Kusaga ampigia simu Diamond Platnumz akiwa live Clouds FM

Sikuzote walikuwa wanaupiga ule Yope original, wameshikwa pabaya[emoji1][emoji1]
Aliyeshikwa pabaya nani!? Maana ukisema hao watangazaji, hao wanafata amri za uongozi na ukisema Kusaga , huyo ni mbia mwenza wa Diamond.
 
Joe Kusaga ni boss wa clouds lakini hiyo ni family business ya kina Kusaga sio mali binafsi ya Joe. Huko Wasafi ndiko kwenye maslahi yake binafsi yeye kama Joe bila kidomodomo cha ndugu zake.
 
Sasa ndugu huyo mwanamke ndiye mke halali wa Kusaga. Yeye mwanamke mambo ya umiliki wa media kayajulia wapi mpaka akaweke fedha humo? Ni wazi Joe kawekeza kupitia mkewe kwa sababu hataki purukushani na ndugu zake.
 
Millard ni muajiriwa wa Clouds na hiyo ndiyo imemsaidia kuitangaza hizo account zake za mitandao. Hategemewi kwenda kinyume na maslahi ya kazi yake.
 
mkuu umeenda mbali japo upo sahihi, kilicholeta ubishani kua mwenye share kubwa ndo mmiliki je sheria inasema hvo?
Mwenye share ndogo na kubwa wote ni wamiliki....hata kama mtu ana hisa 1, naye ni mmiliki. Maana gawio likija, linagawiwa kwa wote.

Mwenye hisa nyingi, kwa maana ya majority shareholder...ni mwenye stake inayoanzia 51% ya hisa zote.

Kuwa majority shareholder maana yake yeye ndiye anaamua maamuzi ya kampuni ambayo wakurugenzi watayatekeleza...yaani yeye ndiye mwenye say kuwa kampuni ielekee uelekeo gani kibiashara wakikaa kwenye members meeting.

Ila maamuzi ya majority shareholder yakitishia usalama wa stake ya minority shareholders, minority shareholders wanaweza kwenda mahakamani kufile case ili kulinda maslahi yao.

Lakini si kweli kuwa mwenye share kubwa, kwa maana ya majority shareholder ndiye mmiliki wa kampuni...wanahisa wote kwa pamoja, majority na minority, members wa kampuni wote kwa pamoja ndiyo wamiliki wa kampuni.
 
mtu anayeleta ubishi wa kipuuzi kama huyo jamaa muulize swali moja tuu, Nani mmiliki wa Kampuni ya Apple?

Watu wote tunajua Steve jobs alikuwa ndiye founder wa kampuni ya apple pamoja na rafiki yake yule steve wozniac.

aende akagoogle owners wa apple then atapata jibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mjadala umeufunga
 
Hv ngoma za mond zinaendelea kupgwa pale mawingu fm

Its not over until its over...[emoji769]
 
Mkuu jamaa anachokueleza ni kweli kabisa... nitakupa mfano toka kwa wenzetu Marekani.
Nadhani unajua kuwa kampuni ya Apple ilianzishwa na Steve Jobs, Woziniak na Ronald Wayne. Lakini kati yao hakuna ambaye ndiye mmiliki wa apple ni kwasababu waliuza share zao ikapelekea hakuna hata mmoja aliyebaki kuwa major shareholder hadi Jobs alifukuzwa kuwa CEO wa kampuni ikabidi aondoke akaanzishe kampuni nyingine mpaka alivyorudhishwa baada ya miaka zaidi ya 10 kuja kuokoa jahazi.
Lakini still hakuwahi kuwa refered kama mmiliki wa apple tena ila tu inakumbukwa kama ni founder.
Major shareholder ndiye uwa ana maamuzi makubwa ya kampuni, ila inawezekana kama umepewa kuwa Mkurugenzi wa board ukaachwa ufanye maamuzi.
Pia inawezekana ukawa labda na 45%, halafu mwingine ana 20% mwingine 35% hawa wanaweza wote kuungana kupiga kura labda ya kukutoa kuwa kiongozi wa board. Maana wakijumlisha watakuwa na shares kubwa kuliko wewe. Ndiyo maana watu wengi utakuta uwa wanauza share ila anabaki na 51% ili hata wale wengine wakiungana bado hawataweza kumtoa maana watakua na just 49%.
 
mkuu usiwe mbishi tulia hujui chochote kwenye michezo
1.Yanga bado hawajaingia kwenye mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa timu,hakuna mkutano mkuu wa yanga uliowahi kaa ukapitisha mabadiliko ya uendeshaji wa timu yao...yanga haijaingia kwenye mfumo mpya wa nabadiliko ya uendeshaji wa timu

2.Simba imeshaingia kwenye mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji wa timu...mkutano mkuu ulishapitisha maazimio ya mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji wa timu...kilichopo sasa kinachofanyika ni kumalizia procedures za kisheria ili timu iendeshwe katika mfumo wa hisa/shares za wanachama na mwekezaji..Tanzania kwa upande wa timu zinazomilikiwa na wanachama ni simba pekee yake ambayo imebadili mfumo wa uendeshaji wa timu na kuwa kampuni

3.Inaonesha wewe siyo mtu wa soka na hujui chochote kuhusu soka...serikali ilishatoa muongozo kupitia kwa waziri wa michezo na Katibu BMT kuhusu timu za wanachama zinazotaka kufanya mabadiliko ya kiuendeshaji na kujiendesha kama kampuni...katika muongozo huo upande wa wanachama inatakiwa wawe na hisa 51% na mwekezaji hisa zisizidi 49%..hi ni kuepusha timu anbazo ni mali ya wanachama mfano coastal,simba,yanga etc zisijekuwa mali ya mtu mmoja...so leo hata billgert na utajiri wake akija kutaka kuwekeza timu kama simba haruhusiwi kununua hisa zaidi ya 49%(nimetolea mfano simba sababu ndo timu pekee tanzania liyoingia kwenye mfumo mpya wa uendeshaji timu kama kampuni)

4.Siku nyingine usirudie ku argue vitu ambavyo huvijui mkuu..argue kwenye vile vitu ambavyo unavijua na unauhakika navyo tu..am done
 
Boss roho safi !
Staff mchawi

TAFUTA MTU YOYOTE UMLAUMU...!
 
kumbe n kweli mi cjui
 
Habari zenu wandugu.
Naomba na mimi nizungumzie kidogo kuhusu umiliki wa hisa kwenye kampuni.
Kuna tofauti kati ya kuwa na majority shares na kuwa na control.
Nadhani hapa ndio mnapotofautiana.
SHAREHOLDER anaweza kuwa na Control over the company kwa kuwa na more than 50% ownership.hii ndio watu wengi wanajua.
Lakini sio lazima mwenye shares nyingi ndio awe na control kwenye kampuni.
Control inawezekana ikaamuliwa kwa agreement baina ya SHAREHOLDERS wenyewe.na hii ndio Founder wengi wanaitumia au serikali nyingi wanaitumia wanapowakaribisha wawekezaji.
Mfano Leo hii serikali inaweza ikauza shares za tanesco na mwekezaji akawa na more than 50% lakini serikali ikasema may be serikali ndio itakuwa mpanga bei ya umeme although serikali ni minority shareholder.
Au serikali ikaamua kati ya ma-directors 10 serikali iwe na power ya kuchagua ma-director 6 and so on.
Hivi nyie mnadhani NMB na NBC serikali ilivyouza ndio mwekezaji ana control kwa kila kitu. Lazima serikali na mwekezaji walikaa chini na kukubaliana serikali itakuwa na sauti kwenye mambo yapi na mwekezaji atakuwa na sauti kwenye mambo yapi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante kwa darasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…