Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Mabasi haya si mageni kwetu, baadhi yanabeba watoto wetu, wa jirani zetu na wengine watoto wetu ndio madereva kwenye magari haya, nina imani wote tutakubaliana kuwa magari haya hasa kwa hapa Dar ambako nimeshuhudia, mengi yanapumulia mashine, hayafai hata kidogo kutumiwa na na watoto wetu.
Na mbaya zaidi madereva wengi wa mabasi haya hawajali, unakuta dereva anaendesha kwa mwendokasi na ku-overtake kama mwehu, mpaka ujiuliza huyu hajui kama yuko na watoto kwenye basi?
Trafiki na polisi kwa ujumla simamieni hili, msisubiri mpaka itokee ajali ndio mje mshtuke, na neno kutaka mtaani ni kuwa madereva wengi wa mabasi hayo hawana sifa wala ujuzi wa kuendesha wanafunzi.
Mkiendela na mpango wenu wa kureact baada ya tatizo kuwa limefanyika na kisha kuzuga siku mbali tatu na kuacha utaratibu mbovu uendelee kufanyika, tutaendelea kupoteza maisha ya eatu kila siku. Polisi amkeni na kufanyia kazi suala hili, hali inazidi kuwa mbaua.
Na sisi wananchi ukikutana na school bus imechoka, wanafunzi wamejazwa kama magunia ya mkaa, dereva anaendesha rafu, tuwe wepesi kuripoti kwa mamlaka husika (askari wa barabarani au vituo vy apolisi ili hatua stahiki zihukuliewe tuepushe majanga makubwa mbeleni.
PIA SOMA
- Serikali: Hatuna mfumo wa ukaguzi wa madereva wa mabasi ya shule
- Tafsiri ya ‘School Bus’ Tanzania ni ipi? Vigezo gani vinazingatiwa ili gari litoe huduma ya kubeba wanafunzi?