Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Ni kipi wachina hawapati hivi sasa kwakuwa hiyo bandari haipo? Kama bidhaa fake ziko za kutosha, kama ni malighafi bado wanapata tena kwa bei ya kutupwa. Jenga hoja za kueleweka acha kuwa kasuku.
Ikiwepo bandari inakuwa ni mkataba. Huwezi kutengua ila kuufuata. Na kwa kutumia hiyo hiyo bandari kuna urahisi wa kufanya mambo yao. Lakini sasa hivi japo yanafanyika lakini hayana ''kibali''. Fikiria nje ya box na usiwe kama nyumbu!
 
Mchina kopa pesa kwingine mpe tender afanye kazi, lakini umkope yeye then kila kitu kitakuwa chini yake, Kule Lindi kuna mradi wa LNG umesimama ile kampuni ni Kifaransa ni wazungu lakini ninahakika hawawezi kuafikiana na Serikali maana walikuja kipindi cha Kikwete sasa mambo yamebadilika ni win win situation alikadhalika na mradi wa Mchumchuma wachina ndo waliomba wawekeze pale lakini mwisho wa siku ripoti waliyowasilisha wao ilionyesha kuna mali 40% kumbe kuna mali 85%.
 
Ikiwepo bandari inakuwa ni mkataba. Huwezi kutengua ila kuufuata. Na kwa kutumia hiyo hiyo bandari kuna urahisi wa kufanya mambo yao. Lakini sasa hivi japo yanafanyika lakini hayana ''kibali''. Fikiria nje ya box na usiwe kama nyumbu!

Wanaweza kufanya kwa urahisi iwapo kuna bandari, sisi hatuna ulinzi wa nchi?
 
Ujinga huu ndio anaommezesha kabudi
 
Duh... wewe ni msomi kweli kweli.asante kwa uchambuzi mzuri. Pengine wakubwa wataiona hii makala na watareview maamuzi yao mara moja. Kujikwaa si kuanguka.
Kwa awamu hii? Labda kumtundulisu. Ushaambiwa haambiwi cha kufanya, ukijaribu kumwambia ndio unapoteza kabisa (ktk sauti ya jiwe)
 
Sioni lolote zaidi ya urafiki binafsi kati ya zitto na jk
Unataka kutuambia mradi huo umesitishwa kwa sababu ya kumlink JK n ZZK? Naanza kunusa harufu hiyo sasa kwa hilo neno lako
 
Watanzani wenyewe ndo hawa! Kazi kwelikweli. Unaambiwa mradi ungetekelezwa kwa FDI wewe unazungumza Habari za hela ya Serikali! Sijui kama unaelewa maana ya FDI?

Kwa aina hii ya watanzania tusitegemee chochote cha maana.
 
Magufuli ni mzalendo wa kweli Hawezi kubali mkataba wa kuikabidhi bandari yetu kwa nchi nyingine kwa miaka 100. Kama huo mkataba utakuwa bila kipengele cha wajenzi (funders) kuiendesha bandari kwa miaka mia JPM anaweza kuufikiria upya lakini siyo huu wa kinyonyaji Kabisa. Jamani kina Zito muwe na mshipa wa aibu. Siyo kila kitu kupinga tu!
 
Kuna watu walishategesha huu mradi wawe wanachuma fedha mpaka vizazi na vizazi huku wabongo wakitaabika.... sasa MKEMIA akafanya TITRATION ya huu mradi kwa muda mrefu kwa kutumia double indicator , kila anapopata jibu linakuwa na linakuwa na insoluble precipitation yenye odour smell. Alivyojaribu ku calculate mole zake katika ionic reaction akawa anasikia pop sound kama anaunguza hydrojen vile. Mtaalamu aka ngastuka akaufyekelea mbali.
 
hii ndo kwanza trela mbona...picha kamili bado kabisa hapo!
 
Zito mi Sawa nakushukuru wale wanaosifia maghorofa ya sauz wakiponda maisha ya hapa lakini Waangalie Waafrika wa kule Ma wa hapa na yupi anatembea kifua mbele? Waache hizo porojo za cijui viwanda cijui kuizidi bandari ya Rotterdam what Nonses watanzania wote hatukuzaliwa Jana? Hao hao wanao shabikia bandari ya Bagamoyo ndiyo walewale waliwajaza watanzania Neema ya gesi ya mtwara lakini......
 

Haa jaami nimecheka sana lakini hongera kwa kwa jinsi ulivyoipresent hiyo hoja ki chemistry
 
"Lakini mimi kwa jicho kali naona itachukua miaka mingi zaidi ya nusu karne Tanzania kuanza kupata chochote kwenye mapato yatokanayo na huo mradi."

Kulingana na uzi wa Zitto,Faida/Mapato yatokanayo na mradi huo ni yapi?
 
Tayari umehaharibu mjadala kwa kutumia maneno makali ya kashifa na dharau.
Ungepukiwa na nini kama usingetumia neno 'upunguani'?

Ni kitu cha ajbu kumuona mwenzio punguani sababu mmetofautiana vipaumbele au misimamo.

Kila la heri kiongozi.
Sorry mkuu
 
Habari hii ya usitishaji wa mradi wa Bagamoyo ni neema ya ajabu sana kwa majirani zetu wa kaskazini.
Hawakutufunga penalti tu, bali wametutoa kabisa kwenye daraja la timu hizo.

Walikuwa na hofu kubwa sana na Bagamoyo, kiasi kwamba nao wanaharakisha mradi kama huo huo uliokuwa umepangwa kufanyika Bagamoyo. Nadhani ma'Bulldozer' hayapo mbali kuanza kazi.

Tutege masikio tu kuisikia DONGO KUNDU ikiunguruma.

Hapa tutakuwa tumelishwa nyongo, kama kweli masharti ndio yalikuwa hayavumiliki!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…