Kushuka kwa kiwango cha ubora wa elimu nan alaumiwe

Kushuka kwa kiwango cha ubora wa elimu nan alaumiwe

mikejo

Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
12
Reaction score
0
Jaman ndugu zangu tunaelekea wapi?Elimu yetu inakoelekea sielewi maana nimeshangaa kutembelea shule moja ya msingi,drs la tatu had la saba kuna robo tatu kila darasa ambao hawajui kusoma wala kuandika hv kwel WALIMU,WAZAZI.VIONGOZI WA SERIKALI.MAAFISA ELIMU NA WASIMAMIZI WENGNE MPO?inaskitisha sana.
 
Kuna makundi kama manne hivi yana husika.
1. Wanafunzi.
2. Wazazi.
3. Walim.
4. Serikali.

Ukiyaweka haya makundi katika power.
1. Serikali.
2. Wazazi.


Mie ngoja nizungumzie upande wa power (Serikali-walimu).

Kupungua kwa mamlaka ya mwalim kwa mwanafunzi kumesababisha baadhi ya mambo yasiende sawa, zamani kidogo mwalimu alikuwa na power juu ya mwanafunzi, (mwalim alikuwa mlezi wa mwanafunzi). Mfano, mwalim alikuwa anaweza akafanya lolote kwa mwanafunzi na asiulizwe kwa hiyo jambo hili lili mfanya mwalim aone ni jukum lake yeye kufanya vyovyote kadri iwezekanavyo mwanafunzi wake aelewe, alikuwa anaweza akampa kazi za ziada nyingi, na kumpa vpindi vya jumamosi kwaajili ya marudio.

Hali hii imeenda ikibadilika siku hadi siku, mamlaka ya mwalim juu ya mwanafunzi yameendelea kupungua, kiasi kwamba mwalim anamuogopa mwanafunzi, mwalim akifanya hiki anaonekana mkorofi/anania mbaya (umkimchapa mwanafunzi siku hizi si ajabu ukatengwa na jamii au wanafunzi kukuwinda mtaani bila kusaidiwa), kwa hiyo mwalim hivi sasa anamuona mwanafunzi wake kama kitu kingine kabisa ambacho haki muhusu, kwa hiyo mwanafunzi aelewe asielewe sawa tu atajijua yeye na wazazi wake.

Ndio maana watoto wengi wanamaliza shule ya msingi hawawezi kusoma vizuri.
 
Mwalimu na mzazi wana mchango mkubwa katika maisha ya wanafunzi.ni jukumu la mzazi katika kufanikisha maendeleo na mafanikio ya mtoto wake.wakati mwalimu anadili na vichwa 100 vyenye uelewa na tabia tofauti darasani,mzazi anashindwaje kudili na kichwa kimoja nyumbani? Sometimes tusiwalaumu walimu katika kufeli ama maendeleo mabovu ya wanafunzi ,wazazi pia wajenge mazingira mazuri kwa watoto wao.
 
Ilikuwa ni ziara ya kiserikali ama ziara binafsi? Na ulifanya ziara kwa udhamini wa watu wa wapi? Maana haya mambo obviously yapo hapa tokea enzi ila mtu ukija kulalama leo seem kama unatoka sayari nyingine1
 
Back
Top Bottom