Kusema 'Nendeni Mkalifanyie Kazi' bila kuwa na KPIs kuna walakini

Mkuu umenena kweli, human nature ipo hivyo,

Bila makaripio na strategy za maana hatutafika popote

Alisikika mwigulu akisema mama hakupi red card ukizingua anakupa ya njano ya Kwanza, atakupa ya pili ukiendelea then mwishoni atajua Cha kufanya

We can't go this way we need smart objectives ambazo zinapimika baada ya kipindi fulani
 
Mifano ni zile hospitali za acovid-19 zilizojengwa kwa muda wa wiki kadhaa tu China kwenyewe na Uingereza.
Aaaaahhh sijaelewa kwahiyo wachina walijenga hospitali ya kovid Uingereza au?
 
Samahani mkuu, pamoja na kusema ukweli halisi, kwa hali tuliyo nayo sasa Tanzania kuipata hali hiyo ni ndoto tupu!

Siyo hivyo tu, hali inavyokwenda sioni kiongozi yeyote wa kututia mori wa namna hiyo unayoielezea wewe, si katika CCM pekee, bali hata kwenye vyama vya upinzani, sioni!

Ninachokiona kila sehemu, ni juhudi za viongozi wetu KUFAIDI NAFASI ZAO wanazozishikilia. Kufaidi uhondo.
 
W
Wanatoa maelekezo ya jumla jumla kiasi kwamba hata anayeagizwa anashindwa kujua kiongozi kamwambia afanyie kazi nini?
 
Maneno ya " nendeni mkarifanyie kazi" yanaonesh hata yeye msemaji hana picha kamili nini kifanyike.
Bado nasema Magufuri alikuwa best president tangu tupate uhuru, yale yanayoitwa madhaifu sijui utesaji n.k mengine yalichochewa na wakwamishaji kufikia malengo. Siasa zinatawala hata mambo muhimu wa uwajibikaji au utekelezaji na mtu akikaa kwenye njia ya treni itamkanyaga. Huwezi kukwamisha kazi kisiasa usishughulikiwe eti haki ya binadamu zitakiukwa. Mimi si muumini wa hizo Haki za binadamu, Haki za wanawake, Haki za watoto ni muumini wa utu, uaminifu na maadili bora yasio upendeleo wala uonezi.
Hata watubwa dini tunajua umechagua kumkataa Mungu utaenda jehanmu ya moto huo ni mpango wa Mungu, sio tena udai peponi iwe haki yako.
Tunakwamishwa na akili tegemezi kuamini kuwa mataifa ya nje yatatuletea maendeleo. Never ever. HAIPO. Wao nao wanataka maisha bora zaidi tena kutokea vile tulivyo navyo.
2aafrika hatuna sera wala hatujui tunasimamia nini kwa faida gani?
Mapungufu ya awamu ya 5 ni kuingilia soko, katika sayari ya free market. Huenda hili lengo si kunufaisha wakulima bali kukusanya pesa kwao kama ndivyo wangejikita kukusanya hizo Tozo nazo ziwe affordable ili usimkamue hadi hawezi tena kuzalisha.
Uongozi wa kusifu mteuzi ni upungufu wa akili kwa mteuliwa, ni dalili ya kuwa upo kwa ajilinya tumbo lako, ni kukosa kujiamini na kudhalilisha elimu na uelewa wako. Hili limebanika mwanzo wa Uviko 19 na baada ya awamu ile kupita . Hata maprofesa na Madaktari wetu wameendelea kuonyesha kuwa Elimu yao si ya KUITUMANI TENA ni vigeugeu.
Wanasiasa wasiwe viongozi lkn bahati mbaya ni vis versa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…