alfani nkaya
New Member
- Aug 1, 2021
- 1
- 0
Utangulizi
Kwa majina Naitwa Alfani Omari, kutoka Arusha.
Nimejitokeza kuandika makala hii yenye kichwa cha habari, Kura Yako, Ufaulu Wao.Tuungane Ili Wafaulu.
Lengo la makala hii ni kuwasaidia wanafunzi kutoka shule ya secondari Kwangunda, wanaotoka katika mazingira magumu. Shule ya sekondari Kwagunda ipo mkoani Tanga, katika halmshauri ya wilaya ya Korogwe vijijini. Ni shule ya kutwa na ni shule ya kata pia.Shule hii inapokea wanafunzi kutoka vijiji mbalimbali vya halmashauri ya Korogwe vijijini, vikiwemo, Mkwakwani, Gereza, Kwagunda, Magunga, Mkokola, Mng'aza, Pacha na Ubiri. Vingi ya vijiji hivi viko mbali na eneo ambako shule ipo. Hali hii husabaisha wengi wanafunzi hawa kutmbea umbali usiopungua kilomita 8 au zaidi.
Kwa mfano, kwa wanafunzi wanaotoka kijiji cha mkokola, hulazimika kutembea kilomita 8(4 kwenda, 4 kurud) kila siku. Nyenzo kuu ya usafiri ni baiskeli, lakini kuna kundi kubwa la wanafunzi ambapo wanatoka katika mazingira magumu, hivyo wazazi wao wameshindwa kuwanunulia baiskeli hali ambayo huwafanya kutembea kwa miguu au wakati mwingine huweza kubahatika lifti kutoka kwa wanafunzi wenye baiskeli. Tatizo la usafiri linachangia kiasi kikubwa mahudhurio duni na hivyo kufanya wengi wao kushindwa kumaliza shule au kufeli kabisa.
Kwanini naomba kura yako?
Baada ya kugundua chanzo kikubwa kinachopelekea wanafunzi katika shule hii kushindwa kumaliza masomo yao, au wengi wao kufeli kwamba yanachangiwa pia na ukosefu wa usafiri hasa kwa wale wanaotoka katika familia zenye kipato duni, nikaona hii fursa mtandaoni ya uandishi wa makala. Nikaona niitumie nafasi hii kuandika makala yenye lengo la kuwaleta wadau pamoja ili tuwe sehemu ya mabadiliko katika jamii zetu haswa kwa kutoa kile kidogo tunachoweza.
Mimi kama muandishi wa makala hii, endapo ikatokea andiko langu likapita na kuwa mshindi wa nafasi yoyote ile, kile kitakachopatikana basi wanajukwaa tununue baiskeli na kuzigawa kwa wanafunzi wasio na baiskeli katika shule hii.Kwakufanya hivyo tutakuwa tumesaidia ndugu zetu kupunguza adha ya usafiri na hivyo kuwawezesha kuhudhuria shule kwa Urahisi.
Ni vipi zoezi la ugawaji baiskeli litafanyika?
Kama andiko hili litapita, na nikatangazwa mshindi, utawala wa jamii forum utahusika moja kwa moja kwenye zoezi la ununuzi mpaka ugawaji wa baiskeli.Na hvyo zoezi zima la ugawaji nitapendekeza lirushwe mubashara ili wanajukwaa wote waone idadi ya baiskeli zitakazogawanywa kulingana na uhitaji.Endapo kuna kiasi kitabaki basi hicho ndio mimi nitachukua.
Hivyo nawaomba, ndugu, jamaa na marafiki, kulipigia kura andiko hili ili tuungane kufanya jambo la kujitolea kwa jamii zetu. na wale watakaolipigia kura wote andiko hili watakaa kwenye list kama waliohusika na utoaji wa msaada huo bila kuwasahau JamiiForums wenyew. Na kama itatokea hivyo pia, nembo ya jamii forum itawekwa kwenye kila baiskeli kama kuthamini mchango wao.
Asanteni, sana
Kura Yako, Ufaulu wao.Piga kura ili uitolee jamii yako.