Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Binafsi naonelea ni vizuri zaidi kurekebisha Katiba yetu kuliko kuiandika upya.
Sababu zangu:
1- Katiba ni waraka wa kihistoria hivyo ni vyema baadhi yake kuachwa kama ilivyo itukumbushe tulikotoka.
2- Si Katiba yote ni mbaya, wala si nusu yake. Why re-invent the wheel?
3- Gharama za kuandika katiba mpya zinajulikana. Hivi nisemavyo mabilioni yamekwshatafunwa kwa muswada wa Kikwete. Tuanze upya? Jamani, waoneeni huruma Watanzania!
4- Wanaojua historia watakuambia afadhali kurekebisha ulichonacho kuliko kuanza upya. Uchumi wa Ufaransa, Urusi, hadi leo hauna umakini kama ule wa Uingereza (ingawaje nchi hizo ni tajiri zaidi kwa rasilimali). Wanahistoria na Wachumi wanaona sababu kubwa ni kuwa nchi mbili hizo zilifanya mapinduzi na 'kuanza upya' ukilinganisha na Uingereza ambayo ilirekebisha tu aina yake ya utawala. ( Kwa mantiki hiyo, angalia Kenya na Tanzania: sisi tulibomoa kila kitu tukaanza upya!).
5- Marekani ndiyo nchi iliyofanikiwa zaidi kwa nyanja zote ( haki za binadamu, utawala bora, ufanisi wa uchumi, teknolojia nk). Nchi hiyo inarekebisha katiba yake, haiandiki upya! Tangu katiba ya kwanza ya Marekani, 4 March, 1789 kumekuwa na marekebisho 33 ya Katiba hiyo.
Marekebisho ya kwanza yametokea hata kabla mwaka haujaisha tangu katiba hiyo ibuniwe! Marekebisho ya tarehe 25 September 1789 yaliyompa Mmarekani haki ya kubeba, kumiliki silaha.
Kabla ya hapo ilikuwa marufuku! Baadhi ya vipengee muhimu vya Katiba hiyo kwa kweli vimekuja kwa njia ya Urekebishaji: Marekebisho ya 13 ya 31 January 1865 ndiyo yaliyoharamisha utumwa na uuzaji wa watu nchini humo! Marekebisho ya 21 ya 18 December 1917, yametoa ruhusa watu kutengeneza na kuuza pombe!
Hii inaonesha wazi kwamba si lazima ubomoe nyumba yote ndiyo utengeneze! Hili liko wazi isipokuwa kwa walaji na wasiojali matumizi ya kodi za Watanzania.