Kusaidia Ndugu/familia ni wajibu au lazima?

Kusaidia Ndugu/familia ni wajibu au lazima?

Hivi kweli kuna haja ya kuuliza kama kusaidia ndugu ni wajibu ?! Ni wajibu na lazima, huwezi acha kuwasaidia ndugu zako na unawajibika kufanya hivyo. Kwani wao hawana wajibu wa kukusaidia wewe?
ww uliyesoma kwa kuchangiwa ada ya masomo una haki hyo

mm nimesoma kwa hela za baba na mama yangu na cjawahi changiwa hata mia ya ndugu ...nitasaidia hao wazazi ila c ndugu yyte ...

maana najua kuwa hata leo hii MUNGU akinichukua hakuna wa kunisaidia familia ni mke wangu atapambana na familia
 
Kwa familia zetu mkuu ni kama lazima, huwezi acha watoto wa ndgu zako wanateketea na hao wazazi wake hawaeleweki ukawaacha eti watakuharibia future yako ukitoa msaada.

Wengi wetu tumelelewa na mikono mingi labda wale wa baba na mama tu, lakini nao wana kaka na dada zao. Aisee familia zetu zina chain ndefu. Tusaidiane tu jama usiache ndgu wakiteketea kama uwezo unao.
 
Kwenye misingi mingi ya familia za ki Afrika sote tumefika hapa tulipo kwa misaada ya wanafamilia kwa namna moja au nyingine kulingana na muundo na hali ya mshikamano wa familia yenu.......

Kila mmoja wetu anajua hali ya familia zao na mshikamano uliopo baina yenu kama wana ukoo au familia......hali hiyo automatically ndio itaamua kuwa uwe msaada kwenye familia kama kulipa fadhila au kuipa kisogo familia..........

NB;
Wanafamilia wengi wa jamii za kiafrika hawajui maana ya msaada.......
 
ww uliyesoma kwa kuchangiwa ada ya masomo una haki hyo

mm nimesoma kwa hela za baba na mama yangu na cjawahi changiwa hata mia ya ndugu ...nitasaidia hao wazazi ila c ndugu yyte ...

maana najua kuwa hata leo hii MUNGU akinichukua hakuna wa kunisaidia familia ni mke wangu atapambana na familia
Unajuaje kama misaada ya ndugu ilipitia kwa wazazi wako....??
 
Kweli ni mambo ambayo waswahili mmejitengenezea huo mfumo na mmeukubali

Na ukitaka kushangaa zaidi unaenda kuchangia harusi au zawadi za birthday hata kama ni mfanyakazi tu mwenzio
Wa kuangalia ni Wazazi au labda kuna watoto wameachwa yatima na hawana uwezo

Ukiweza saidia tu kwa hiari ila hakuna ulazima nyie ndio mmeufanya ulazima
 
Jamani jamani wapendwa

Kuna watu humu tumepata mafanikio kutokana na kulelewa na watu ambao sio wazazi wa kutuzaa. Kuna baadhi wazazi wenu walilelewa na wajomba/bamkubwa and all the like.

Upendo ni kitu kidogo sana. Sikulazimishi kupenda lakini upendo unalipa. Kuna mahali unapata msaada usifkiri ni wewe hapana ni sadaka ya mzazi wako alimlea mtu au kumsaidia mtu.

Binafsi yangu wengi walionisaidia kufika hapa sio ndugu wa ukoo ni watu baki kabisa..sikuwafahamu..

Mnahisi connection zinatoka wapi???ishi na watu vizuri na Mungu atakuinulia watu wa kukushika mkono somewhere. Hakuna asiyehitaji msaada nenda hata kwenye biblia akina Yusufu pale ambapo walitajwa kwa Farao yote kwa kumtafsiria mtu ndoto...

#tupendanewapendwalifeistooshorttohate#
 
Kama umesaidiwa nawe saidia... huo ni utu

Kama hujasaidiwa na una uwezo wa kusaidia, saidia.. huo ni ubinadamu

Kama umesaidiwa na huna uwezo wa kusaidia, usisaidie... huo ni umaskini

Msaada ni hiari, kwa wengine ni sadaka na kwa wengine ni kutafuta kiki

Uamuzi ni wako, hakuna anayekulazimisha.... kutotoa msaada sio kosa kisheria

Relax, vuta pumzi. Maisha ni hayahaya.... Ishi utakavyo
Kwa andiko hili naamini wewe ni mcha Mungu na bila shaka ni mtu mwenye mafanikio. What a great thinker! Thanks.
 
Kusaidiana kupo lakini isiwe wao wanaweka vijambio chini wakisubiria misaada toka kwa wengine.
Maisha ni kupambana sio kukaa kikhanithi mwisho wa siku unaanza kulaumu ndugu yako kuwa hakusaidii.
 
Kuna wale wanaoomba mitaji, hawajiulizi wewe ulipewa na nani huo mtaji?

Mtu mwenye nguvu na afya lazima afanye kazi na sio kusubiri kupewa. Tena waomba mitaji wengi huwa wanawaza milion kwenda juu [emoji3][emoji3], kifupi mtu anakuwa anatafuta shortcut ya mafanikio.

Mimi nitasaidia mgonjwa, mtoto yatima aliyepo shule na mzee asiyejiweza, ila hawa wengine tutashikana ubaya. Mimi nifanye kazi nimpe yeye hela akale na mke wake, hapana aisee.
 
1 Timotheo 5:8

"Lakini kama mtu hawatunzi watu wa jamaa yake, hasa wale wa nyumbani kwake, basi, mtu huyo ameikana imani, na ni mbaya zaidi kuliko mtu asiyeamini"

Mkuu hudumia kwanza familia yako, hakikisha wanapata mahitaji yao kwa usahihi, kisha saidia sasa na wengine kama uwezekano huo upo. Usije hudumia wengine huku familia yako inapitia magumu, walimwengu si wema kivile, watakuwa wa kwanza kukunanga kuwa ulijifanya una huruma sana.
Nimeona sehem nyingi, familia nyingi na hata mmoja wa polisi aliyefariki kwa tukio la Juzi inaonesha kua alikua tegemeo la familia nzima mpaka mtoto wa kaka yake.

Hoja yangu ni moja.
Hii ni tamaduni au ni vipi!?

Unamaliza shule, unapata kazi baada ya hapo unatakiwa kusaidia familia nzima na ndugu wa pembeni(kitanzania)

Mtazamo wangu:
hii ni moja ya kurudishana nyuma kimaendeleo

Nilidhani ni vema iwe kutazama future ya yako kwanza na kuhudumia/kusaidia wengine isiwe ni wajibu/lazima bali iwe HIYARI kulingana na uwezo wa mtu.
 
🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾🙌🏾👍🏽Siyo lazima ni hiari.
Nadhani ilifike hatua tujue kusaidiana inategemea na mfuko wa yule unayetaka akusaidie hivyo sio lazima sababu ilivyo sasa mtu akishajua una ka ajira basi ye moja kwa moja anajua uwezo wa kumpatia akitakacho kwa muda autakao inawezekana huku akiwa hajui hata kipato / mipango iko vipi kutokana na hicho ukipatacho.

Na hii ndo mwisho inaletaga kutokuelewana kisa tu mtu amehitaji msaada kisha ukamwambia sina kwa wakati huo.
 
Inatagemeana na jamii tajwa ilihusika vip katika mafanikio yako ,kuna wengine walisomeshwa au kuwezeshwa na hao ndugu kunzia kula kusoma nk. Kama binadamu anayethamini msaada kutoka kwa mtu ambaye si mzazi wake naye kutoa msaada sio dhambi.
 
hii kitu ngumu sana ndugu zangu...tunapaswa kuwasaidia hakika...ila ukicheza hao ndio watakuangusha.....nlishawasomesha shemeji zangu duh...mie sikufika univ....hakika nliwalipia kwa kuunga unga.....walichokuja kuniambia....ila nimewasamehe kabisa...eti " kama baba etu angekuwepo angeweza kutosomesha...tukipata kazi tutakurudishia" na wamepigika na digrii zao...wacha...mmoja fundi simu posta,,,,mwingine keshatunguliwa 2 na baba tofauti......mie nadunda tuuu....adabu imewakaa....
 
Ubinafsi si mzuri kama una nafasi au kipato saidia tu wenye uhitaji kwa kufanya hivyo unajenga koo au familia yenye nguvu kiuchumi na maamuzi ktk jamii
 
Mimi nasema kusaidia baadhi ya watu ni nuksi hasahasa upande wa ubabani buziiiiii sana.


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Back
Top Bottom