Kushiriki kwenye webcast live toka AfroIT

Kushiriki kwenye webcast live toka AfroIT

Kilongwe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Posts
423
Reaction score
116
Wana Jamii,Katika kuhakikisha tunashirikiana kikamilifu,Timu nzima ya AfroIT imeandaa mazungumzo kwa njia ya mtandao(Webcasting) ambapo tutaongelea masuala mbalimbali ya ICT.

Mazungumzo haya yatakuwa Live, vilevile kopi itapatikanika kwenye Website yetu na totuvi rafiki kwa wale waliokosa,ingawa tunashauri wadau zaidi washiriki kwenye hili.

Muda:Jumamosi,Saa kumi hadi kumi na moja jioni kwa saa za Afrika ya mashariki.

Mada:Fursa na Changamoto za ICT Tanzania

Jinsi ya kushiriki: Tutawaletea ufafanuzi kabla ya ijumaa,ila kitu cha kufahamu ni kuwa conference hii itakuwa ni online ambapo wewe kama mchangiaji huitaji kuwa na programu yoyote zaidi ya browser na internet.

Vifaa: Microphone,Webcam(kama unahitaji,sio lazima) na data zako.

Note: Katika hii conference kila mshiriki anauwezo wa kushare kila kitu toka kwenye kompyuta yake na kuwaonesha washiriki,hivyo kama una data zozote zilizo kwenye pdf,word,movie nk basi ziweke tayari.

Ushiriki: Ili kuhakikisha lengo linafikia,kutakuwa na kikomo cha idadi ya washiriki,hivyo tunaanza kupokea maombi ya ushiriki leo.

Kushiriki tuma e mail yako kwenda podcast@afroit.com ukijumuisha Jina lako kamili,namba ya simu,fani yako au kazi unayofanya na Nchi(Mji) uliyopo. Hatutagawa taarifa za mtu ila zitatusaidia katika kuhakikisha tunaandaa mazingira mazuri kwa washiriki.

Pia tunapokea michango ya wanajamii,je ungependa tujadili kitu gani katika webcast zijazo? Pia je ungependa kuwa mtoa mada mkuu kwenye AfroIT webcast?

Tutumie e mail podcast@afroit.com leo kwani wakati ni ukuta.

Kama una maswai,maoni au ushauri basi usisite kutembelea AfroIT Forums


Nyoni
AfroIT Group



 
hongereni sana kwa hatua hii honestly nimefurahishwa kwa hatua kubwa hii hope mwisho wa siku itaweza kukuza vipaji vya wana IT na kuwajumuisha pamoja na kuchangia hoja pamoja big up
 
Webcast itakuwa hewani kesho saa tisa kamili,tunawashauri washiriki kuingia kwenye system mapema kidogo ili kuhakikisha wanazoea utumiaji,Kuanzia saa nane na nusu system itakuwa tayari ipo online hivyo unaweza kuingia bila hofu.Details na password zitatumwa kwa washiriki kupitia e mails zao kama walivyojiandikisha,kwa sasa application za webcast ya kesho zimefungwa ila tunaanza kupokea kwa ajili ya webcast ya wiki ijayo.
 
Muda si mrefu tumemaliza conference yetu ya kwanza kabisa.

Webcast ya leo wal;iohudhuria walitoka UK,China na Afrika ya kusini,hivyo tunapenda kupata maoni toka kwa walio nyumbani,sababu gani zimewakwanza au kuwatatizo kuhudhuria conference ya leo.Tulizungumzia sana juu ya kuweka misingi thabiti kwa ajili ya webcast zijazo kwani safari ndio imeanza.yafuatayo ndio yalijadiliwa.

1.Kuhamasisha wanajamii zaidi juu ya ushiriki wa hizi conference.

2.Kuboresha njia za ushiriki wa conference,kwani kuna wadau walishindwa kushiriki kwani kwa watu wanaotumia kompyuta za cafe ingewawia ugumu zaidi kuweza kushiriki kutokana na kutoruhusiwa kusimika programu.

3.Kubadilisha muda wa conference toka saa kumi jumamosi hadi saa nane ya kila jumapili(Saa za Tanzania).

4.Kutengeneza Group ambayo itakuwa inapokea Updates za conference zote zinazofanyika,ikijumuisha dondoo na maazimio.

5.Mapendekezo ya conference ijayo ambao wadau walipendekeza iwe ni ya kupanga maazimio ya pamoja.

Hatukuweza kurekodi kwakuwa kuna baadhi ya wadau walichelewa kuingia online.Hivyo ni dhahiri kuwa kuanzia wiki ijayo wengi wetu tutashiriki zaidi na mazingira ya ushiriki yatakuwa rahisi zaidi kwa watu wa maziingira yote.

NItapost agenda ya wiki inayokuja siku si nyingi ili wadau wapate muda wa kujiandaa.

AfroIT Group
 
Back
Top Bottom