Kurudia mtihani wa kidato cha Nne kwa udhamini wa serikali je ni suluhisho la kufeli ?

Kurudia mtihani wa kidato cha Nne kwa udhamini wa serikali je ni suluhisho la kufeli ?

Mchokozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2012
Posts
215
Reaction score
29

Wana JF, nimesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari na magazeti kuwa serikali inaangalia uwezekano wa wanafunzi 60% waliofeli warudie mtihani na hata ikiwezekana walipiwe gharama za kurudia, je hii itakuwa ndiyo Muarobaini wa kufeli?
 
Mimi naona ni bora warudie mitihani na suruhisho litapatikana
 

Wana JF, nimesikia na kusoma kwenye vyombo vya habari na magazeti kuwa serikali inaangalia uwezekano wa wanafunzi 60% waliofeli warudie mtihani na hata ikiwezekana walipiwe gharama za kurudia, je hii itakuwa ndiyo Muarobaini wa kufeli?
Mchokozi watarudia mtihani bila kuandaliwa? Mfano ambaye hajasoma somo la biology tokea ajiunge Form I hata akirudia mara kumi atafaulu? na kama wataandaliwa; idadi ya wanafunzi kwa shule ni kubwa sana kiasi kwamba hakuna nafasi "facility" ya kuwaweka na tatizo la upungufu wa walimu liko pale pale
 
Last edited by a moderator:
Serikali imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa 240,903 wa kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni, kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.

Source: Habari Leo.
 
Hiyo siyo fair inabidi warudie wote wanaotaka na si kuchagua kundi moja
 
sasa na sisi tuliopata zero miaka ya nyuma watatufanyia nini mbona ina uamuzi ambao sio fair kabisa.Tunateswa na zero zetu leo hawa wanafanyiwa favor.Hiii serikali ni matatizo matupu yaani.
 
Bora warudie au wasahishe upya kuna watoto wanauwezo sana, wamepata ziro kuna ambao walikuwa hakuna kitu kabisa kichwani mpka walimu wanashanga wamepata dv 2.
 
Waliosomea shule za anasa nao wanarudia?, mimi nafikiri watafute wale waliosomea shule za serikali tu. Waliosoma private watajua wenyewe kwa maana wazazi wao waliwatafutia mazingira mazuri lakini wakafeli.
 
ama wapelekwe fm5 na wao watapimwa hukohuko zile K tatu kama hawa wa fm1 ..kweli elimu imekuwa ghari sana hapa Tz
 
Hivi wangefaulu sana serikali ingerudia mitihani hiyo? Unategemea ninicha zaidi kwa hao walioandika matusi na wasiotaka kujiandaa lakini wanapenda kufaulu.
Kama ni kweli siasa imeanza kazi yake, na huo ni utumiaji mbovu mwingine wa pesa za wavuja jasho, mnetumia pesa hizo kuboresha mashule na vifaa vya kufundishia bila kusahau madai ya walimu yalipwe.
 
kwa hiyo wrudie,tuchakachue wafaulu, wazazi wasio na akili watupigie kura kwisha
 
Kwani kilicho wafelisha ni ada ya mtihani au ................
UPEMBUZI YAKINIFU UNAHITAJIKA KUBAINI CHANZO CHA TATIZO.
 
Hata wasipo chakachua watanzania haichukui wiki watakuwa wamesha sahau...watakuwa wanazungumziaelimu ya John Mnyika na Nape....
kwa hiyo wrudie,tuchakachue wafaulu, wazazi wasio na akili watupigie kura kwisha
 
serikali inajua tatizo na kila mwananchi analitambua hilo,hawana sababu ya kurudia mtihani ili kujisafisha.
Swali,je ni kila matokeo yatakapokuwa mabaya watafanya hivyo?
Au kiini macho kwa ajili ya kujiandaa na kampeni za 2015,ili waje waseme serikali yenu ni sikivu ndio maana ikawapa nafasi tena ya kurudia mitihani vijana wetu.
 
Back
Top Bottom