Kurudi katika mzunguko wa hedhi baada ya kujifungua kwa njia ya operation

majeshi 1981

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2013
Posts
2,090
Reaction score
812
Wakuu naombeni msaada wenu, mke wangu alijifungua mtoto mwaka mmoja uliopita kwa njia ya operation lakini hadi sasa haoni siku zake.

Hii imemletea hofu kubwa sana ingawaje hataki kunieleza lakini naona kabadilika na kupungua sana, pamoja na kuendeleza kiapo changu kwake cha kumpenda muda wote wa raha na shida lakini naona hataki kubadilika.

Naogopa hata kumwambia nimpeleke hospitalini kucheki tatizo lakini nahofia kumwongezea tatizo pindi akipewa majibu ambayo ni negative kwake na kwangu.

Je? ni kawaida kukaa muda wa mwaka mmoja bila hedhi baaada ya kujifungua? Wakuu, tatizo hapa linaweza kuwa ni nini? Naombeni ushauri wenu kwani mke wangu ni mpole sana na sitaki hauzunike hata kidogo.
 
Bado ananyonyesha? Mimi nimezaa normal na kwa CS lakini huwa napata hedhi after one year kujifungua nadhani ni mwili wangu ulivyojiadapt maana niienda kwa DR. aliniambia since nanyonyesha nisiogope ni hormonal changes itakuja tu. Ila kama hanyonyeshi subiri wataalamu zaidi wakujulishe
 
Ila kuwa makini maana mimba zinaingia kama kawaida maana hata mimi watt wangu niliwazaa karibu karibu kwa sababu ya hii shida.
 
bado ananyonyesha dada angu!
 
Ila kuwa makini maana mimba zinaingia kama kawaida maana hata mimi watt wangu niliwazaa karibu karibu kwa sababu ya hii shida.

nashukuru kwa ushauri, ila hofu yangu kuu ilikuwa isije ikawa walimwondoa kizazi bahati mbaya wakati wa CS
 
kawaida mi sijazaa kwa operesheni ila nimekaa miesi tisa
 
Ni kawaida kama ananyonyesha, unakuta mwingine haoni siku zake mpk atakapoacha kunyonyesha. So ni hormone tu za mtu mana watu wanatofautiana, mf. Mm mtoto wangu ana miezi 5 nisharudia siku zangu, uwe na amani kaka!!
 
ahsante sana, inatia hofu sana kwa jinsi ninavyompenda na anavyoonekana kukosa amani kabisa
 
Ni kawaida kama ananyonyesha, unakuta mwingine haoni siku zake mpk atakapoacha kunyonyesha. So ni hormone tu za mtu mana watu wanatofautiana, mf. Mm mtoto wangu ana miezi 5 nisharudia siku zangu, uwe na amani kaka!!

nashukuru sana!
 
Mkeo anakosa amani kwa mambo mengine sio ilo, Mkague mtoto kafanana na wewe? Isije ikawa umeveshwa na huko kupenda kwako
 
Mie sijazaa ila mama angu yeye akijifungu akaanza kunyonyesha baasi mpk atakapoacha kunyonyesha ndio ataona siku hata akinyonyesha miaka mi3 basi ujue na siku haoni ila akiacha tuu amalizi siku 7 anaanza kuona siku zake. Kwa mujibu wa maelezo yake ktk story za maisha but sasa kashafkia ukomoo aoni tena siku coz yupo kwenye 65'yrs
 
Hakuna shida hapo baadhi ya wanawake wakinyonyesha vizuri huwa hawapati siku zao hormone zinazorutubisha yai hushuka sana hivyo hapati hedhi.ndiyo maana breast feeding ni njia ya uzazi wa mpango.akiacha kunyonyesha atapa tu,kipindi hiki ndo kizuri kumpa haki yake
 
wewe mtoto, mama ako anajua unatembelea huku na kutoa siri zake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…