Kusimamishwa kwa shahada za uzamili na uzamivu --kiu

Kusimamishwa kwa shahada za uzamili na uzamivu --kiu

MKL

Senior Member
Joined
Mar 2, 2012
Posts
126
Reaction score
77
Kampala International University, Dar es SalaamConstituent College (KIU-DCC)
KampalaInternational University, Kampasi ya Dar-es-Salaam (KIU-DCC) kilichopo Gongo laMboto, Dar-Es-Salaam ni Chuo kilichopewa idhibati na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania(TCU). Kufuatiakuendesha mafunzo ya shahada ya Uzamili (Masters) na Shahada za Uzamivu (PhD)kinyume cha utaratibu na kutokua na wahadhiri wa kutosha wenye sifa stahili,Tume katika mkutano wake wa hivi karibuni ulikiamuru Kampala InternationalUniversity, Kampasi ya Dar-es-Salaam ifuatayo;1. KIUisimamishe mara moja mafunzo yote ya shahada za juu (Postgraduate) ikiwa nipamoja na Shahada za Uzamili (Masters)na Shahada za Uzamivu (PhD) katika kampasi ya Dar-es-Salaam2. KIUishirikiane na wanafunzi wote iliyowadahili katika programu zilizotajwa hapojuu waweze kuhamia kwenye vyuo vingine vyenye idhibati ya kutoa mafunzo hayo.Tumehaitatambua shahada yeyote ya Uzamiili au Uzamivu itakayotolewa na chuo hichokwa watakaosoma katika kampasi ya Dar-es-Salaam. Angalizo:Chuocha KIU Kampasi ya Dar-es-Salaam kina ithibati na kitaendelea kutoa mafunzo yashahada ya kwanza (Bachelors), Diploma au vyeti zilizopitishwa na TCU kwamujibu wa Ithibati husika tuu.
Imetolewa na:
Katibu Mtendaji
TUME YA VYUO VIKUU TANZANIA (TCU)
 
Kama kawaida, Watanzania wameliwa tena. TCU wakiweka miwani sawa kuna vyuo kadhaa vitafungiwa kama havitabadilika haraka, ikiwamo Stephano Moshi (SMMUCO) na Eckenforde.
 
vyeti ambavyo havitambulika vinanzia lini au mwaka gani maana kilishatoa wahitimu miaka miwili iliyopita.
 
Kama kawaida, Watanzania wameliwa tena. TCU wakiweka miwani sawa kuna vyuo kadhaa vitafungiwa kama havitabadilika haraka, ikiwamo Stephano Moshi (SMMUCO) na Eckenforde.

ni kweli kabisa mkuu, mfano mwaka juzi 2011 wanafunzi wa SMMUCO waligoma na kuamua kuacha chuo baada ya kugundua kozi wanazosoma hazijasajiliwa na TCU na zina curriculum mbovu.
 
Kama kawaida, Watanzania wameliwa tena. TCU wakiweka miwani sawa kuna vyuo kadhaa vitafungiwa kama havitabadilika haraka, ikiwamo Stephano Moshi (SMMUCO) na Eckenforde.

Mkuu hapo kwenye bold na hivyo ni vyuo vinavyotoa degrees hata Tanzania...!!!!?????
 
Back
Top Bottom