Kushawishiwa kwa Jaji Ramadhani. Je, ni uthibitisho kwamba CCM imeoza na imeshindwa?

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
34,188
Reaction score
62,952
..tunaambiwa kwamba huyu bwana amebembelezwa ili agombee.

..taasisi yoyote inapoamua kutafuta mtu wa kuiongoza nje ya taasisi hiyo, basi uwezekano mkubwa ni kwamba walioko mle ndani wamekosa sifa za kuipeleka mbele taasisi hiyo.

..sasa ni nini kimeisukuma CCM kutafuta mgombea nje ya makada wake ambao wako-active?

..Je, ni kukiri kwamba makada na watendaji wa CCM kwenye chama na serikali wamechoka na hawana uwezo?

..kwanini wananchi wachague chama hiki, wakati wenye chama wenyewe wanakiri kwamba wameshindwa kiasi kwamba wamelazimika kwenda "nje ya chama" kutafuta mgombea?

..Je, Jaji Ramadhani atatimu makada wote wa ngazi za juu, kati, na chini, ili kusimika mfumo mpya utakaoendana na matakwa ya wananchi? Uwezo huo anao?

cc Rev. Kishoka, Kapwela, Mkandara, Ritz, Kobello, Kiranga, Nyani Ngabu, Mzee Mwanakijiji, Ngongo, zumbemkuu, ZeMarcopolo, VUTA-NKUVUTE, Mag3, Pasco, Nguruvi3
 
JokaKuu hapa ndio tutakapoona umakini wa Tanzania katika uchaguzi ulioyaeleza ni kweli kwa watu wenye maono hilo pekee lingekipumzusha ccm.
 
Last edited by a moderator:
Jaji Ramadhani ametimiza miaka mitano kama mwanachama wa CCM ili kukidhi masharti ya kugombea urais kwa tiketi ya chama?

Si amestaafu Ujaji Disemba ya 2010?

Sasa ina maana alikuwa mwanachama wa CCM wakati akiwa Jaji?
 
Mmmh, naona dodoma kitanuka, kiukweli hata aletwe masihi Yesu au mtume muhamad, au malkia au nabii yeyote wa dini yeyote kuombwa kugombea kupitia CCM atakuwa ameombwa na mfumo wa kifisadi kulinda ufisadi wao, hakika na yeye atakuwa fisadi, huwezi kulinda mfumo wa kifisadi bila wewe kuwa fisadi
 

Kama ni mwanachama si sahihi kusema amechukuliwa toka nje. Lakini pia kumbuka kuwa CCM bado haijapata mgombea. No need to speculate, time will tell.
 
Jaji Ramadhani ametimiza miaka mitano kama mwanachama wa CCM ili kukidhi masharti ya kugombea urais kwa tiketi ya chama?

Si amestaafu Ujaji Disemba ya 2010?

Sasa ina maana alikuwa mwanachama wa CCM wakati akiwa Jaji?
Hapo sasa!
 
Kama ni mwanachama si sahihi kusema amechukuliwa toka nje. Lakini pia kumbuka kuwa CCM bado haijapata mgombea. No need to speculate, time will tell.
Kiranga anasema miaka 5 haijatimia. Maswali zaidi yanazuka, je aliwahi kuwa mwanachama wa CCM?
Je, uanachama wake ulikoma lini?
Je, uanachama mwingine ulianza lini?
Nini nafasi ya mahakama katika kutoa haki ikiwa majaji wanakuwa makada wa serikali? (chama legelege huzaa serikali legelege-JKN)

Hata kama hajawa mgombea, kutajwa tu jina lake kunatia ukakasi.
Kuombwa kugombea ndilo chimbuko la swali la ZeMarcopolo. Je CCM wamefikia hatua ya kutafuta tafuta wakiwa madarakani miaka 50?

Je, walioko hawafai na kama hawafai nini uimara na udhubuti wa chama?
Je, wanastahili muda zaidi au wapewe muda wa kupunzika ili wajaipange zaidi?
 

Hakuna matakwa ya kikatiba ya miaka mitano.
Hakuna ushahidi kuwa ameombwa na CCM.
Yeye ni mwanachama, huwezi kumtenganisha na wanachama wengine. Ana haki zote.
Ni kweli kuwa kugombea kwake kunaacha maswali, ila speculations pia zinaongeza maswali.
 
Hakuna ushahidi kuwa ameombwa na CCM.
Yeye ni mwanachama, huwezi kumtenganisha na wanachama wengine. Ana haki zote.
Ni kweli kuwa kugombea kwake kunaacha maswali, ila speculations pia zinaongeza maswali.
Mkuu ima nimechanganyikiwa au kuna kitu sielewi. Samahani naomba nisome uzi vizuri tena
 
Kadi yake ni ya 1993.
Mkuu haya niliyaandika sehemu fulani, ukipata nafasi yasome.

 
Kama ni mwanachama si sahihi kusema amechukuliwa toka nje. Lakini pia kumbuka kuwa CCM bado haijapata mgombea. No need to speculate, time will tell.

..hoja yangu ni kwamba hajawahi kushika nafasi yoyote ile kubwa ya kisiasa.

..kwa mfano hajawahi kuwa mbunge. hajawahi kutumikia serikalini.

..uzoefu wake uko kwenye mhimili wa mahakama.

NB:

..habari kwamba ameombwa agombee zilitoka kitambo kidogo ktk gazeti la raia mwema. nadhani ni jarida linaloaminika.

cc Pasco, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
....CCM....
Je, wanastahili (CCM) muda zaidi au wapewe muda wa kupunzika ili wajaipange zaidi?

Hili pia nililiandika sehemu fulani humu jamvini


 
kama ameshawishiwa basi kashawishiwa na wapambe wake,ambao watafaidika na nafasi yake kama atapata,sio CHAMA
nasikia watu wanazungumza kuhusu Ujaji,hivi Warioba ni Jaji au,na ni mwanachama wa CCM
Jaji A.Ramadhani, kadanganywa na uchambuzi wa Mtatilo
 
Mpaka dakika hii sitaki kuamini kwamba Jaji Augustino Ramadhani kaamua kuchukua fomu kwa utashi wake mwenyewe. Ninachojiuliza ni mbinu gani wametumia mafisadi walioiteka CCM mpaka akawakubalia, what hold do they have on him maanake kwa vyovyote vile watakuwa wamempa offer he cannot refuse.

Hakuna watu hatari kama CCM wakinuia kukushughulikia if you don't toe the line. Ni siri gani wanayo mpaka wamemnasa kirahisi hivyo? Nasema hivyo kwa sababu sioni ni kwa vipi ameweza kuafikiana nao hadi kuchukua fomu kupitia CCM, je kasalimu amri kwa mafisadi? Since he couldn't fight them, he has joined them.

There is something very fishy here, Jaji yaonekana kalamba garasha.
 

Samahani mkuu,

Kwani kuna ajabu Jaji Ramadhani kuchukua form? Inamaana alikuwa anapingana nao siku za nyuma? Kwanini apingane nao?
 
kinachonifurahisha ni jinsi gani hata yule aliye safi anapigwa vita vya kiufundi. Je Watanzania mnamtaka nani? Maana hakuna hata mgombea mmoja ambaye hatazushiwa visababu vya mikingamo na mizengwe.

Kama tulidiriki kumpa Kada mzoefu na ameshindwa kabisa kukiongoza chama katika mstari ulionyooka na njia sahihi (Kikwete), iweje leo tumhofie Jaji Ramadhani eti ni shina gani aliwahi kuliongoza?

NI makada wangapi tena waliosomea Kivukoni na hata nchi za kijamaa ambao leo wamewageuka watanzania na wana CCM wenzao kwa kuabudu mali, utajiri na utegemezi na kuachana kabisa na dhana ya juhudi, maarifa, ujamaa na kujitegemea?

Mtu kuamua kuchagua chama ni utashi, sawa na kuchagua mume au mke, sawa na ushabiki wa Simba na Yanga, iweje tumhoji leo kwa nini hakwenda chama kingine?

Kama tutamhoji yeye kwa nini aende CCM chama kichafu, basi tuwahoji wanachama wote Milioni 7 kwa nini wanashabikia chama kinachoangamiza maisha ya Watanzania wengine Milioni 35?

Kama mtu ana dhamira ya kweli, ana busara, hekima na uimara wa kukemea, kuadhibisha, kukiri makosa na usikilivu akajitwisha mzigo huu mkubwa, basi na tumpe nafasi hiyo bila kutafuta visingizio vya kumnyima hiyo nafasi.

Mbona hatushangai umahiri wa mawaziri utitiri na watangaza nia wengine wa CCM ambao wamekaa ndani ya CCM kama vigogo na watendaji ndani ya NEC na CC, lakini bado CCM inakwenda mrama na Tanzania inaangamia katika lindi la umasikini?

Kumjibu JokaKuu- Serpent General swali lake je ataweza? nasema ni jukumu letu kumwezesha kuifanikisha kazi hii kwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita na kuuchukia mfumo wa kinyonyaji uliotuzalishia uvivu, uzembe, ufisadi na kulelea kutokuwajibika na kukomaza umasikini.

Yeye kutokuwa ndani ya NEC na CC ni jambo zuri kabisa tena sana maana akiupata uenyekiti, atakuwa hana makundi au kuburuzwa na mifarakano ndani ya chama, bali naomba Mwenyezi Mungu yeyote atakayeshinda, aisimamie haki kwa busara, hekima na uimara Taifa lisonge mbele.
 


Jokakuu:

Alikuwa jeshini na kufikia cheo cha ubrigedia. Hivyo uzoefu anao wa kiserikali. Au jeshini haiingii kwenye hesabu za kiserikali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…