Kurudishwa kwa January Makamba ni dalili tosha kwamba Rais Samia ameanza kuliogopa kundi linalompinga ndani ya CCM!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Labda uwe mtu poyoyo sana wa kufikiri ndio hutaelewa hii move ya Raisi Samia ya kuanza kusema anawarudisha kina January Makamba kwa mama. Hii sio bure, na kama January anafikiri kwamba anachofanyiwa na Raisi Samia ni hisani, basi yeye ni one of the most naive, pathetic and disgusting politicians kuwahi kutokea katika nchi hii, kuweza kuimeza move ya Samia, hook, line and sinker kirahisi kiasi hiki, especially anapoanza kuimba "nampongeza mama kwa kuchaguliwa na Mkutano Mkuu kuwa mgombea wa CCM"!

Anaefaidika na "kurudishwa kwa mama" hapa wala sio January, bali ni Raisi Samia. January Makamba anaonekana kufurahia. Labda pia ni kwa kuwa anajua kilichomfanya aondolewe uwaziri (kuna mtu alisema aliondolewa uwaziri kwa kosa ambalo ingekuwa Tanzania ni China angehukumiwa kifo!). Na pia January anaweza kuliona hili katika kutengeneza matumaini yake ya 2030. Ila asisahau kuna kina Mwigulu pia wenye matumaini hayo!

Samia anajua wazi kwamba kilichofanywa na Mkutano Mkuu hakikukubaliwa na vigogo wengi ndani ya CCM, kutia ndani kina January Makamba, ambao walijua wazi kilichofanywa na Mkutano Mkuu kililenga kuwapiga chenga katika mkakati wao. Tayari kulikuwa na vuguvugu ndani ya CCM la kujaribu kutompitisha Samia kama mgombea wa CCM wa 2025, na hii ndio iliyofanya Samia na kundi lake kutumia Mkutano Mkuu "kujipitisha" kuwa wagombea wa CCM.

Samia anachofanya sasa ni kutumia mbinu ya "divide and weaken" kwenye hili kundi la ndani ya CCM ambalo anajua lina nguvu na linaweza kukwamisha ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu. Anaanza kuwavuta mmoja, akianza na kina January Makamba, kwa kutumia "emotional blackmail", eti "kurudi kwa mama". Na pia atawatupia vizawadi vingine vya uteuzi ili kuwatoa kwenye kundi la ndani ya CCM la "Samia Must Fall", ambapo kimsingi kufanya hivyo ni corruption. Kumteua mtu asiyefaa au aliyefanya kosa kubwa ili ufaidike na kuungwa mkono kwake ni rushwa.

Samia anajua wazi kwamba upinzani anaoukabili kulelekea uchaguzi Mkuu wa 2025 sio tu unatoka kwa wapinzani kama kina Lisu, bali kuna kundi ndani ya CCM lenye nguvu sana, ambalo linatia ndani watu wa karibu wa Magufuli waliowekwa kando, ambalo lilishajiweka sawa kupanga mkakati wa aidha asiteuliwe kuwa mgombea wa CCM au asishinde uchaguzi wa kuwa raisi. Sasa kikwazo cha kuteuliwa aliwapiga chenga kwa kutumia Mkutano Mkuu. Lakini Samia anajua wazi hiyo haitoshi. Na sasa anaanza "kuwarudisha kwa mama". Ni wale walio naive na waroho wa madaraka tu ambao watashindwa kuliona hilo na kukubali "kurudi kwa mama", na kuacha kuwa sehemu ya "Samia Must Fall" ndani ya CCM.

Upande wa pili kuwarudisha hawa watu kina January kunaweza kukamgeuka Samia. Ni kwamba bila kujua anawaweka zizi moja wale wote waliokamia kuwa maraisi 2030 - January, Mwigulu, Mchengerwa, Nchimbi, Biteko, Tulia, Ridhiwani, nk. Sasa ndani ya hawa, kuna baadhi kufanikiwa kwao 2030 maana yake Samia asifanikiwe 2025. Tusubiri yajayo!

Pia soma: Rais Samia: Nilimpiga kikofi January leo namrudisha kwa mama
 
Labda uwe mtu poyoyo sana wa kufikiri ndio hutaelewa hii move ya Raisi Samia ya kuanza kusema anawarudisha kina January Makamba kwa mama. Hii sio bure, na kama January anafikiri kwamba anachofanyiwa na Raisi Samia ni hisani, basi yeye ni one of the most naive, pathetic and disgusting politicians kuwahi kutokea katika nchi hii, kuweza kuimeza move ya Samia, hook, line and sinker kirahisi kiasi hiki!

Anaefaidika na "kurudishwa kwa mama" hapa wala sio January, bali ni Raisi Samia. January Makamba anaonekana kufurahia. Labda pia ni kwa kuwa anajua kilichomfanya aondolewe uwaziri (kuna mtu alisema aliondolewa uwaziri kwa kosa ambalo ingekuwa Tanzania ni China angehukumiwa kifo!).

Samia anajua wazi kwamba kilichofanywa na Mkutano Mkuu hakikukubaliwa na vigogo wengi ndani ya CCM, kutia ndani kina January Makamba, ambao walijua wazi kilichofanywa na Mkutano Mkuu kililenga kuwapiga chenga katika mkakati wao. Tayari kulikuwa na vuguvugu ndani ya CCM la kujaribu kutompitisha Samia kama mgombea wa CCM wa 2025, na hii ndio iliyofanya Samia na kundi lake kutumia Mkutano Mkuu "kujipitisha" kuwa wagombea wa CCM.

Samia anachofanya sasa ni kutumia mbinu ya "divide and weaken" kwenye hili kundi la ndani ya CCM ambalo anajua lina nguvu na linaweza kukwamisha ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu. Anaanza kuwavuta mmoja, akianza na kina January Makamba, kwa kutumia "emotional blackmail", eti "kurudi kwa mama". Na pia atawatupia vizawadi vingine vya uteuzi ili kuwatoa kwenye kundi la ndani ya CCM la "Samia Must Fall", ambapo kimsingi kufanya hivyo ni corruption. Kumteua mtu asiyefaa au aliyefanya kosa kubwa ili ufaidike na kuungwa mkono kwake ni rushwa.

Samia anajua wazi kwamba upinzani anaoukabili kulelekea uchaguzi Mkuu wa 2025 sio tu unatoka kwa wapinzani kama kina Lisu, bali kuna kundi ndani ya CCM lenye nguvu sana, ambalo linatia ndani watu wa karibu wa Magufuli waliowekwa kando, ambalo lilishajiweka sawa kupanga mkakati wa aidha asiteuliwe kuwa mgombea wa CCM au asishinde uchaguzi wa kuwa raisi. Sasa kikwazo cha kuteuliwa aliwapiga chenga kwa kutumia Mkutano Mkuu. Lakini Samia anajua wazi hiyo haitoshi. Na sasa anaanza "kuwarusisha kwa mama". Ni wale walio naive na waroho wa madaraka tu ambao watashindwa kuliona hilo na kukubali "kurudi kwa mama".
Porojo ni kitu cha hovyo sana hasa ukiwa umefikisika na kuishiwa kabisa hoja za kuibua jukwaani 🐒
 
This is beyond your brain power to comprehend. Acha wenye akili wa discuss. Hii siyo porojo, ni analysis na analysis can never be porojo kwa sababu inatokana na uwezo wa kuona na kuelewa ambao ni wazi wewe huna.
 
Labda uwe mtu poyoyo sana wa kufikiri ndio hutaelewa hii move ya Raisi Samia ya kuanza kusema anawarudisha kina January Makamba kwa mama. Hii sio bure, na kama January anafikiri kwamba anachofanyiwa na Raisi Samia ni hisani, basi yeye ni one of the most naive, pathetic and disgusting politicians kuwahi kutokea katika nchi hii, kuweza kuimeza move ya Samia, hook, line and sinker kirahisi kiasi hiki!

Anaefaidika na "kurudishwa kwa mama" hapa wala sio January, bali ni Raisi Samia. January Makamba anaonekana kufurahia. Labda pia ni kwa kuwa anajua kilichomfanya aondolewe uwaziri (kuna mtu alisema aliondolewa uwaziri kwa kosa ambalo ingekuwa Tanzania ni China angehukumiwa kifo!).

Samia anajua wazi kwamba kilichofanywa na Mkutano Mkuu hakikukubaliwa na vigogo wengi ndani ya CCM, kutia ndani kina January Makamba, ambao walijua wazi kilichofanywa na Mkutano Mkuu kililenga kuwapiga chenga katika mkakati wao. Tayari kulikuwa na vuguvugu ndani ya CCM la kujaribu kutompitisha Samia kama mgombea wa CCM wa 2025, na hii ndio iliyofanya Samia na kundi lake kutumia Mkutano Mkuu "kujipitisha" kuwa wagombea wa CCM.

Samia anachofanya sasa ni kutumia mbinu ya "divide and weaken" kwenye hili kundi la ndani ya CCM ambalo anajua lina nguvu na linaweza kukwamisha ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu. Anaanza kuwavuta mmoja, akianza na kina January Makamba, kwa kutumia "emotional blackmail", eti "kurudi kwa mama". Na pia atawatupia vizawadi vingine vya uteuzi ili kuwatoa kwenye kundi la ndani ya CCM la "Samia Must Fall", ambapo kimsingi kufanya hivyo ni corruption. Kumteua mtu asiyefaa au aliyefanya kosa kubwa ili ufaidike na kuungwa mkono kwake ni rushwa.

Samia anajua wazi kwamba upinzani anaoukabili kulelekea uchaguzi Mkuu wa 2025 sio tu unatoka kwa wapinzani kama kina Lisu, bali kuna kundi ndani ya CCM lenye nguvu sana, ambalo linatia ndani watu wa karibu wa Magufuli waliowekwa kando, ambalo lilishajiweka sawa kupanga mkakati wa aidha asiteuliwe kuwa mgombea wa CCM au asishinde uchaguzi wa kuwa raisi. Sasa kikwazo cha kuteuliwa aliwapiga chenga kwa kutumia Mkutano Mkuu. Lakini Samia anajua wazi hiyo haitoshi. Na sasa anaanza "kuwarudisha kwa mama". Ni wale walio naive na waroho wa madaraka tu ambao watashindwa kuliona hilo na kukubali "kurudi kwa mama", na kuacha kuwa sehemu ya "Samia Must Fall" ndani ya CCM.
Nasubiri akifika Tanga mjini Jimbo la Ummy mwalimu mambo yatakuwaje
 
Najiuliza Sasa afadhali yake ni ipi kati ya kuwarudisha au kuwaacha nje ya mfumo?

Haoni kama akiwarudisha ndyo anasogeza maadui ndani kwake?
 
Hizi ni porojo za kijinga. Mkutano mkuu ukishafanya azimio lake hakuna yeyote anayeweza leta figisu tena. Makamba na wenzake hawana uwezo wa kufanya lolote dhidi ya mgombea urais wa CCM Dr Samia. Hilo genge unalodhani lipo ndani ya CCM wasithubutu kuchezea sharubu za Simba.
 
Jiulize, kwa alivyomchezesha sindimba January Makamba, amemweka karibu kuwa adui yake au kuwa chawa wake?
Mimi naamini yule ni adui yake sikuzote, ila kama anategemea awe chawa wake basi awe makini maana January sio fala kukubali kutumika kwa maslahi ya Mama na target zake kuelekea uchaguzi.
 
Hii nchi ni ya kijinga haswa, yaani tunaishi kwa hisani ya Rais
Yaani tuna tatizo moja kubwa sana, na ni wenye akili tu wanaoliona na kuelewa tunakabiliwa na nini. Watanzania wengi leo wamekuwa wajinga kuliko wakati tukipata uhuru! Maradhi tumejitahidi kuondoa, umasikini pia, lakini ujinga tulikazania kufikiri kuondoa ujinga ni kujua kusoma na kuandika, kumbe kwa wengi kujua kusoma na kuandika kumewafanya kuwa wajinga hata zaidi! Na kadiri tunavoendelea katika kusambaza tasnia ya habari kama TV, Yutube, TikTok nk, ndivyo tunazidi kuwa na wajinga wengi zaidi.
 
Hizi ni porojo za kijinga. Mkutano mkuu ukishafanya azimio lake hakuna yeyote anayeweza leta figisu tena. Makamba na wenzake hawana uwezo wa kufanya lolote dhidi ya mgombea urais wa CCM Dr Samia. Hilo genge unalodhani lipo ndani ya CCM wasithubutu kuchezea sharubu za Simba.
Sasa umeona hii thread imekataa hilo au imesema Samia kishawapiga chenga kupitia Mkutano Mkuu? Ndio maana uliibuka na F nyingi, huna uwezo wa kusoma na kuelewa kitu
 
Back
Top Bottom