Kurt Gödel: Mwanasayansi aliyekufa kwa njaa

Kurt Gödel: Mwanasayansi aliyekufa kwa njaa

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Upo mstari mwembamba sana kati ya akili (intelligence) na uchizi (craziness). Mara nyingi watu wenye akili nyingi sana huwa na uchizi fulani. Ukipata nafasi ya kuwasikiliza machizi waliopo mtaani utagundua wana akili nyingi sana hadi wewe unaweza kujiona ndio chizi.

Waswahili husema akili zikizidi zinakua uchizi. Bila shaka hiki ndicho kilimkuta Mwanahisabati maarufu Kurt Gödel, Mjerumani aliyehamia Marekani kukwepa mkono wa chuma wa Adolph Hittler, kama ilivyokua kwa Albert Einstein.

Godel alikuwa na uwezo mkubwa wa akili tangu akiwa mdogo na alivushwa madarasa kadhaa kutokana na kuyamudu vizuri masomo. Alijiunga na chuo kikuu cha Vienna akiwa na miaka 17 tu (huku Afrika wengi wapo form 3B).
Alichaguliwa kusomea Shahada ya Fizikia lakini alibadili na kusomea hisabati (Mathematical logic).
_
Alihitimu shahada ya kwanza akiwa na miaka 20 na alipojiunga na shahada ya uzamili ilionekana uwezo wake ni mkubwa sana. Yani alikua mbele ya nyakati. Ikabidi wampe udahili wa kufanya PhD. Kwahiyo akafanya PhD bila kusoma Masters kutokana na uwezo mkubwa wa akili.

Hapa TZ tunaye mtu mmoja wa aina hiyo. Anaitwa Joyce Ndalichako. Baada ya kuhitimu UDSM alipata ufadhili wa kwenda kusoma Masters University of Alberta, Canada. Lakini alionekana yupo mbele ya majira. Kwahiyo wazungu wakampeleka Ndalichako moja kwa moja kufanya PhD badala ya Masters.

Anyway turudi kwa Godel. Alihitimu PhD yake mwaka 1929 akiwa na miaka 23 tu, na aligundua incompleteness theorems in Mathematics. Godel anatajwa katika orodha ya watu 100 duniani waliokua na akili sana karne ya 20 (100 Greatest Minds of the 20th Century).
_
Mwaka 1940 alihamia Marekani. Alifanya kazi kwa karibu na Albert Einstein, na alimkubali sana.

Lakini Godel hakuwahi kuamini chakula cha mtu mwingine zaidi ya mkewe Adele Nimbursky. Aliamini akila chakula kingine atawekewa sumu. Alikua akiamini kuna watu wanamuwinda wamuwekee sumu (obsessive fear of being poisoned)
_
Mwaka 1977 mkewe aliugua sana na kulazwa hospitali kwa muda mrefu. Godel akakosa mtu wa kumpikia. Akagoma kula chakula kingine chochote hadi akafariki dunia kwa mwili kudhoofu (malnutrition and inanition caused by personality disturbance). Yani aliogopa kufa kwa sumu akaamua kufa kwa njaa. Alizikwa huko Princeton, New Jersey, na Rais Richard Nixon alieleza kusikitishwa sana na kifo chake.

Mwandishi David Cycleback alimuelezea Godel kama mtu mwenye akili nyingi lakini mwenye maisha ya kustaajabisha katika makala yake "The Strange, Brilliant Mind of Kurt Godel" iliyochapishwa katika gazeti la New York Times mwaka 1996.

104095654_3076915449066793_8861967463372961275_o.jpg

[Pichani Kurt Godel akiwa na Albert Einstein mwaka 1948 katika taasisi ya Saynsi na utafiti ya Princeton, New Jersey].​

Credit: G. Malisa
 
Huyo pamoja na akili zake alijitendea dhambi mwenyewe, aliogopa kifo cha sumu lkn kafa
wa njaa huo ni upunguani wake hata ingawa alikuwa mwenye akili
 
Huyo pamoja na akili zake alijitendea dhambi mwenyewe, aliogopa kifo cha sumu lkn kafa
kwa njaa huo ni upunguani wake hata ingawa alikuwa mwenye akili
 
Kumbe akili nazo zikizidi ni majanga, nasikia mzee wa gravitational force sir isaac newton alikuwa anasahau kula na mwenyewe muda mwingine eti alikuwa anasahau jina lake.
 
Back
Top Bottom