moyafricatz
JF-Expert Member
- Nov 27, 2015
- 2,904
- 4,902
Tarehe 11 Agosti, 2021 Dare es Salaam.
Kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa UVlKO-19 Duniani, ambapo Tanzania ilipata kisa cha kwanza cha mgonjwa wa UVlKO-19 tarehe 16 Machi 2020, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo upimaji wa wasafiri wanaoingia na kutoka nchini.
Aidha, Serikali imeendelea kutoa miongozo mbalimbali ikiwemo mwongozo wa Wasafiri (Traveler Advisory) na kuuboresha ili kuendana na mwenendo wa ugonjwa wa UVlKO-19.
Gharama za upimaji wa UVlKO-19 kwa wasafiri wanaotoka na kuingia nchini zinalipwa na wasafiri wenyewe kwa kiwango cha dola mia moja ($100) sawa na shilingi laki mbili na thelathini za kitanzania (Tsh kwa kipimo cha RT PCR na dola ishirini na tano ($25) sawa na shilingi elfu hamsini na saba na mia tano za kitanzania (Tsh 57,500/=) kwa kipimo cha Antigen RAPID TEST kwa wasafiri wote.
Mnamo tarehe 04 Mei, 2021 Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya ziara ya kikazi nchini Kenya.
Kufuatia ziara hiyo, Mhe. Samia Suluhu Hassan, alitoa maelekezo ya kutatua kero ya vibali na upimaji wa UVIKO-19 kwa abiria wanaovuka kupitia mipaka ya nchi kavu kati ya Kenya na Tanzania. Mheshimiwa Rais alielekeza Mawaziri wa nchi zote mbili wakutane ili kumaliza changamoto hizo.
Kufuatia agizo hilo la Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto (WAMJW) imepitia upya gharama ya upimaji wa ugonjwa wa UVIKO-19 kwa wasafiri wa wote nchini na kutafuta namna ya kupunguza gharama hizo ili kuwezesha wasafiri wengi kupata huduma hii muhimu.
Kutokana na mapitio pamoja na uchambuzi wa gharama za upimaji wa ugonjwa wa UVIKO-19, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepunguza gharama za upimaji wa ugonjwa wa UVlKO-19 kutoka dola za Marekani 100 kwenda dola 50 kwa kipimo cha RT PCR na kuondoa gharama za kipimo cha Antigen RAPID TEST mipakani isipokuwa viwanja vya ndege ambapo wasafiri watalipia dola 10 tu kwa kipimo cha Antigen RAPID TEST.
Sababu ya kushusha gharama za upimaji wa UVlKO-19 inatokana na gharama za uendeshaji kutengwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia bajeti yake ya mwaka wa fedha 2021/2022.
Kwa wasiojua kiswahili ,summary hii hapa chini ya kizungu.
1.RTPCR Test Charges reduced from $100 to $50
2.Free Rapid Test for Truck Drivers at Border
3. Return Air travellers Rapid test from $25 to $10
Alamsiki