Kurejeshwa kwenye Cabinet kwa mawaziri Simbachawene na Mwigulu - tatizo ni bulb au holder?

Hiyo inaitwa kampa kampa tena,hakuna tatizo hapo.Tatizo sio holder wala bulb ilikuwa ni loose connection tusha ifix.
 
Kina Rizone sijui wana gundu gani, mana jamaa ni msomi wa sheria tena ana Masters kabisa
 

Mkuu kipindi cha Corona Hii. Acha ujinga. After all humpendi JPM so maamuzi yake kwa Nini unahangaika Nayo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Holder ndo mbovu
 
Sisi wananchi ndio mazwazwa na watawala washatuona kama wanaweza kufanya wanavyojisikia na tusifanye lolote!

Angalia mambo yanayoendelea hapa nchini lakini tunapiga kelele mitandaoni tu.. Hakuna anayechukua hatua,tumekua waoga! Hii nchi sijui tulilishwa nini? Kuna wapuuzi wachache wanafanya wanavyotaka,wanatumia vyombo vya usalama ambavyo vinalipwa kwa kodi zetu kutunyanyasa!

Kuna viongozi mwezi huu wa ramadhani nao wamefunga! Wengine leo jumapili na kanisani wameenda! Hivi ni Mungu yupi wanaomuabudu? Tatizo hapa sio holder wala bulb bali mfumo mzima ndio tatizo na ndio maana mara leo iwake kesho izime!
 
nunua revolver ndugu!
 
Simbachawene hakuondolewa kuwa na kimbukumbu

Nchemba kichwa chake kipo vizuri naona leo ufipa hamlali mnalialia tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Kichwa cha huyo Nchemba wakati anaondolewa kwa kejeli hakikuwa vizuri? Ww sema tatizo ni holder ama bulb, acha maelezo mengi.
 
Mwigulu ni mchapakazi ni kwamba alipumzishwa tu na kazi inaendelea

Kama unampumzisha mchapakazi, hapo tatizo ni holder ama bulb? Sisi tunaoamini kuwa tuna rais, lakini rais asiye na uwezo wa kazi ya urais bado tuko sahihi sana.
 
toka nimezaliwa sijawahi kusikia popote duniani eti waziri wa katiba na sheria ambaye hana elimu ya sheria...haya ni maajabu duniani!.

kwa uelewa wangu mdg, baadhi ya wizara ni lazima waziri awe na taaluma husika

Sent using Jamii Forums mobile app

Kichekesho ni pale aliyesomea sheria anasimamia michezo, na aliyekariri mambo ya uchumi anasimamia sheria! Halafu eti hicho kichwa ndio kinatamba kuwa kitaua upinzani kutokana na utendaji wake mzuri!
 
Chodomo mmepata pa kusemea. Tatizo lenu huwanasubiri hadi watawala wafanye kitu ndo muanze kuropoka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Pitia vizuri michango ya huku ndani toka huyo jamaa kaingia madarakani kama aliwahi kupata sifa zozote. Nyie mliolishwa sifa za kijinga ndio mlidhani jamaa yuko vizuri, ila mmeanza kumjua vizuri mkiwa mmechelewa.
 
Tatizo ni holder
 
Tatizo ni holder ndiyo maana bulb zinaungua.Tuna utawala wa kipekee duniani.
 
Wamekwisha kuwa refined cholesterol free now.
 
Unapokuwa na vibovu tupu na huwezi kununua vipya, basi unaangalia tu kati ya vile vibovu chenye unafuu kidogo hichohicho unachukua kusogeza siku.
 
Kichekesho ni pale aliyesomea sheria anasimamia michezo, na aliyekariri mambo ya uchumi anasimamia sheria! Halafu eti hicho kichwa ndio kinatamba kuwa kitaua upinzani kutokana na utendaji wake mzuri!
Upinzani ni itikadi ni iman huwezi iuwa physical kwa kutumia polisi, wasiojulikana, DPP,manunuzi,nk ni lzm utumie spiritual technics
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…