Habari zenu wandugu.
Naomba na mimi nizungumzie kidogo kuhusu umiliki wa hisa kwenye kampuni.
Kuna tofauti kati ya kuwa na majority shares na kuwa na control.
Nadhani hapa ndio mnapotofautiana.
SHAREHOLDER anaweza kuwa na Control over the company kwa kuwa na more than 50% ownership.hii ndio watu wengi wanajua.
Lakini sio lazima mwenye shares nyingi ndio awe na control kwenye kampuni.
Control inawezekana ikaamuliwa kwa agreement baina ya SHAREHOLDERS wenyewe.na hii ndio Founder wengi wanaitumia au serikali nyingi wanaitumia wanapowakaribisha wawekezaji.
Mfano Leo hii serikali inaweza ikauza shares za tanesco na mwekezaji akawa na more than 50% lakini serikali ikasema may be serikali ndio itakuwa mpanga bei ya umeme although serikali ni minority shareholder.
Au serikali ikaamua kati ya ma-directors 10 serikali iwe na power ya kuchagua ma-director 6 and so on.
Hivi nyie mnadhani NMB na NBC serikali ilivyouza ndio mwekezaji ana control kwa kila kitu. Lazima serikali na mwekezaji walikaa chini na kukubaliana serikali itakuwa na sauti kwenye mambo yapi na mwekezaji atakuwa na sauti kwenye mambo yapi.
Sent using
Jamii Forums mobile app