Kushabikia Soka la Ulaya hakutusaidii

Nafikiri watu bado wanapenda Simba na Yanga, lakini vilabu na menagement ya soka kwa ujumla ndio inayowaangusha. Soka la nyumbani likifanya vizuri utashangaa mashabiki na wakereketwa wametokea wapi, si unakumbuka miaka ile Simba ilipofanya vizuri kwenye kombe la Africa, nchi nzima ilizizima kwa ushangiliaji. Kwa sasa watu wamechoka kushabikia madogori, bora wajiliwaze na EPL, La liga, Bundesliga nk.
 
Mfumo wa uendeshaji wa team za tanzania ni kichefuchefu sana. Imagine team ina miaka 80 haina uwanja, haina kombe kubwa la afrika lolote. Sasa utasema tunafanya nin??

Team inaongizwa na the so called wazee wa club ambao mawazo yao hayapo dunia ya sasa. Nlikuwa shabiki wa Yanga ila nlianza kuona i'm just a looser wasting my time talking about tanzanian soccer.

Kifupi fanya kile roho yako inatidhia, toa uzalendo to a place or team they deserve.

Sishabikii Taifa Starz, au club yeyote ile Tanzania au africa.

Sitakaa nipoteze muda wangu kuangalia mechi yeyote ya ligi kuu bara, au taifa starz au club bingwa africa au kombe la mataifa africa.

Do what your heart tells u, and this is what i'm hearing from my heart.
 
Uchambuzi wa kiji.nga ever siwezi kuacha kumuangalia Rosicky kisha nikaangalie mpira uwanja wa taifa baada ya mechi moja kocha anafukuzwa

nitajidhulumu nafsi yangu
eti nisimuangalie Messi nikamuangalie Okwi hapa ni kufananisha chakula na mavi
wachezaji wenu wenyewe wanawaangalia wazungu ndio maana kujibadilisha majina
singano anajiita Messi
Niyonzima anajiita Fabregas
nadir haroub anajiita cannavaro
 
Sikubaliani na mtazamo kuwa kushabikia timu au mashinadno ya nje ni ulimbukeni. Kwa dunia ya sasa mpira (na michezo mingine) ni bidhaa kama zilivyo bidhaa nyingine, kama unataka watu wanunue bidhaa yako (ambako ndio kushabikia) ni lazima uwe na bidhaa bora na uitangaze sana. Sasa huwezi kumlazimisha mtu apende bidhaa ambayo haina ubora na wala haitangazwi. Ni sawasawa na kuwaambia watu waache kununua bidhaa za kutoka nje wakati za hapa ni hafifu au hazipo. Mlaji (mshabiki) akiwa na chaguo lazima atachagua bidhaa iliyo bora na atailipia bei yoyote ili mradi kiu yake inakatwa.

Huwezi kunishawishi kushabikia mpira wetu uliojaa fitna, timu zenye viwango hafifu, viongozi wa mpira wasio na dira na mengine mengi tu, hapana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…