Uchaguzi 2020 Kura yako Uchaguzi Mkuu 2020

Uchaguzi 2020 Kura yako Uchaguzi Mkuu 2020

Machomane

Member
Joined
Jul 10, 2020
Posts
6
Reaction score
4
#28oktoba2020

Kila mwananchi ana nafasi ya kupanga na kuchagua aina ya maisha anayotaka na hata maisha ya kizazi chake kijacho. Kwa Kupiga Kura ni nafasi yako ya kuchagua au kutetea Maswala unayohitaji kama vile, Afya, Elimu, Miundombinu nk. Kitendo cha Kupiga Kura ni sawa na kuamua au kushiriki katika maamuzi yatakayo amua mustakabali wa maisha yako juu ya mawala yako muhimu.

Serikali huundwa na Wawakilishi wetu ambao tumewachagua kwa Kupiga Kura na ili wakaunde Serikali itakayo amua mustakabali wa maisha yetu ya sasa na ya vizazi vijavyo tunapaswa sisi kama jamii kujitokeza na kwenda Kupiga Kura.

Ili ufanye maamuzi sahihi juu ya maisha yako na kizazi chako juu ya maswala muhimu ni vyema ukatenga muda wako na kwenda kushiriki katika mikutano ya Kampeni ili uweze kusikiliza Ilani na Sera za Vyama vya Siasa na Wagombea wao ili uweze kufanya chaguo na maamuzi sahihi. Kitendo cha kwenda kusikiliza Ilani na Sera za Wagombea kitakusaidia kujua maamuzi yako yatakuwa na athari gani kwako na, kwa jamiii na Taifa kiujumla kwa maisha ya sasa na yajayo.

Mabadiliko yanaanza na mimi na wewe, ili kwa pamoja tuweze kubadili maisha yetu na jamii zetu kwa ujumla, Tunapaswa kuamua, Kuamua kwa ajili yetu na kwa wale tunaowajali yaani; ndugu jamaa na marafiki, Ikiwa wewe unayo fursa ya Kupiga Kura, pengine ndugu jamaa na marafiki watakosa fursa hiyo kutokana na sababu mbalimbali basi fanya maamuzi kwa niaba yao.

Tanzania ni Moja. Sisi ni Wamoja.
 
Hili ni kweli kabisa KURA YANGU ndio itaamua hatma yangu na kizazi changu, kujitokeza kwa wingi katika mikutano ya Kampeni na kusikiliza Sera za wagombea na kuzichambua zipi Pumba na Upi Mchele kisha OKTOBA 28,2020 Mapemaaaaa unaenda kumchagua kiongozi unaeona atatujali sisi wananchi na si vinginevyo.
#KuraYakoSautiYako
#TwendeKupigaKura
 
Mwaka huu tutapiga kura,hatuwezi poteza nafasi ya kuchagua viongozi wetu.
God Bless Tanzania
 
Selikali ya chama cha mapinduzi na NEC yao ya kishamba HAWATAKI WATANZANIA TUPIGE KURA.

1. Wameamua kuiingiza nchi masikini kama hii kwa kishindwa kutoa vitambulisho vya Taifa ambavyo tungetumia kupiga kura.

2. NEC NA CCM wameamua watanzania wasipate fursa ya kupiga kura hata ya urais nje ya kituo walichojansikishia.

3. CCM NI WOGA SANA.
 
Back
Top Bottom