Kusema Rais anashauriwa vibaya ni kujaribu kueleza kuwa Rais hana akili; naona ni ukosoaji wa kinafiki

Raisi hakosei labda atoke waziwazi akiri kuwa alikosea.

Tofauti na hapo, ikiwa nyeupe ni sifa kwa raisi na ikiwa nyeusi wateule wamempotosha na atawajibika mtia saini/mkuu wa idara/wizara n.k yeye kama yeye binafsi.

Thisi izi Afrika my furendi.
 
You have hit on the nail good. Tuna Raisi goigoi
 
 
Unaweza kushauriwa hata na watu MILIONI 30.

Lakini bado una hiari ya kuchagua ukatae ushauri upi ukuballi upi. Bado kichwa chako ndio kitaamua.

Tena katiba yetu inasema Rais halazimiki kufuata ushauri wa mtu yeyote.

Kwahiyo ukiboronga ni wewe.

Suala la watu kusema, Rais kashauriwa vibaya ni la KINAFIKI, KICHAWA, KUJIKOMBKOMBA na kumuona Rais mungu mtu, hawezi kukosea, akikosea kapotoshwa.
 
Wewe hapo ungekuwa na Rais na hivyo viakili vyako ungekuwa ndio Mwanasheria,injinia,daktari,mwanausalama nk?

Kuna watu wao ndio wenye hizo kazi Rais anawapa hints na wanampa mrejesho kama Kuna shida sometimes hao ndio wa kuwajibishwa.
 
Ukiangalia habari hii utaona kuna matatizo ya kimfumo yaliyowapita washauri, kiasi cha washauri wengine wanaotaka kutetea mkate wao kuona ni bora wanyamaze tu au washauri kinachotakiwa kusikika na wakubwa lakini si kinachopaswa kusikika.
Dah!... hatari kweli kweli...hapo penye kurekebisha mfumo ndio kipengele.
 
Dah!...tuna tatizo kubwa sana hasa kwenye utekelezaji wa tulichopanga nadhani tunahitaji sana kujifunza hapo.
 
Neno washauri limekuwa maarufu sana awamu hii sababu jamii bado inaamini mwanamke hawezi kuongoza nchi hivyo kuna watu nyuma yake kwenye kila kitu.

Ajabu akifanya jambo jema washauri hawatajwi.
 
Hadi nimekumbuka Gibson Sembuli aaaaaaaaa!!!!!!!
 
Kama hiyi habari niyaukweli basi rais Nyerere alikuwa mjinga na Mpumbavu ...huwezi kukapata ushauri kwenye mambo ya straightforward kama hayo.
 
Mbona Nyerere alishauriwa vibaya kuhusu vijiji vya jamaa na watu wakafa na hatukusema Nyerere Hana akili??
No no no Usidanganye. Watu hawakufa kwasababu ya Vijiji vya Ujamaa. Kijiji gani hicho? Kama unayo taarifa kamili weka hapa au tukuite mdanganyifu hapa jamvini.
Kiuhalisia Raisi Julius Nyerere hakushauriwa vibaya kuhusu Ujamaa ila, viongozi walishindwa kuelimisha na kuratibu dhana yake hiyo. Ujamaa Village kwa lugha ya Leo unaweza kuifananisha na Economic zone minus all the jargons- na kwaavile alikuwa katika vita ya Uchumi, mipango mingi ilivurugika na ikavunjika. Wacha kupandikiza uwongo kwa Vijana.
 
Wewe hapo ungekuwa na Rais na hivyo viakili vyako ungekuwa ndio Mwanasheria,injinia,daktari,mwanausalama nk?

Kuna watu wao ndio wenye hizo kazi Rais anawapa hints na wanampa mrejesho kama Kuna shida sometimes hao ndio wa kuwajibishwa.

Hujui maana ya Rais. Itoshe kusema hivyo.
 
Wewe unajua?

Unaweza ukatamka neno alafu usijue maana yake, ndio wewe Sasa.

Ukishakuwa kiongozi au Mtawala jua lolote utakaloshauriwa liwe zuri au Baya. Ukilifanya jua wewe ndio umefanya. Hivyo mkosolewaji wa Kwanza ni wewe kiongozi.

Kama ungejua Maana ya Rais basi ungeelewa kuwa anauwezo, mamlaka, na nguvu ya kuchunguza Jambo(ukweli wake) Kabla hajalifanya.
 
Kila mara vitu vikianza kwenda kombo, swali au maswali tunayojiuliza ni Kwanini? Why?

Kwa kawaida tunasema oh haya mambo yametokea kwa sababu ya A B C au kwa matendo ya mtu, hapa Raisi. Mara nyingi hii ni kweli na athari inaweza kufuatiliwa kwa kurudi nyuma.

Lakini wakati hili ni kweli, hatupaswi kulaumu kila kitu kwa mtu mwingine au hapa kwa washauri tu. Kama agizo maelekezo amri na what have you yametoka juu, tunaweza kurudi juu, meaning from C to A. Na amini kila mtu ana wajibu kwa kile anachochagua kukifanya. Including hawa washauri. Wawajibike au Wawajibishwe.

Anyways, the Buck stops with her.

Nachelea kusema, haya ya kudai anashauriwa vibaya ni woga!
 
Ww ndo mafuru ,eti well informed bank
 
Umemaliza kila kitu mjadala ufungwe
 
Hiyo ni tafsiri Yako,sheria zetu zinaweka distinction hasa Kwa ngazi ya Rais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…