Kurugenzi ya Habari Ikulu ifafanueni vizuri 'Vyeti Feki' nao 'Kulipwa' kwani huku Mitaani Mbwembwe na Hofu zimetawala

Kidogo nimekuelewa kwa Hoja tukuka.
 
Hehehehe.

Unajipa umuhimu usiokuwa nao. Takataka kabisa.

Sasa wewe hata ukinifahamu utanifanya nini wewe mbwiga??
Ukitoka hapo utapitia njia ya kule nyuma kama unaenda Silver Pipe ( Hotel ya Hanspoppe ) ili utokee pale Triple Seven au utapitia hii ya hapa Jirani na ulipo ( mlipo ) Lugalo Golf Court ili ukatokee zako Kawe?
 
Kwanza mimi napendekeza hiyo mifuko iondolewe kila mmoja awe anatunza kilichochake. Kama nimeweza kutunza mke wangu kwa miaka 20 sasa, siwezi kushindwa kujitunzia mwenyewe akiba ya uzeeeni. Hao wahanga wa vyeti feki walipwe mafao yao. Pia sisi ambao serikali inaamin tuna vyeti safi lakin kichwani hatuna kitu basi ituruhusu tuanze kujiwekea akiba zetu wenyewe. Naomba kuwasilisha.
 
Kabisa hata mie naunga mkono hoja, hawa ni binadamu kama wengine, je ndo tuseme hata wabunge waliopita kwa kuiba kura wasipate kiinua mgongo?
Maana wapo wengi tu na madiwani pia.
Mama awe na huruma ktk hili.
 
Sheria inasemaje?
Mbona mnatoana macho bila sababu?
Tafsiri ya sheria ifanye kazi.

Pia point ya double standard ni muhimu kuizingatia, kwa nini zoezi la vyeti fake halikugusa baadhi ya kada?!
Ukitaka mbwai na iwe mbwai kwa wote, sio kwa kundi fulani tu.
 
Yes; there is some controversy. This needs clarification.
 
This issue is similar to demanding a kilo of flesh without blood. The president has to apply the concept of "creative accounting or dying a little" to resolve the dilemma.
 
Usisahau: Na "PhDs" nyingi ni fake.
 
Fruits of a poisonous tree
 
Huwezi chukua zile fedha bila hukumu ya mahakama. Serikali itafata utaratibu upi kuzitoa kwenye account za wahusika kwenye mifuko ya jamii?

Serikali ikizitaka zile fedha iwashtaki, mahakama itoe hukumu ya kutumia hizo fedha kuwa fidia kisha wanaweza zichukua kwa kibali cha mahakama. Kinyume na hapo serikali labda itumie unyang'anyi.

Tatizo ni kwamba mahakama ikijiridhisha kuwa serikali ilifahamu mapema juu ya uwepo wa hawa watu na wakaendelea kuwa watumishi basi hukumu inaweza kuwa tofauti kabisa.
 
Kuutetea Uhalifu na Wahalifu ni Ujuha.
Uhalifu ni pamoja na kuchukua fedha bila hukumu ya mahakama au kibabe.
Kama tumeamua kufuata sheria basi tuzifate hata kwenye kutaifisha hizo pesa. Washtakiwe mahakama itoe hukumu inayoruhusu utoaji wa hizo pesa kwenye accont za watu husika kwenye mifuko ya jamii.
 

 
Kuna Watu nilikuwa nikiwaheshimu sana hapa JamiiForums hasa kwa Michango yenu ila taratibu sasa kwa kuja na Hoja zenu zenye Huruma za Kinafiki kwa 'Wahalifu' niseme tu kuwa nitaanza Kuwadharau na kuwaona ni 'Hopeless' wakubwa tu.

Wewe katika kusoma kwako koteee haujawahi kufake?
 
Kuna umuhimu wa kulitolea ufafanuzi hilo swala ni kweli mtaani kuna mkanganyiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…