Kuna makundi kama manne hivi yana husika.
1. Wanafunzi.
2. Wazazi.
3. Walim.
4. Serikali.
Ukiyaweka haya makundi katika power.
1. Serikali.
2. Wazazi.
Mie ngoja nizungumzie upande wa power (Serikali-walimu).
Kupungua kwa mamlaka ya mwalim kwa mwanafunzi kumesababisha baadhi ya mambo yasiende sawa, zamani kidogo mwalimu alikuwa na power juu ya mwanafunzi, (mwalim alikuwa mlezi wa mwanafunzi). Mfano, mwalim alikuwa anaweza akafanya lolote kwa mwanafunzi na asiulizwe kwa hiyo jambo hili lili mfanya mwalim aone ni jukum lake yeye kufanya vyovyote kadri iwezekanavyo mwanafunzi wake aelewe, alikuwa anaweza akampa kazi za ziada nyingi, na kumpa vpindi vya jumamosi kwaajili ya marudio.
Hali hii imeenda ikibadilika siku hadi siku, mamlaka ya mwalim juu ya mwanafunzi yameendelea kupungua, kiasi kwamba mwalim anamuogopa mwanafunzi, mwalim akifanya hiki anaonekana mkorofi/anania mbaya (umkimchapa mwanafunzi siku hizi si ajabu ukatengwa na jamii au wanafunzi kukuwinda mtaani bila kusaidiwa), kwa hiyo mwalim hivi sasa anamuona mwanafunzi wake kama kitu kingine kabisa ambacho haki muhusu, kwa hiyo mwanafunzi aelewe asielewe sawa tu atajijua yeye na wazazi wake.
Ndio maana watoto wengi wanamaliza shule ya msingi hawawezi kusoma vizuri.