Kusingiziwa kunauma jamani asikwambie mtu

Ndo huwa naamini vile hadi leo maana hajawahi tubadilikia kiasi kile tangu ameanza kutufundisha darasa la 5. Zaidi alipoulizwa alikana akatusingizia kama ni tabia yetu kuacha kufanya mazoezi yake.
Kwa hiyo mwalimu alihusisha uvumi ndio akalipiza au..
 
Ndo huwa naamini vile hadi leo maana hajawahi tubadilikia kiasi kile tangu ameanza kutufundisha darasa la 5. Zaidi alipoulizwa alikana akatusingizia kama ni tabia yetu kuacha kufanya mazoezi yake.
[emoji23][emoji23][emoji23] aisee umenikumbusha tukio moja nimecheka sana japo halihusiani na mada. Kuna
mwalimu mmoja alikuwa anamfukuzia binti mmoja alikuwa anafundisha kwa kujitolea mimi nilizoea kumuita dada maana alikuwa rafiki yake sister na alikuwa home girl. Siku moja my sister alikuwa amesafiri yule mwalimu kaja kuniita darasani akaniambia kaniitie dada yako mwambie aje kule kwenu na mara nyingi alizoea kunituma hata akiwa kwao. Mimi nikafanya nilichotumwa nikapeleka mrejesho kumbe yule mwalimu wa kiume ana kipindi darasani kwetu ile anajiandaa kuondoka mkuu wa shule kaingia staff akasema walimu nani ana kipindi darasa la saba naona wanapiga tu kelele (hii tuliambiwa na mwenzetu aliyekuwepo ofisini muda huo) aisee alikuja kwa hasira alitutandika fimbo za mgongoni kama anachapa ng'ombe kwa madai tunapiga kelele kwenye kipindi chake yaani alipiga hajali amepiga mgongo, kichwa, mkono, ye twende tu yaani alipiga hadi kipindi kinaisha, anauliza swali mkimbwela kidogo piga sana, sitasahau sijui alikuwa ndio ameahidiwa atapewa siku hiyo maana sio kwa mihasira ile.
 
Nilisingiziwa nimepita na best friend wa my better half. Ilikuwa ndani mtiti nje mtiti. Imani ilishuka jumla jumla.
 
Hahahaaa! pole mkuu maana mie situ naogopa ni bakola hadi umri huu, Mie hizo 5 tu nlishikiliwa je mgongoni. But sometimes hawa mwl hasira zao wanakujaga kumalizia kwetu.

Mie mwanagu nitakuwa namsikiliza sana kuliko mwl hata kama kosa ni lake.
 
Pole sana
Hapo ndio utajua kuna watu wengi wako jela kwa kusingiziwa.
Imagine mtu kahukumiwa miaka kwa kosa ambalo hajalifanya.
Umefanya niwaze sana kwa kweli
Mimi niliwahi kushtakiwa kwa jambo ambalo wala nilikuwa silijui ila niliadhibiwa na kulazimishwa kukubali kosa
Kwa kweli Africa ni shida yaani bahati ilikuwa ni shule tena hata sijabalehe halafu nabambikiwa kesi, yaani ukiukaji kabisa wa haki za watoto
Na hapo ndio tumepata uhuru hata miaka 10 haijafika
Anyway pole sana dear nenda tu ukasafishe majeraha hayo maana bila kumkabili huwezi kusamehe
 
Asante mkuu yaani ni kweli ndio unaelewa kweli si wote walioko jela ni wahalifu
 
Huo ndio ukweli,uongo wa kusingiziwa unauma sana. Mimi kama mwalimu kijana na hata wale walimu wenzangu vijana najua mnajua ninachomaanisha.ila mungu atulinde tu.maana sometimes mtu unakua unawaza mengi sana.
 
Nakumbuka nikiwa O level wanaume tulikua boarding halafu kina dada walikua wanasoma day,kuna siku tunaingia kwenye pindi tukakutana na kina dada wanatoka basi zile purukushani za kupishana,kuna dada alikua ana chura balaa akashikwa tako halafu nikasingiziwa ni mimi

Daah nikapelekwa staff,walimu walinishambulia balaa,nilipigwa kama paka mwizi!
 
Huo ndio ukweli,uongo wa kusingiziwa unauma sana. Mimi kama mwalimu kijana na hata wale walimu wenzangu vijana najua mnajua ninachomaanisha.ila mungu atulinde tu.maana sometimes mtu unakua unawaza mengi sana.
Haha pole mkuu ila na nyie mnahukumiwa kutokana na matendo ya baadhi yenu si unajua mtu uking'atwa na nyoka
 
Maskini pole yaani watu huwajui tu demage wanayofanya kwa wenzao
 
WATAKUJA WALEEEEE.... WAZEE WA CHAI YA RANGI ISIYO NA SUKARI NDANI YA HUU UZI, AMA KWELI HII DUNIA INA MAAJABU SANA MAANA INA WATU, VIATU, VIJITU, MIJITU, MAJITU, VIJIMTU NA MAWATU.

My name is...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…