Clouds na Wasafi nazifananisha na Freemasons
Freemasons they are secrett society ambao kuanzia vikao,ibada zao,sherehe zao zinafanyika kwa siri sana bila watu wa nnje kufahamu,watu huiongelea Freemason kwa maneno ya kusikia tu na kuhisi hisi ila hamna anaejua ukweli au kuthibitisha anachokiongea.
Clouds na Wasafi ni kampuni mbili tofauti zenye mmiliki mmoja mwenye team mbili tofauti,ili kuweza kuunganisha team zake ni lazima huyu mmiliki aishi kama walivyo freemasons.
Tutasema kila tuwezacho ila ukweli wanaujua wenyewe hizo media mbili wanakutana saa ngapi,wanafurahia mafanikio yao muda gani,naamini kabisa hizi kampuni mbili "kuna siri kubwa ndani yake watu wa nnje hatuwezi ijua" so tunavyo zi discuss ni sawa na kupiga tu story ambazo hazina mwisho.
Nionavyo mimi
Clouds ni mzazi na Wasafi ni mtoto
Kuna kasumba ya kwamba mzazi hakosei (sio kweli) Mzazi kuna wakati anakosea na wazazi wapo baba na mama mara nyingi ukifanya kosa mama akikusemea kwa baba Utazibuliwa hiyo haijalishi baba kaona kosa ulilofanya ila anakuadhibu kwa sababu anaamini "mama" hawezi kukusingizia.
Baba anapokuadhibu japo hajaona kosa ulilofanya hawezi kaa upande wako maana itakua ni kama kakubali ungana na ujinga wako,kivyovyote vile baba ataungana na mama na wote watakua na hasira juu yako.
Miaka inaenda mtoto aliyeadhibiwa na baba umri unakua akili inapanuka,akiwa mkubwa anakumbuka kuna siku baba alinipiga kwasababu mama alimwambia kuwa alikosea,mtoto anaamua kumfata baba kwa ujasiri kumuuliza swali
Eti baba nilipokua mdogo kuna siku ulienda kazini uliporudi mama akakwambia mimi nilifanya kosa,wewe ulinipiga sana ile siku hadi ukaniachi hii alama,Hivi baba kwann ulinipiga vile? ulikua na uhakika gani kua ni kweli nilifanya kosa? unajua mama alinisingizia siku ile akaniambia ukirudi lazima akwambie ili unichape?
Mtoto atamtwanga baba maswali kisha atamrudisha baba nyuma atamuelezea sababu za kwann mama aliamua kumsingizia ili achapwe...
Baba huyu baada ya kuelewa sababu na kugundua kweli mwanae alisingiziwa sasa inampasa kwanza "kukiri kosa" na pili inampasa tena "kumuomba msamaha" mtoto wake, "Huyo ndie mzazi bora".
ila ukiona mzazi anapoulizwa maswali na mtoto magumu magumu halafu mzazi anatumia Mabavu,ubabe,cheo cha "mzazi" kutomjibu mtoto anaamua tu kumfokea na kuyapangua maswali,unagundua fika huyu mzazi kuna NATI kichwani haijakaza ana upungufu wa kinga ya HEKIMA akilini mwake.
Sioni tatizo wala shida kama JOE atakiri kosa na kuomba msamaha, kwenye case hii namuweka JOE kama BABA na marehemu kama MAMA, ila anapoendelea kushupaza shingo kutafanya mtoto aone BABA nae ni wale wale tu.