Kurithi majina ni chanzo cha koo tajiri kuwa tajiri na koo masikini kuwa masikini

Kurithi majina ni chanzo cha koo tajiri kuwa tajiri na koo masikini kuwa masikini

Kiplayer

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
1,180
Reaction score
1,964
Tunaporithishana majina huwa tunarithishana vingine vingi vinavyoambatana na mwenye jina linalorithiwa. Inachanganya sana, hii iko vipi wataalam wa mambo?

Lakini nimeshuhudia koo nyingi zinafana kizazi kimoja kwenda kingine. Mtazamo wangu majina tunayorithi huwa yanaambatana na tabia, hali aliyokuwa nayo mmiliki wa awali wa jina. Ndio maana koo tajiri zimeendelea kuwa tajiri na masikini zimeendelea kuwa masikini.
 
Hivi koo ikiwa tajiri inkua na nini na koo ikiwa masikini inakua na nini... mfano mwenye ngombe wengi na mwenye magari mengi nani tajiri.? au tuseme mwenye chakula na mwenye hela ya kununu chakula nani tajiri?

Ni hivi... utajiri ni hali ya kufikirika na umasikini ni hali ya kutoridhika.. sasa majina yanaingiaje hapo.. isipokua kuna uhusiano wa majina na hali ya maisha utakauoyaishi napo ni kama jina ulilopewa linakuhusu au halihusiani na wewe.
 
Tunaporithishana majina huwa tunarithishana vingine vingi vinavyoambatana na mwenye jina linalorithiwa. Inachanganya sana, hii iko vipi wataalam wa mambo? lakini nimeshuhudia koo nyingi zinafana kizazi kimoja kwenda kingine. Mtazamo wangu majina tunayorithi huwa yanaambatana na tabia, hali aliyokuwa nayo mmiliki wa awali wa jina. Ndio maana koo tajiri zimeendelea kuwa tajiri na masikini zimeendelea kuwa masikini.
👍👍👍 Hii ni kweli kabisa sikupingi hata chembe.

Majina ya kurithi yanabebaga sana hatma ya maisha ya wanaorithishwa
 
Ulaya mtu anaitwa Stone na anatoboa Afrika Njemba inaitwa Suleiman ( Mfalme na Boss kweli ) ila ndo kajisajili Meridian na M-Bet ili aishi vizuri.

Jina lina kawaida ya kukushambulia Hadi ufanane nalo.
 
Ona matajiri ni wale wanaorithi nyenzo na mifumo ya kufanya kazi na kuuza huduma na bidhaa kwa watu wengi

Masikini ni wale wamejirithisha mifumo ya kufanya kazi na kununua huduma na bidhaa kutoka kwa watu wengine

Jina, sijui pesa au mali pekee hazitunzi huo utajiri. Na kuongezea tu: ni akili ya kimaskini kudhani kuwa kuwa tajiri kunategemea kile, atapokea na kurithi kwa maana ya mali na pesa ghafi.
 
Hapo ligi kuu uingereza Kuna wachezaji wanaitwa
Cash,stones, drinking water, etc
Vip hapo unazungumziaje

NB:hao wanacheza timu kubwa na wanapesa
 
Hapo ligi kuu uingereza Kuna wachezaji wanaitwa
Cash,stones, drinking water, etc
Vip hapo unazungumziaje

NB:hao wanacheza timu kubwa na wanapesa
Inategemea jina limerithiwa kutoka kwa nani kama sio la kurithi hao Wana maisha yao binafsi.
 
Back
Top Bottom