Kushindwa siyo kukosa

Kushindwa siyo kukosa

Mr George Francis

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
234
Reaction score
376
SOMO LA LEO

"KUSHINDWA" sio "KUKOSA"

Karibu sana katika somo la leo, linaloletwa kwenu nami Mr. George Francis Mwanasheria na Mwalimu wa maisha. "A Lawyer and LifeCoach"

Leo napenda kuwaambia wasomaji wa makala zangu kwamba "KUSHINDWA" sio "KUKOSA"

Hapa sina lengo la kupingana na watu wanaoamini kwamba "KUSHINDWA" ni "KUKOSA " bali nataka ufahamu pia, mtu anaweza "KUSHINDWA" lakini bado anaweza "KUPATA."

Najua unaweza kushangaa kwamba hii imekaaje? Yaani mtu ANASHINDWA halafu bado ANAPATA. Ondoa shaka ni swali jepesi sana hili.

Hebu fikiria mfano rahisi tu wa Bondia Karim Mandoga, bondia ambaye amejibebea umaarufu sana mtandaoni kwa siku za hivi karibuni.

Unadhani umaarufu wa Mandonga umetokana na KUSHINDA mapambano yake ya ngumi? Jibu ni hapana bali umaarufu wake umetokana na yeye KUSHINDWA katika mapambano yake mawili ya hivi karibuni aliyopigana. Na hii ni kutokana na namna alivyojitangaza kabla ya pambano na alivyokubali matokeo baada ya pambano.

Kumbe ukishindwa hautakiwi kuwa mnyonge bali unatakiwa uendelee jasiri na kujiamini.

Si ajabu kuona kwamba endapo bondia huyo angeshinda basi leo hii hakuna mtanzania ambaye angeongelea habari zake, yaani kusingekuwa na maajabu yaani hakuna jipya. Hata mimi pia nisingemuongelea.

Lakini KUSHINDWA kwake kumempa umaarufu na kumefanya apate matangazo mengi na deals mbalimbali zinazomwingizia pesa kuliko hata hao waliomshinda katika ngumi huko ulingoni.

KUSHINDWA kumempa connection za kujuana na watu wanaoweza kumshika mkono na kumpa madili mengi ya kupata pesa au mafanikio mengine.

Kwahiyo kumbe KUSHINDWA kunaweza kusababisha wewe UKAPATA kitu kikubwa kuliko hata kile ulichokuwa unakipigania.

Je tuache kufanya tunachokifanya kwasababu tumeshindwa? Jibu ni hapana, usiache kufanya endelea kwa bidii zote kwani katika kushindwa kwako kuna ushindi uliojificha.

Mfano mimi nilishindwa (nilifeli) kidato cha nne lakini sikuacha kusoma mwisho wa siku nilihitimu chuo kikuu "Bachelor Degree of Laws." Hivyo usiruhusu kushindwa kwako kufanye ukakosa kutimiza ndoto zako. Bado una uwezo mkubwa wa kutimiza ndoto zako.

Hakuna mshindwa bure. Kila anayeshindwa kuna kitu anapata. Kama sio kujifunza ili wakati mwingine ufanye kwa ubora zaidi basi kuna fursa mpya inafunguka kwaajili yako na kukuletea matokeo ya mojakwamoja ambayo yanaweza kubadirisha maisha yako.

Harmonize na Ali Kiba waliposhindwa kutimiza ndoto za kucheza mpira hawakubaki na kujutia bali waliangalia fursa mpya katika muziki na leo hii tumawaona kama wasanii wakubwa wenye mafanikio hapa Tanzania.

Hivyo, usilie wala kukata tamaa eti kwasababu umeshindwa katika kile ulichotaka kikupe mafanikio. Haujashindwa bure bali kuna kitu bora umepata, lakini ukiendelea kulia hautakiona.

Tuliza akiri, fikiria vizuri ni kwa namna gani unaweza kuinuka upya na kufanya makubwa yatakayo washangaza wapinzani wako na kuwaacha kinywa wazi wakilalamika kuwa hukustahili kufanikiwa kuliko wao wakati wao wanajiona wana uwezo mkubwa kuliko wewe.

Nashusha kalamu yangu kwa kukumbusha kuwa

"KUSHINDWA sio KUKOSA unaweza KUSHINDWA na bado UKAPATA."

Nakuhusia na kujihusia mwenyewe kwamba "Tuendelee kupambana, kupanda na kushuka ni sehemu ya maisha. Tusivunjike moyo kwa tuliyoshindwa bali tujenge ujasiri na kuendelea kupigania mafanikio tunayoyatafuta na hakika tutayapata."

Ahsante.
--------------
It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
____________________

IMG_20220812_130143_219.jpg
 
BL

View attachment 2321904
Blessings
 
Back
Top Bottom