Kushiriki usafi Jumamosi ya kwanza ya mwezi ni lazima kisheria?

Kushiriki usafi Jumamosi ya kwanza ya mwezi ni lazima kisheria?

Hivi jamani wadau huu usafi wa jumamosi umekuwaje? Ni kila jumamosi ama?
Leo naelekea kazini nasimamishwa kwanini huendi kwenye usafi na kweli watu wengi walikuwa wanafyeka.

Nikazozana nao kidogo ndo wakaniachia maana niliwaambia nina funguo za ofisi hivyo nitawaweka watu nje muda mrefu.

Hivi hizi sheria huwa zinapitishwa na chombo gani au mkuu wa wilaya au mkoa akijiskia tu basi anatoa tamko.

Hivi kodi zetu zinafanya nini? Asubuhi kweli nikafyeke? Sasa shule nilienda kufanya nini? Hizo kodi zetu kwanini zisilipie watu watakaofanya kazi hizo tena sasa hivi ni kila wiki.
Mkuu wa mkoa au waziri au authority yoyote ya serikali kuu haiwezi tunga sheria mpaka wapewe nguvu na sheria ya bunge isipokuwa raisi ambaye yeye amepewa mamlaka na katiba.

Ukiona waziri katunga sheria ujue kuna sheria ya bunge na immempa madaraka ya kufanya hivyo.
 
Hilo Tamko Ni la Uchochezi Kuingilia Uhuru Wa Kuabudu Wa Dhehebu la Wasabato na wengine Siku hii Kwa Wengine Ni Siku ya Kurelax Na Familia zao

Mfano Sisi wa Siku Jumapili Ingekuwa Kila Jumapili ya Mwisho wa Mwezi Ni ya Kufanya Usafi Au IJUMAA ya Mwisho wa Mwezi Kwa Ndugu Zetu waislamu ingependeza Na Ingekuwa Mwisho wa Hilo Tamko
Mbona kuna wenzako walishaifungulia kesi mahakamani hili swala na maamuzi kama utapata time pitia case ya Ezekiah Oluch v. Ag kama sikosei ni case ya mwaka 2016.
 
Back
Top Bottom