindwa kuelewa huyu mbunge wa ccm amepata wapi ujasiri kukiaibisha chama chake namna hiyo.
SWALI LANGU; Hivi kwanini wabunge wooote wa CCM wamesapoti kura ya wazi, hakuna hata mmoja aliyetaka ya siri, kuna nini nyuma ya pazia?
mwisho wa yote, nawapongeza waliosapoti kura ya siri, kwasababu hiyo ndiyo democrasia ya kweli. kusema ukweli wabunge hawtakiwi kutudanganya, miaka ile ya unafiki imepitwa na wakati, kizazi kile cha zamani kimepitwa na wakati, siku hizi mnatakiwa kufanya kitu kinachoeleweka na watu wakakubali kuwa kweli kitu hiki kinaeleweka, kutufanya watz kama mbumbumbu, mnapika bomu. Mungu ibariki tz.