[emoji23][emoji23][emoji23] aisee umenikumbusha tukio moja nimecheka sana japo halihusiani na mada. Kuna
mwalimu mmoja alikuwa anamfukuzia binti mmoja alikuwa anafundisha kwa kujitolea mimi nilizoea kumuita dada maana alikuwa rafiki yake sister na alikuwa home girl. Siku moja my sister alikuwa amesafiri yule mwalimu kaja kuniita darasani akaniambia kaniitie dada yako mwambie aje kule kwenu na mara nyingi alizoea kunituma hata akiwa kwao. Mimi nikafanya nilichotumwa nikapeleka mrejesho kumbe yule mwalimu wa kiume ana kipindi darasani kwetu ile anajiandaa kuondoka mkuu wa shule kaingia staff akasema walimu nani ana kipindi darasa la saba naona wanapiga tu kelele (hii tuliambiwa na mwenzetu aliyekuwepo ofisini muda huo) aisee alikuja kwa hasira alitutandika fimbo za mgongoni kama anachapa ng'ombe kwa madai tunapiga kelele kwenye kipindi chake yaani alipiga hajali amepiga mgongo, kichwa, mkono, ye twende tu yaani alipiga hadi kipindi kinaisha, anauliza swali mkimbwela kidogo piga sana, sitasahau sijui alikuwa ndio ameahidiwa atapewa siku hiyo maana sio kwa mihasira ile.