Kuna tetesi zinasema kuwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kinaandaa sherehe za siku ya walimu duniani ambayo itafanyika mkoani Ruvuma na mgeni rasmi atakuwa J.M. Kikwete. Hii inaweza kubadilisha upepo wa kisiasa na kuongezea angalau kura kwa JK na CCM. Hapa la msingi zaidi ni kuwa Dk. Yahya inabidi aongeze mara dufu ulinzi usioonekana maana akianguka katika sherehe hizi uchaguzi utakuwa umeishia hapa. Mwenye habari zaidi, atujuze zaidi. :spider:
Bwana Mungu tunaemwamini ndiye atakayesimamia uchaguzi wa 2010, hakuna cha Ndumba wala wizi wa kura, wakirusha roho wachafu ili shaba tuone Dhahabu watarudi kwao kwa njia saba,
Dhahabu itabaki kuwa dhahabu, na shaba kuwa shaba
Laana zote na manuio na dhambi zilizofanya Tanzania kulaaniwa na watu wake kulaanika imeshaondolewa kwa damu ya Yesu Kristo.
Huyu ndiye Mungu ninaemtegemea na alisema katika Neno lake Iwapo mtu mmoja atasimama kwa ajili ya Nchi nitaiponya nchi.
Nami nasimama kwa ajili ya Tanzania Ee Bwana ukapata kuiponya..
Tunataka nchi yetu uliyotupa ya asali na Maziwa.....
Tunataka watu kutoka mbali watuletee dhahabu na Almasi......
Zaburi 17: 14( Ee Bwana kwa mkono wako uiokoe Tanzania na watu wa dunia hii, ambalo fungu lao li katika maisha haya. Matumbo yao wameyajaza kwa hazina yako. Hushiba wana huwaachia watoto wao akiba zao.
Hii ni IMANI YANGU NA SI UDINI, WOTE WANAOAMINI KWA IMANI HII NA WASIOAMINI BALI WANAITAKIA TANZANIA MEMA WASEME AMEN.