JamboJema
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 1,143
- 209
- Thread starter
- #21
Thanks a million ndugu yangu, Section 24 ya PSA 2002 nimeiona na nimejiridhisha nashukuru sana, ila sababu yakuuliza ilikuwa ni kupata kujua kuhusu NUSU MSHAHARA ambapo nimeona kuwa kumbe imewekwa kwenye Kanuni ya 34 (4) ya Regulation ambayo nakili bado sijaipata. Naomba sana ukiipata soft copy unitumie kwenye jumuhurihuru@rocketmail.com
Katika pekua pekua yangu kuna kitu nimegundua hasa ukizingatia kuwa hoja ya msingi ilikua ni kukinzana katika maswala ya mshahara wakati mtumishi wa serikali yupo suspension. Pia hoja zingine zilikua kuhusu mambo mbali mbali yanayotofautiana kati ya Publice Service Act na Employment and Lobour Relation Act (ELRA).
Regulation ya Public Service Act (Kanuni ya 34 (4)) kama ilivyowekwa na Mjaumbute hapo juu inasema nusu mshahara wakati G.N. No 42 Rule 27 (1) ya ELR Act inasema full remuneration. Hapa sitaki kusema sheria ipi ina nguvu kuliko nyingine ila swala nalotaka kusema ni Sheria ipi itatumika wakati Mtumishi wa Serikali yupo suspension. Tukilijua hilo ndio wote tutakubalia kuwa Mtumishi wa serikali aliye suspension anatakiwa kulipwa nusu mshahara au mshahara kamili.Katika hizo Sections hapo juu kwanza utaona wigo ambao ELR Act of 2004 imepewa, pili utapata tafsiri ambapo serikali nayo inatambuliwa kama ni Mwajiri , tatu ni uwezo/nguvu iliyopewa Labour Court. So hapa kwanza tutakubaliana kuwa kumbe Public Servant nao wanalindwa na sheria hii (ELRA No.6/2004) inapotokea kuna dispute. Hivyo nachelea kusema kuwa mfanyakazi wa serikali anapokua suspension anapaswa kulipwa mshahara kamili kama G.N No 42, Rule 27 (1) inavyosema. Ambapo kwenye the same (G.N No 42) Rule 2 inasema itatumika hata kwa Government Officials.
- Kwanza wote tunakubaliana kuwa Mahakama ndio chombo kilichopewa dhamana yakutafsiri sheria, na pia huwa kinatunga sheria (Precedent/Case Law). Hivyo basi kwa mujibu ya Ruling ya kesi kati ya The Attorney General vs. Maria Mselemu, nyingine kati ya Attorney General vs. Allan Mulla (Revision No 270 and 271 respectively) . Ambapo kati ya disputing issue zilizosababisha preliminary objection (PO) moja wapo ilikua ni "Jurisdiction of CMA to entertain the dispute where the government is part" Maauzi ya CMA yaliungwa mkono na Rweyemamu, J katika revision aliposema "…CMA had acted properly and dismissed PO number 1 the court emphasized that, under Section 2 of ELRA No.6/2004 the CMA has jurisdiction to labour disputes defined by Section 4 of ELRA No.6/2004 and those reversed for the decision of the Labour Court under Section 94(1)(a) to (f) of of ELRA No.6/2004"
Hivyo basi Mwajiri Serikali anapata advantage ya kihistoria kuwa na "employment policy or practice" kabla ya Waajiri wenzake kama ambavyo imetafsiriwa kwenye Section 7(9)(c ) ya ELRA No.6/2004. Mbali na hivyo pia alishawahi kuwa na policies and procedures that establish standard of conduct required of her employee. Kama ilivyo kwenye Rule 11 (1) to (6) of G.N. No 42. Kwa mantiki hii The Public Service Act, Regulation na Standing Orders zote pamoja na mambo mengine yanayoendesha mahusiano kati ya Serikali kama Mwajiri na Wafanyakazi wake yapo subject to ELR Act of 2004. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo;-
- Pili kama ambavyo sheria yenyewe inavyojiita kwenye Section 1 "The Public Service Act" hii inamaanisha ni sheria ya wafanyakazi wa Serikali ambapo Serikali yenywe ni Mwajiri. Hapa tunaona kwamba, na ni ukweli usiofichika kuwa Serikali ni Mwajiri kama alivyo Mwajiri mwingine inapokuja kwenye maswala ya kazi au mahusiano kazini. Achilia mbali kazi zingine za serikali ikiwa pamoja na kulinda mipaka ya nchi. Lakini hapa tunamwangalia Serikali kama mwajiri na si vinginevyo. Ambapo kihistoria ndio alikua mwajiri mkubwa alishajitengenezea Sheria na Kanuni zake mbalimbali kabla hata hii ELRA No.6/2004 haijatungwa.
(i)Article 36 (4) ya Katibu ya Tanzania inampa Rais nguvu yakuchukua hatua za kudhibiti nidhamu ya watumishi na utumishi katika Serikali. Hapa inamaanisha, kwa namna moja ama nyingine Rais ndio Kiongozi mkubwa wa mwisho katika Serikali ambayo ni Mwajiri.Ndio maana hata appeal za maswala ya kinidhamu za wafanyakazi wa Serikali zingine anapelekewa yeye kwa mujibu wa Section 25 (1) to (2) ya Public Service Act. Mfano Section 25(1)(d) inasema "where a public servant or the disciplinary authority is aggrieved with the decision in………… shall appeal to the President whose decision shall be final". Hapa ukomo wa maamuzi ya Rais ni Final katika maswala ya kinidhamu kwa Public Servant ambao ni wafanyakazi wake na yeye akiwa kama boss wao wa mwisho. Kama ilivyo kwenye makampuni binafsi ambapo Wamiliki/ Directors/ Managers wanavyotoa maamuzi ya mwisho ndani ya kampuni.
(ii)Nikilejea kwenye Section 25(1) (d) niliyoitaja hapo juu kwamba Rais decision yake ni final only katika maswala ya mahusiano ya kikazi kati ya Mwajiri (Serikali) na Mwajiriwa (Public Servant). Endapo Public Servant atakua hajalidhishwa na maamuzi ya Rais ambaye kwa mujibu wa taratibu zao ni final basi mtu huyo anayohaki ya kwenda kwenye vyombo vya sheria ambavyo ndio vina jukumu lakutoa haki. Hii ni kwa mujibu wa Article 107A ya Katiba ya Tanzania ambayo inasema "Mamlaka ya utoaji haki ktk Jamuhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama…..". Kwa hiyo sio Rais wa Tanzania ndio atatoa haki, so hapa tutakubaliana kuwa Rais ambaye ni Kiongozi wa Serikali ni Mwajiri kama walivyo Waajiri wengine. Hivyo basi Publice Service Act na Regulation zote zipo subject to ELR Act of 2004.
(ii) Kwa kumalizia ni kwamba hata Section 24 (1) ya Public Service Act inayompa Rais nguvu yakumtoa Public Servant kazini if in the interest of public. Hakifanya hivyo bila kufwata taratibu zilizowekwa kwenye Rule 13 of G.N No 42 halafu hiyo kesi ikaenda CMA itakula kwa Mwajiri ambaye ni Serikali na Kiongozi wake ni Rais. Swala la Public Interest haliwezi likafanya mtu akose haki yake na wakati tumeona kuwa mtoa haki kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania ni Idara ya Mahakama.
Wanajamii vipi hapo mmenielewa?????
Uchambuzi wako nimeupenda sana, na umenikosha! Thanks.