Aiseeeee mambo ya kusahau ni hatari ,leo sijui ingekuwaje ,gari ilikuwa imepaki kwenye jua muda mrefu wakati wa kuiwasha nikashusha vioo vyote kuondoa joto kwanza ,katika kupandisha nikasahau kupandisha kioo kimoja cha nyuma ,nikatembea umbali mrefu kidogo kagiza giza mpaka kakaingia.
Nikafika sehemu nikaipaki ili nichukue mazagazaga ya kwenda home nayo ,nikaacha simu mbili kwenye kiti cha abiria mbele Smart na Kitochi na pia nikaacha Laptonga ila niliiweka chini ya kiti...Nikapotea kutafuta Mazagazaga kama 15mins hivi,ile narudi kuangalia daaaaah dirisha la nyuma lipo wazi,kitu cha kwanza ni kufungua mlango na kuangalia chini kama laptop ipo ,aiseee sikuamini niliikuta ,nikaangalia mara tatu kama ni kweli au macho yangu yanaona vibaya,baada ya hapo ndio nikaangalia simu nazo zilikuwepo.
Nafikiri giza watu walihisi ni TINT ndio maana hawajajua kama kioo kilikuwa hakijafungwa....USAWA huu wa Mi5 tena ningetoa wapi hela ya kununua Laptop na Smart Phone? Simu na laptop nilinunua kipindi cha kikwete!!