Kurudisha nyuma ODO kilometer

Kurudisha nyuma ODO kilometer

deecharity

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2010
Posts
932
Reaction score
506
Habari wakuu, naomba kuuliza na kupata ukweli juu ya hili. Je ni kweli hapa Bongo kuna watu wanaweza kurudisha nyumba ODO kilometers? Na hasa hawa watu wa showrooms, au ni uongo unaelekea kuwa ukweli?
 
deecharity, Baadhi yao wanafanya hivyo. Hata wanaouza Magari yaliyotumika hapa nchini baadhi yao wanarudisha nyuma km, unaponunua Kabla ya kulipia upate file la gari wakati linakuja hapa nchini itakusaudia kufahamu kama hizo km zimechakachuliwa ama la.

Husichakachue, uza na km zake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo, unaweza..iwe digital ama ya kawaida, tena ya kawaida hata wewe unaweza. Digital inabidi upitie viprocess vya kiutaalam wa fundi umeme.

Bottom line, inasemekana, haijawahi kuthibitishwa kuwa baadhi ya wauzaji wa magari hapa nchini hasa kwenye yadi wanafanya hivyo, narudia haijathibitishwa

na bei invyosemekana ni kuanzia tzs 50,000 kwa digital
 
Kuongezea hapo juu, unaponunua gari liwe yadi ama kwa mtu,,,, tafuta fundi mzuri, wawe wawili mmoja wa umeme na mmoja wa engine, kwani shilingi ngapi?.....huna hasara ukiweza kununua kitu kilichothibitishwa, usiangalie mileage, lakini wakikagua VIZURI, kila kitu ndipo uridhike na kuondoka na gari.

Hivi unajua vile vi screw vya dashboard mtaalam anajua akiangalia anajua hii imeguswa, hata bodi kama imepigwa rangi nzuri na kung'arishwa akicheki anajua imepigwa ama hata dalili za kutu
 
Kuna matapeli wa Magari wanarudisha nyuma cluster tena wapo wanaotumia program Fulani ya computer kurudisha nyuma na ipo njia nyingine ya kutumia manual

Screenshot_2019-07-16-15-50-16.png
 
Ni kweli mkuu magari mengi sana yanarudishwa kilomita nyumba mfano niliwahi iona Crown ya 2008 GRS201 wakati inakaguliwa bandarini ina km 189,000 ilivyofika mikononi mwa watu inauzwa ina km 72,000 vile vile Mark X..kibao
 
Kwaio dawa ya kuthibitisha kama gari ni genuine au la mwambie anaekuuzia gari akupatie file la gari..lilie lililolipiwa kodi bandarini i.e TZDL-18-xxxxxx hapo utaona inspection certificate ya TBS i.e TBS waliikagua hio gari ikiwa na km ngapi...
 
Mambo hapo haya, drilling machine inafungwa hapo wanavyojua mafundi, wakiiwasha ikianza kuzunguka kilometa zinarudi.

Heri uagize gari lako mtandaoni
 
Hata hii tbs document ya inspection inaeditiwa vyema kabisa, dawa ni muagize gari direct Japan, ongea na agent akutafutie garage nzuri,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom