Kusahau kufunga Mlango wa Gari kunaweza kuua/ kuathiri uzima wa Battery ya Gari

Uliposema gari nikakumbuka land rover 109 yangu
Nikaona hainihusu

Ila nadhani hyo si sababu
 
Hapo hakuna kilichokufa ila unapoacha mlango wazi battery hutumika kwakuwa system inakuwa standby, ishu ya power window pia sio tatizo kabisa hapo gari kutokana na kuisha chaji battery inahitaji reset hivyo nenda kwenye kila kioo shusha hadi mwisho then pandisha hadi juu shusha tena kitakuwa kimejiset na Fanya hivyo kwa vioo vyote,
 
Boss sio rahisi kwa masaa nane tu kuua betri yako,kuna uwezekano betri yenyewe ilishaanza kuchoka,Pia kama ni gari ndogo ambayo unatumia N45 ili uepukane na hizo changamoto ndogo ndogo pachika N50.
 
Mkuu mimi nakupongeza kwa kumiliki gari, japo sina lilote la kukushauri
 
Aiseeeee mambo ya kusahau ni hatari ,leo sijui ingekuwaje ,gari ilikuwa imepaki kwenye jua muda mrefu wakati wa kuiwasha nikashusha vioo vyote kuondoa joto kwanza ,katika kupandisha nikasahau kupandisha kioo kimoja cha nyuma ,nikatembea umbali mrefu kidogo kagiza giza mpaka kakaingia.

Nikafika sehemu nikaipaki ili nichukue mazagazaga ya kwenda home nayo ,nikaacha simu mbili kwenye kiti cha abiria mbele Smart na Kitochi na pia nikaacha Laptonga ila niliiweka chini ya kiti...Nikapotea kutafuta Mazagazaga kama 15mins hivi,ile narudi kuangalia daaaaah dirisha la nyuma lipo wazi,kitu cha kwanza ni kufungua mlango na kuangalia chini kama laptop ipo ,aiseee sikuamini niliikuta ,nikaangalia mara tatu kama ni kweli au macho yangu yanaona vibaya,baada ya hapo ndio nikaangalia simu nazo zilikuwepo.

Nafikiri giza watu walihisi ni TINT ndio maana hawajajua kama kioo kilikuwa hakijafungwa....USAWA huu wa Mi5 tena ningetoa wapi hela ya kununua Laptop na Smart Phone? Simu na laptop nilinunua kipindi cha kikwete!!
 
Tuambie ni gari aina gani kwanza,isije ikawa una kifaa cha kukusogeza kutoka sehemu moja kwenda nyingine unasema ni gari, kumbe umechanganya...
Wewe jamaa ndio maana wengine tumebaki wa kusoma tu comments...
 
Hakuna uhusiano na alichooandika Mleta Mada. Mleta mada hajazungumzia kusahau. Umeleta tu stories zisizo na msingi na za utoto. Yeye anazungumzia battery yake je imekufa sababu ya taa kuwaka. Wewe leo hii unaona gari ,laptop ni issue ya kututangazia? Very stupid. Nyie kwa nini hampendi kupata elimu mkaelimilika?
 

Hapo chances ni battery! Alternator za kuanzia Miaka ya tisini zinatumika zile za diode ambazo kitaalamu zinavumilia sana na zipo very accurate kuliko zile za cutout nje .

Battery ikianza kuchoka huwa inabehave Kama hiyo yako.
 
Battery imechoka hiyo ila sio kwamba imekufa cha msingi itoe nenda kaichaji masaa 4 rudisha itakua poa.
 
Mkuu indicator ya mlango wazi inatumia nguvu ndogo sana, haiwezi kumaliza battery ndani ya masaa 8.
Uwezekano pekee ni kama kuna taa (bulb) nyingine inawaka sabamba na hiyo.
Kama ukifungua buti kuna taa inawaka ndani ya buti, hiyo inaweza kumaliza battery hasa kama hilo battery linakaribia ukomo wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…