Kusaga : Tulipopiga wimbo wa Mbosso tuliambiwa tujieleze kwanini tulikuwa hatupigi nyimbo za wasanii wa Wasafi. Uongozi wa WCB uulizwe

I support Diamond lakini seems his management ni waswahili sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio waswahili wanaijua biashara ya muziki. Katika maamuzi ya maana kabisa waliyofanya kibiashara ni kutaka majibu ndio miziki yao iendelee kuchezwa clouds.
Clouds waliazimia kuwauwa ila wakagundua wao ndio wanapoteza. Sasa wakataka warudi waendelee kuwatumia Wasafi... Mwenye akili lazima ustuke, nimekuwaje mzuri bila maelezo?!
 
Kuna ubaya gani taasisi kama clouds kueleza why walifikia maamuzi ya kutocheza nyimbo zao? Wasafi hawakuwa na haki ya kujua walikosea wapi mpaka wakapata adhabu?
Mtu aliyeazimia kukumaliza, halafu akaona ndio kwanza unazidi kuimalika. Ghafla akarudisha upendo bila maelezo. Kuna ubaya kutaka kujua dhamira yake?

Hao jamaa waligundua wanapoteza, walirudi sio kwa ajili ya kuwanufaisha wasafi ila kuwatumia kibiashara.
Kina Sallam wakastuka, biashara imeamia kwetu jamaa wanataka kuichukua tena technically. So naona mameneja wapo sahihi kabisa, afterall hatuoni kinachopungua wasafi zaidi wanazidi kushain.
 
Ambaye hatakuelewa na hapa basi atakua na matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biznez strategy mzee,adui akijirudi kaa chini tafakari kwa nini kajirudi? je ana nia ya dhati kujirudi au ana plan B ya kukumaliza kwa njia ya kujifanya rafiki? "yani ni kama vile ccm kutaka kuwachagulia chadema mwenyekiti"...nadhani utakua umenielewa
 
EATV waliacha kupiga myimbo za Mond mapema kabisa baada ya kukataa kushiriki tuzo zao za kichonganishi,EFM ishu za kimapenzi za boss wanazileta keenye kazi....hakuna mwenye sababu za msingi saaana za kuwatenga wcb,hata shigongo nae ilikua hivyo hivyo.
 
Ni kweli uongozi wa WCB umekataza nyimbo zao zisipigwe Clouds FM? Mbona Diamond amekuwa akilalamika kuwa nyimbo zake azipigwi baadhi ya radi huku wao ndio wamekataza?
Uongozi wa WCB umemficha Diamond ukweli?
Kama ulisikiliza interview ya Ommy (Times FM) na Diamond miaka miwili iliyopita, na kama ungeangalia cku ya uzinduzi wa Wasafi TV bila shaka ungekuwa umeshapata jibu! Kama umesahau, wacha nikukumbushe.

Siku ya Interview kati ya Diamond na Ommy, Diamond aliweka wazi kuhusu mtafaruku uliokuwa umetokea na chanzo kikiwa Clouds kutaka kumtumia Harmonize bila kutoa chochote; hata nguo za kupandia stejini! Sasa kwavile (according to Diamond) Clouds hawakuwa tayari kutoa chochote; Diamond nae akagoma Clouds kumtumia Harmonize kwenye Fiesta!! Aidha, according to Diamond huyo huyo, baada ya Diamond kugoma kumtoa Harmonize, Clouds nao waka-retaliate kwa kuanza kutopiga ngoma za Wasafi!

Na kabla ya hapo, wiki chache nyuma(or possibly mbele; sina kumbukumbu), kama unavyomjua Sallam, aliwahi kambwatukia Ruge vibaya sana kule Instagram na akasema wazi kwamba Ruge nitakuumbua!



Hata hivyo, saa chache baadae, Sallam akasema kwa heshima ya Kusaga, na kwavile kamuomba, ana-let it go!



Sasa siku unafanyika uzinduzi wa Wasafi TV, Babu Tale ndo akamwaga mboga kabisa! Akiwa Live (Angalia hapo Dakika 2:15) anasema:

Sasa hapo ukiangalia Tale hakuitaja Clouds, ila alichosema, wale ambao waliacha kupiga nyimbo zetu basi wasipige!

Hivi sasa Kusaga anasema aliwaambia Clouds wapige nyimbo za Wasafi lakini uongozi wa Wasafi ukamtaka ajieleze kwanini walikuwa hawapigi huko nyuma! Sasa kama Tale hakuitaja Clouds, na Kusaga nae akaja kugundua kwamba nyimbo za Wasafi hazipigwi, huo ni ushahidi tosha kwamba Clouds walikuwa hawapigi sio kwa sababu uongozi wa Wasafi walikataza, bali walikuwa hawapigi hata kabla uongozi wa Wasafi hawajatoa tamko la "...wale ambao waliamua media zao zisipige nyimbo zetu" waendelee kutopiga! Hapa Clouds walijua kwamba hiyo kauli na wao ilikuwa inawahusu kwa sababu walikuwa hawapigi hata kabla ya tamko!

Kwa maana nyingine, Diamond HAKUDANGANYA aliposema kuna media hazipigi nyimbo zao! Na hapa tusisahau siku Lady Jaye Dee alipotoa tuhuma mzito dhidi ya Kusaga na Ruge; Ruge alifanya haraka kutoka mbele kukanusha tuhuma za Jide! Hata tuhuma za Sugu dhidi yake kuhusu Malaria No More pamoja na suala la Studio ya Wasanii, Ruge alikanusha! Lakini shutuma mzito kutoka kwa Diamond hakuwahi kukanusha hadi ameingia kaburini!
 
We jamaa umemaliza kila kitu uzi ulitakiwa uishie hapa.
 
Mbona hawajampa airtime Qboy msafi, Harmonize au Rich Mavoko ...


Msiyoyajua ni sawa na usiku wa giza...


Au mbona hawawafanyii interview watangazaji wa clouds. Najua utakuwa umeona tatizo lilipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
umenena wapo vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona hawajampa airtime Qboy msafi, Harmonize au Rich Mavoko ...


Msiyoyajua ni sawa na usiku wa giza...


Au mbona hawawafanyii interview watangazaji wa clouds. Najua utakuwa umeona tatizo lilipo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kati ya watu weupe wa humu jamvini basi wewe utakuwa mmojawapo anajifanyaga mjuaji kumbe hamna kitu.hoja za humu zimekuzidi uwezo wako wa akili.
 
Kwa uzi wako huu tayari umeshaonesha upo upande gani.Una uhakika gani kama kweli uongozi wa CMG ulizuiwa kupiga nyimbo za wasanii wa Wasafi,vipi akaja mtu mwingine naye akawa upande mwingine na kudai tofauti na maelezo yako. Vitu kama hivi ni bora tuwe na ushahidi wa kutosha kama hiyo barua ili tujiridhishe kwa pande zote.
 
Diamond ana hisa 45% halafu unasema Diamond katoa jina, Kusaga ndo katoa mzigo?! Acheni masihara nyie watu! Halafu kiroja kingine ni hapo unaposema Kusaga ndie kaamua Wasafi miziki yao isipigwe kwenye baadhi ya radio wakati Kusaga mwenyewe wakati anahojiwa kasema wazi hana mamlaka yoyote juu ya WCB Label. Sasa how come tena awe na ubavu wa kuwapangia nyimbo zao zipige wapi na wapi zisipigwe?! Na kama aliamua zisipigwe, mbona baada ya uongozi wa WCB kugoma nyimbo zao mbona hajashinikiza ikiwa anao huo ubavu?!

The problem nyie watu bado hamtaki kukubali kwamba Diamond amepiga hatua kubwa sana, na matokeo yake ndo hayo! Kila kubwa linalofanyika, mnaamimi sio lake kwa saababu you don't believe ni SELF MADE hususani kutoka kwa mtu kama Diamond ambae hata shule yake yenyewe ndo hivyo tena!!!

Mwaka 2016, Diamond aliwahi kuhojiwa na kusema amekataa kusainiwa na Roc Nation ya Jay Z! Pitia huo uzi uone watu walivyokuwa wanamkejeli na kumwita muongo mtafuta kiki kwa maana hakuwa na ubavu wa kuwatolea nje ya Roc Nation! Na hao waliona Diamond alikuwa anatafuta kiki kwa sababu walikuwa hawataki kukubali kwamba jamaa alishapiga hatua kubwa!

Wote hao wakaja kuzibwa midomo baada ya hatimae Diamond kusainiwa na Universal! Na hata ukiangalia sababu alizotoa Diamond kwanini alikataa kusainiwa na Roc Nation, utaona alikuwa sahihi manake mkataba na Universal ulikuwa tofauti!!
 
Umemwambia jamaa ukweli
 
Tatizo la kua na Mameneja uchwara Waswahili na Walozi,.

Wiki Ijayo utamuona Salam kwenye icho kipindi akimwambafai,. Kama ilivyokua kwenye kauli ya penseli Mzee wa kwenda na bit

Tena mm namuona kama Sallam ndio ttzo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…