Kusema kuna watu wanamshauri vibaya Rais au wanampotosha Rais ni kumtukana Rais

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Hii kauli imezoeleka sana na watanzania. Ukweli hii ni kumtukana Rais. Maana yake unasema kuwa Rais hawezi kung'amua ushauri mbaya na mzuri.

Kwamba wewe umeweza kuona ushauri mbaya aliopokea lakini Rais ana uwezo mdogo wa kutambua mambo hivyo amashindwa kujua zuri na baya!?

Wengi wanafikiri kwa kusema hivyo wanamtetea Rais lakini ukweli ni kuwa wanamtukanisha. Pengine labda waseme kuna watu wenye nguvu wanaomshinikiza Rais kufuata ushauri fulani mbovu, lakini kusema Rais anashauriwa vibaya inamjengea Rais picha mbaya.
 
Mkuu, alipoteua, akatengua kabla hajaapisha, kwa mara ya kwanza, tukasema kuteleza kupo, ingawa si jambo hilo kwakuwa anazo tools zote za kuhakikisha kuwa makosa hayatokei, muda upo kwakuwa haikuwa dharula.

Kwa mara ya pili, ya tatu....hapo unasemaje?
 
Hii kauli imezoeleka sana na watanzania. Ukweli hii ni kumtukana Rais. Maana yake unasema kuwa Rais hawezi kung'amua ushauri mbaya na mzuri.

Kwamba wewe umeweza kuona ushauri mbaya aliopokea lakini Rais ana uwezo mdogo wa kutambua mambo hivyo amashindwa kujua zuri na baya!?

Wengi wanafikiri kwa kusema hivyo wanamtetea Rais lakini ukweli ni kuwa wanamtukanisha. Pengine labda waseme kuna watu wenye nguvu wanaomshinikiza Rais kufuata ushauri fulani mbovu, lakini kusema Rais anashauriwa vibaya inamjengea Rais picha mbaya.
Kitwanga alikuwa ameshakunywa Konyagi wakati anaongea maneno haya. Huyu naye ni wa kumchukulia seriuos kweli?
 
Kuna mtu mwenye nguvu kuliko raisi nchi hii?
Si nchi hii tu, na si zama hizi tu. Watawala wengi, hata machief wa kijadi walikuwa na kundi la watu nyuma yao wenye nguvu. Watu walioweza kumfanya kiongozi afanye mambo fulani hata kama hakunaliani nayo.
 
Kitwanga alikuwa ameshakunywa Konyagi wakati anaongea maneno haya. Huyu naye ni wa kumchukulia seriuos kweli?
Kitwanga si wa kumchukulia serious, sema ni wengi wamekuwa wakisema kauli kama hizi na kwa miaka mingi.
 
Middle class acheni uzuzu wa kiuoga, kwani president hakosei?,au ndiyo yale yale ya kumwona Rais kama nusu Mungu!,ninakubaliana na mchango niliousoma humu kuwa wana sumbawanga wana mchanganyiko na wazambia (hawa ukiwatibua wanabadilisha tu )
 
Si nchi hii tu, na si zama hizi tu. Watawala wengi, hata machief wa kijadi walikuwa na kundi la watu nyuma yao wenye nguvu. Watu walioweza kumfanya kiongozi afanye mambo fulani hata kama hakunaliani nayo.
Kuendelea kujibizana na wewe humu ni kazi bure tu.

Nchi hii high rank ya uongozi ni Urais sio wafalme au marais wastaafu. Kama wapo huyo ambae tunajua katiba yetu inasema yeye ndio top leader nchi hii na anawasikiliza sana hao ambao hawapo kikatiba badala ya kusikiliza vyombo vivyo chini yake na anavyovisimamia basi hatuna budi kusema hajui baya/wala zuri. Nao hao anao waona wazuri kwakwe ndio wanampotosha.

NB. Masuala ya nchi hayaongozwi kwa historia kama ngonjera zako za machief wa kijadi n.k. nchi inaongozwa kwa taratibu na kanuni ambazo kwa pamoja zinaitwa sheria.
 
Ah,Kitwanga ndiyo yule mheshimiwa aliyekuwa amelewa bungeni?
Ndio ni yeye, ila safari hii maneno haya ameyasema akiwa hajalewa!.
So tambua hata walevi huwa wana akili timamu na wanaongea facts.
Mama ajitafakari genge linalomzunguka.
 
Kitwanga kasema ukweli mtupu ila shida Watanzania hatupendi kujadili hoja bali mtoa hoja.
 
Kitwanga alikuwa ameshakunywa Konyagi wakati anaongea maneno haya. Huyu naye ni wa kumchukulia seriuos kweli?

Na huyu je?

FpJ7vnuWcAAbZ_x.jpeg
 
Hii kauli imezoeleka sana na watanzania. Ukweli hii ni kumtukana Rais. Maana yake unasema kuwa Rais hawezi kung'amua ushauri mbaya na mzuri.

Kwamba wewe umeweza kuona ushauri mbaya aliopokea lakini Rais ana uwezo mdogo wa kutambua mambo hivyo amashindwa kujua zuri na baya!?

Wengi wanafikiri kwa kusema hivyo wanamtetea Rais lakini ukweli ni kuwa wanamtukanisha. Pengine labda waseme kuna watu wenye nguvu wanaomshinikiza Rais kufuata ushauri fulani mbovu, lakini kusema Rais anashauriwa vibaya inamjengea Rais picha mbaya.

"Mtu mwenye akili akikuambia kufanya jambo la kipumbavu na wewe ukakubali atakudharau." -- JKN.
 
Hii kauli imezoeleka sana na watanzania. Ukweli hii ni kumtukana Rais. Maana yake unasema kuwa Rais hawezi kung'amua ushauri mbaya na mzuri.

Kwamba wewe umeweza kuona ushauri mbaya aliopokea lakini Rais ana uwezo mdogo wa kutambua mambo hivyo amashindwa kujua zuri na baya!?

Wengi wanafikiri kwa kusema hivyo wanamtetea Rais lakini ukweli ni kuwa wanamtukanisha. Pengine labda waseme kuna watu wenye nguvu wanaomshinikiza Rais kufuata ushauri fulani mbovu, lakini kusema Rais anashauriwa vibaya inamjengea Rais picha mbaya.
Wengi ni waliokosa uteuzi kama akina Kitwanga
 
Back
Top Bottom