Kusingiziwa kunauma jamani asikwambie mtu

Mbona hujaisema ile waliyokusingizia eti mimi na wewe tulikuwaga tunabanjuana kwenye shamba la mihogo unapokwenda kuchota maji ziwani au umesahahu!!!!
 
Mimi nilikuwa mkorofi tena mkorofi haswa, jeuri, ukinizingua mchana usiku lazima upite mitaa ya kwetu uchezee mawe au kipigo kama nakuweza, kuvunja vioo vya shule , kugomea waalimu , na mengine mengi ambayo nitakuja kuyajumuisha siku moja kwenye struggle to success stori yangu/zangu,.

nirudi kwenye mada ,vya kusingiziwa vingi ila hiki ndo kinaniumaga zaidi, ilikuwa ndo kipindi smartphones zimetoka , kuna sehemu me napaita safe place/zone nikipiga mtu, nkizingua skani naenda kuchill na wadau kihvyo ani , sasa kuna dogo akaiba smartphone ya mzee wa jirani na safe zone , siku hyo natoka skuli mzee huyu hapa alikuwa mshkaji wangu hatari kanambia dogo njoo nielekeze ishu fln kwenye cm sielewi , nlikuwa na miaka kumi na tano kipindi hiko, nikaenda ghafla kanikwida mtama chali anaanza kuuliza simu yangu iko wapi 😭😭 me machozi tuu, sina majibu na school uniforms zangu nachezea kipigo.
Akasema hutaki kujibu sasa utaona nitakachowafanya alikuwa na kijana wake wa kazi kanipakiza kwenye toyo hao tukaenda somewhere kunishusha wakanipeleka kwenye banda la kuku ghafla nawakuta machalii tunaokutanaga safe zone wamepigika hatari wote wamenitaja me kisa sikiwepo isipokuwa mwanangu sana Mr A popote ulipo mungu akubariki kama upo humu me ni E kaka, .

machalii kuulizwa tena wakakana wakasema siyo huyu ila isipokuwa mmoja ambaye ni sbd b , akawa anakazia me nlichukua nkamshirikisha ani hapo nalia kama my mother ndo kafa ani alafu dogo anakazia si mnaona anavyolia ukweli unauma,
nikavuliwa nguo nkapigwa shoti , me sikukubali coz sijafanya , damu puani manundu kila kona sikukubali ikafika zamu ya sbd B kupigwa shoti mbona alikubali kuwa yeye ndo kaiba simu akaenda kuitoa kwenye banda la majani dooh nlishindwa kumpiga nlikuwa hoi , granny alifanya kuja kunibeba kunipeleka hospitali , kesi ilienda ishia mahakamani
naumiaga hadi today , nlipokuwa nakuja kusalimiwa hospitali mtu akiniambia pole ndo uache kuhang na wezi machozi na uchungu kama wote , ila yule dogo hajafikaga mbali alikuja kufungwa 2 years kwa kosa la wizi na uuzaji wa bangi.

ILA MPAKA LEO HUWA NINAE KOVU LA HYO MSALA KILA NIKILIONA LAZIMA NILIE AU NIKOSE AMANI
 
Hili jambo ni uduwanzi kweli yaani mtu sijui anapata faida gani kukusingizia yaani nina visa vingi vya kesi ya kusingiziwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…