Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,120
Tusitafute majibu rahisi kwenye maswali magumu. Kwenye siasa za kidemokrasia, uchaguzi ni kitendo kitakatifu zaidi.
Majibu ya viongozi wa CCM na serikali yake kuwa, muda uliobakia ni mchache kuweza kufanya mabadiliko ya kuruhusu uchaguzi ufanyike kwa haki na uhuru, hivyo twende hivyo hivyo, kihuni kihuni kufanya uchaguzi wa kihuni kihuni.
Kelele za kutaka reform zimeanza tangu mwaka 1993 wakati mfumo wa vyama vingi uliporejeshwa hapa Tanzania, hivyo tumekuwa na muda wa zaidi ya miaka 32 wa kuweza kurekebisha mifumo yetu ili kuruhusu kuwepo chaguzi za haki, uhuru na uwazi zifanyike lakini hatukufanya hivyo. Kilichopo sasa, tusifanye kabisa uchaguzi mpaka ili hizo reform zifanyike kwanza.
Kama sote tunajua uchaguzi ndio husimika watawala na sauti za watanzania zinasikia kupitia uchaguzi, basi tusijaribu kamwe kuruhusu uchaguzi wa kihuni. Ni bora uchaguzi ukachelewa kufanyika ili kuepusha wahuni kutumia uchaguzi kihuni kujitwalia madaraka. Tusijaribu kulifanya taifa letu kuwa taifa la wahuni.
Kilichofanyika mwaka 2019, 2020 na 2024 kilikuwa ni kitendo cha kihuni kwa 100%. Tumechoka na wahuni. Tanzania ni yetu sote, tuheshimiane.