Kurudi kwa michango mbalimbali mashuleni. Je, Serikali imeshindwa kutekeleza sera ya Elimu bure?

Kurudi kwa michango mbalimbali mashuleni. Je, Serikali imeshindwa kutekeleza sera ya Elimu bure?

Dudukubwa

Member
Joined
May 13, 2021
Posts
26
Reaction score
28
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kumekuwa na wimbi kubwa la kuongezeka michango ya lazima katika shule za serikali, baadhi ya michango hiyo ni majengo, taaluma, madawati lakini watu wameenda deep zaidi hadi pesa za mitihani ya shule.

Hizi ni dalili tosha kabisa kwamba sera ya Elimu bure haitekelezeki.

Ndugu zangu kushindwa sio dhambi, dhambi ni kuendelea kudanganya kwamba umeshinda wakati umeshindwa.

Kama ilivyokuwa kwenye Corona, serikali itangaze RASMI KUACHANA NA ELIMU BILA MALIPO!

Sisi ni waungwana sana, kama tulivyokubali kwenye tozo kandamizi basi hata kwenye hilo tutakubaliana na serikali.

Kazi iendeleee!
 
Hakuna elimu Bure, ni wakati Sasa wa serikali kurudisha ada,
 
Michango ilishakuwa tabia ya hizo shule hivyo kuondolewa walimu wanahisi kama wamepungukiwa, ndio maana lazima wairudishe kwa namna yoyote ile, mkitaka iondoke moja kwa moja pandisheni mishahara ya walimu na muwalipe stahiki zao kwa wakati.
 
Mabadiliko siku zote hupingwa
Wanaochangisha hii michango wanaweza kusema JPM hayupo ila wasisahau serikali iliwaelekeza nini na aliyekua msaidizi wa JPM katika kupanga hayo mama SSH ndio Rais sasa
 
Back
Top Bottom