Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Nyinyi ndio wale watz wachache mnaotegemea akili za mtu kuishi.

Yaani kila mtu unataka akubaliane na huyo zitto, kwanini una imani naye kiasi hicho!!!

Kwenye hili swala mnaonyesha upumbavu kiwango sana bila kusita.

Najua baada ya Spika kulala mika jana , saa hzi akili zishakuruka unashindwa uegemee upande gani.
 
Najua baada ya Spika kulala mika jana , saa hzi akili zishakuruka unashindwa uegemee upande gani.
Ndugai ni wa kuniyumbisha mimi[emoji23][emoji23][emoji23], huyo anayumbisha akili za nyumbu pekee, angalia saa hii keshakuwa role model wenu[emoji23][emoji23].
 
Kutoka bagamoyo hadi dar nikilometa chache sana.Ujengaji wa bandari kubwa ya bagamoyo itasababisha bandar ya dar pamoja na tanga kufa.Na tukumbuke mradi wa bagamoyo siomsaada ile ni investment yao kwa gharama yao.Baada ya kujengwa lazima itakuwa chini yao kwamiaka ili irudishe pesa yao na riba.kipindi hicho chote bila kujua nimiaka mingapi bandar zetu hasa hizi mbili zitakiwa hoi.Investment hii ni nzur lakin why bagamoyo!nasio tanga!.Tunaweza kujimaliza bila kujua,sidhani kama raisi anaweza kuruhusu kitu hicho kitokee kwenye utawala wake,ataacha ili labda watawala watakaomfuata waamue hilo.
 
Kwi kwi kwi swali zuri.. akijibu nitagi.
Anasubiri afanye mazingaombwe wamchague tena

Nope huo mradi ulikuwa unajibeba wenyewe, yaani hela ni za wachina na wa oman ila sisi kwenye hati ndo ilitakiwa tufanye ujasusi wa kiuchumi wa maana haswa!
 
Nope huo mradi ulikuwa unajibeba wenyewe, yaani hela ni za wachina na wa oman ila sisi kwenye hati ndo ilitakiwa tufanye ujasusi wa kiuchumi wa maana haswa!
Unaifundisha china ujasusi wa kiuchumi[emoji16][emoji16].

China anafanyiwa ujasusi wa kiuchumi na nchi kama marekani au canada hivi, sio hii nchi wanaoyoishi akina zitto kabwe.

Yaani wanaume waweke mezani $10b,wewe upeleke vitambi, halafu utegemee usawa kwenye makubaliano[emoji23][emoji23], tunafikiri vibaya sana.
 
Mbona Tanganyika inamiliki bandari za Zanzlbar baada kuvamia
 
Ujinga ni mzigo mzito sana sema aliyeubeba hasikii uzito wake
 
Hili swala la Bandari ya Bagamoyo ni jambo sensitive sana. Ni jambo ambalo linaweza kuja kujeuka kuwa kashfa ya kuuza nchi kama halitaangaliwa vizuri. Nadhani serikali inafanya vizuri kuliangalia upya na kitaalamu zaidi (kama ndivyo) kabla ya kusaini huo mkataba. Haya siyo mambo ya kutanguliza tu siasa mbele bali utaalamu ndiyo muhimu kutanguliza.
Nchi hii wananchi tu mashahidi wa mikataba mingi mibovu ambayo serikali imesaini na haina tija kwa taifa letu. Licha ya faida za mkataba ni lazima kufanyike "a thorough assessment" ya eneo husika na kufahamu kuwa ni vitu gani tunaweza kupoteza.
Inaweza kuwa muwekezaji keshaona kitu cha ziada kitakachomnufaisha sana na sisi hatukioni. Kwa mathlani, wanaweza kuwa wanaondoka na mamilioni ya tani za samaki, prawns, kobe wa baharini nk.nk. wakajitajirisha kwa hilo sisi tubakie tunachekelea bandari tuu kama mazuzu.
Bandari hiyo ni muhimu saana tena sana. Tunaiomba serikali ijipange vizuri kuhakikisha kuwa huo mkataba unakuwa makini sana. Muda wa kuisimamia uwe realistic, namna ya kuhakiki mapato yake iwe wazi na isisimamiwe na wao peke yao tu bali kuwe na experts wengine kutoka kona nyingine ya dunia, tena kinzani.
Jeshi letu liwe trained kulinda sehemu zenye miradi kama hiyo kuhakikisha hakuna sub-marine zinawasili usiku na kupakia mizigo.

Usingizi wetu umeshatuponza sana na kwa muda mrefu, tuutumie wakati huu wa serikali hii makini kuhakikisha kuwa kila kitu kinafanyika vizuri kwa maslahi mapana ya taifa letu.
 
ZZ
ZZK anawaona awamu ya 5 kama washamba na kana kwamba waliopita ni "washua" na walikuwa very intelligent kwenye economic diplomacy.
Pengine atusaidie kujibu, kwanini toka 2012 kwa mara ya kwanza draft ya kwanza imeanza, ikaja 2013 yote kimya, ikaja 2014 yote kimya na 2015 mpaka August uchaguzi unapamba moto kimya...
Huo muda ni mrefu sana toka awamu ya 5 anaowaona washamba wa economic diplomacy wakiwa madarakani. Ni wakati huohuo Rais wetu aliepita mpaka akapewa U-profsesa wa heshima hukohuko China.

Akiweza kuwa msemaji wa economic diplomacy ya awamu ya 4 na wao kuwa hesitant mpaka muda wao ukaisha, pengine tunaweza kumwelewa.

Suala la exports ya agro products kwenda Oman hata sasa laweza kufanyika kwa bandari hii hii. Ila tukubaliane, exports ya agro-products iwe ni nyama, samaki, mchele wa pisholi unaolika sana Oman, matunda na mbogamboga, hapa panahitaji uwekezaji wa KILIMO cha kibiashara ambapo tunahitajika kutoka kwenye subsistance farming na kwenda kwenye commercial/industrial farming. Na ili tufanye hivyo tunahitaji technology na consultants wa ku-transfer know-how kwenye production, packaging, logistics, legal na financial management. Haya hayakuhitaji uwepo wa Bagamoyo port. Tukubaliane kwa muda mrefu Wizara ya fedha na imeshindwa kuwa na visionaries wa kuja na comprehensive project financing kwenye agri-business.

So far, ZZK awe mkweli na asichangenye watu kwa ukweli na matango pori ili kupata cheap popularity kwenye facts
 
Ndugu kwa perspective ya pure economic inayo tizama tuu uzalishaji na faida bila kujali athari nyinginezo upo sahihi. kwa sisi political economists bado tunaona kuna haja ya kuwa makini na mambo mengi zaidi ya faida unazo ziona wewe.
 
LABDA TUANZIE MBALI KIDOGO,,HIVI MTU ANAYEJENGA HOTEL YA KISASA HATA YA BILLIONI 10 AU 20,,KWENYE ENEO LA ARDHI LA HEKTA 20 KWA MFANO,, HIYO ARDHI ALIYOTUMIA KUJENGA HOTEL INAKUWA CHINI YA UMILIKI WA NANI?
 
Hapo Mh Zuberi umeelezea vizuri, lakin bado kwa upande wa Serikali kuna uwezekano baadhi mambo hawajataka kueleza wazi wazi kuhusiana na huo mradi, kwanza ni vizuri tukafahamu je baada ya huo ujenzi hao waajiriwa wote wangekuwa watanzania au ni hao hao wachina wenyewe? je mgawanyo wa mapato ya faida ya bandari baada ya ujenzi ungekuwa vipi?? kwa ninavyo fikiri kuna mambo flani ambayo serikali haijatueleza bayana, na sidhani kama mradi huu umesitishwa kwa nia mbaya bali kuna uwezekano mkubwa kukawa na vifungu vya kinyonyaji katika makubaliano, ambapo Mh Raisi wetu ameona mradi huu hauna manufaa.
 
Pesa ya kujenga mradi haitoki Tanzania ni pesa zao wenyewe usidanganywe na watengeneza propanganda wa CCM
 

Kinachokwamisha mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni mkopo aliokwenda kuomba ulaya na America ndipo wakampa mashariti makali kuwa lazima awatose wachina kwanza ndipo apewe pesa, sasa kagundua watanzania watachukia wakiona hakuna Bandari ya Bagamoyo ndipo wamebuni propanganda kibao za kuwasingizia wachina kuwa wana mikataba mibaya na hatari
 
Kuna kikundi cha wajanja wachache huko CCM kimeomba milion 100 kama pesa za kutengeneza vipeperushi Uongo visingizio na kila aina ya vishawishi kuwaaminisha wananchi kuwa mikataba ya wachina ni mikataba mibaya, Bandari ya Bagamoyo sasa ni fursa kwa cyprian Musiba na Le mutuz kula pesa za Bashite na mtukufu malaika kiulaini, Naibu Rais kampelekea Bajeti mtukufu Rais kapitisha wapewe pesa za propanganda ni Aina ya matumizi mabaya ya pesa za umma, wachina wanajipanga kuwaadhibu CCM kwa kutowapa pesa za kuendesha uchaguzi mwaka 2020 kwani wamegundua CCM ya sasa si ile CCM rafiki waliyorithi toka kwa Nyerere
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…