Kura za wamachinga ni haramu

Kura za wamachinga ni haramu

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Muda wote mwanasiasa wa Tanzania huwa anafikiria uchaguguzi, kura na wapiga kura kiasi cha kuwafanya watafute hata kura haramu kwa njia haramu. Miongoni mwa kura haramu hizo ni kama zile za kushindwa au kuacha kutekeleza mipango yenye maslahi mapana kwa watu wengi na kwa taifa kwakuhofia kukosa kura za kundi fulani hata kama kundi hilo linafanya makosa. Barabara ya Msimbazi Kariakoo imebanwa sana kutokana na ujio wa mabasi yaendayo haraka, pamoja na ufinyu wa barabara hiyo wamachinga nao wametandaza bidhaa zao kweñye njia za wapita kwa miguu kiasi cha kusababisha msongamano mkubwa sana unaosababisha watu watumie barabara za magari kupita, kusukumana na kuibiana kwa urahisi. barabara na kariakoo nzima inanuka mikojo na takataka kutokana na ukosefu wa miundombinu ya taka ngumu na vimiminika kama mkojo na haja kubwa. Utafutaji wa kura kwa style hii sio sawa. Miji ya wenzetu ni misafi na kura wanapiga na mshindi anapatikana, kulikoni sisi? Tanzania tunayo ardhi ya kutosha kwanini utafutie wavamizi maeneo ya kufanya biashara? unachopaswa kufanya ni kusema hapa haparuhusiwi lakini pale panaruhusiwa kwa kufuata utaratibu huu na ule basi. Mbona Machinga hawaendi kwenye viwanja vya mlimani city au Ikulu kutandika chini biashara zao?
 
Back
Top Bottom