Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 5,119
- 4,569
Kusema na kueneza uwongo hapa hasa ukiwa chini ya kiapo ni kosa kubwa sana (felony) kwenye nchi yo yote hapa duniani. Na baya zaidi hasa uwongo huo unaweza kusababisha uvunjifu wa amani. Hata vitabu vitakatifu vya biblia Qurani vinaliorodhesha kosa hili kuwa kati ya dhambi kubwa ambalo adhabu yake ni moto wa milele. Kwenye sheria za nchi nyingi duniani adhabu yake ni kifungo jela cha miaka isiyopungua miaka mitano.
Sasa jee huyu mgombea urais ambaye mtaji wake mkuu wa kusaka kura umekuwa ni kueneza uwongo anafikiri ataachwa hivi hivi baada ya kumalizika zoezi hili la uchaguzi mkuu?
Anafikiri kuwa ukiwa mgombea urais au ubunge au udiwani unakuwa na kinga (immunity) ya kufanya kosa kubwa kama hili? Anadhani hatafikishwa mahakamani kuongeza mashitaka yake ya uchochezi?