Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Kifupi hoja za ZZK zinaeleweka na kumpinga au kumkosoa lazima pia uje na hoja zinazoeleweka maana si kila msomaji anaujua uchumi kiundani ila ukiweka maelezo vizuri basi kila kitu kitaeleweka na hata asiye mchumi ataelewa.
Mwandishi kaeleza vizuri madhara ya huu mkataba. Sawa upime hayo madhara na hiyo ajira ya wachina. Kama huelewi basi ni kwa vile hutaki tu kuelewa. Waswahili husema ukopenda chongo huona kengeza
 

Kama hofu ni kuhusu ulinzi basi natumai watanzania sisi ni wavivu sana wa kusoma au tuna hitilafu kubwa sana kwenye uelewa wetu. Ukisoma The Belt-Road Initiative unakuta bandari kama hii ya Bagamoyo imejengwa kula Pakistan kwenye mji wa Gwadar, kwa mfumo wa masharti haya haya ya bandari ya Bagamoyo. Serikali ya Pakistan imeenda mbali na kukubali kuendesha mradi huu kwa muda wa miaka 40 wakati serikali ya Jakaya ilikubali kuendesha bandari kwa muda wa miaka 30.

Hoja ya hofu ya ulinzi nadhani haina mashiko sana kwasababu naamini nchi kama Pakistan wako mbele sana kiusalama kuliko sisi watanzania na hata changamoto zao za kiusalama ni kubwa kuliko sisi.Kama Uchina ingekuwa ni tishio kiasi hicho ambacho nchi za kibepari zinataka kutuaminisha basi Pakistan naamini ingekuwa imeshaukataa huu mradi muda mrefu sana.

Nilikuwa nasoma Africanarguments (https://africanarguments.org/2018/07/18/politics-ports-horn-war-peace-red-sea-rivalries/)wiki chache zilizopita nikaona jinsi ambavyo nchi za pembe ya Afrika kama Djibouti, Eritrea, Sudan na Ethiopia zinachangamkia miradi ya bandari kwa kuangalia sana faida za kiuchumi. Kama ulivyosema Tanzania ni lazima ijifungue kwa Oman, nchi za pembe ya Afrika zimejifungua kwa falme za Kiarabu, mataifa ya ulaya na Uchina.

Miaka 10 mbele nchi hizi zitakuwa kituo kikubwa sana cha biashara hapa duniani, juzi kuna kikao cha Umoja wa Afrika kinaitwa African Union High Level Implementation Panel (AUHIP) kiliongozwa na Thabo Mbeki ujumbe kutoka Algeria ulipendekeza waanzishe The Red Sea Forum ambayo itatunga sheria ambayo itasimamia uwekezaji na ushindani kwenye pembe ya Afrika kwa nchi zote zenye maslahi kibiashara na kiulinzi (https://www.theeastafrican.co.ke/op...world-powers/434750-5080848-99nd7b/index.html). Hapa wakimaanisha nchi kama Ethiopia, Eritrea, Djibouti, Sudan, Algeria, Egypt, Turkey, China, U.A.E na Saudi Arabia.

Katika kitu ambacho serikali ya Tanzania imejipiga risasi mguuni basi ni hili la bandari ya Bagamoyo, kwasababu hata isopkuwa Tanzania, hii bandari ni lazima ijengwe inaweza ikawa Kenya au Msumbiji. Maana kimakakati ni kwamba lazima nchi moja ya Afrika (Kenye, Tanzani au Msumbiji) kupitia bahari ya Hindi ijiunganishe njia ya bandari Gwadar nchini Pakistani ili kuepusha usumbufu wa safari ndefu ya meli kupita kule Pasifiki kwenye mifereji ya Malacca, Sundar au Makassar.
 
serikali ya wanyonge bana inachekesha kweli. inajadili maslahi ya kitaifa badala ya kutoa brief kwa wanyonge inayowatumikia eti inafanya siri. wewe umepenyezewa waliyojadili sisi wanyonge tutapenyezewa lini? kwanini nchi inaendeshwa kisiri siri?
 

Naona hujasoma hapo juu kuwa huo mradi ni uwekezaji wa nchi tatu, China kwa ujenzi na pesa zao, Oman kwa pesa zao na Tanzania kwa eneo tu.

Hivi mnachokisoma huwa hamuelewi au ni upunguani tu?
 
Kumbe mimi umeona post yangu imekuchoma 💉💉💉💉 ukaomba itolewe. Kuandika uandike wewe.. sisi tunaojua kukugusa kwenye ukweli umeniogopa.

Sasa nakupa cha kufikiria.. nataka nije nifungue uzi nikuulize maswali. Majibu uyajibu ndani ya 90 seconds. Nakusubiria tupange siku na muda.

Kama mdau wa JF mwenzangu... umetia aibu kuogopa post.. kumbe upo hivi.. muoga eeeeeeeeeh.. nimekushusha zaidi..
 
Kama huu mradi ungekuwa unafanyika kule kijijini kwetu Chatu nina imani ungefanyika. Ila kwakuwa ulipangwa ufanyike kijijini kwenu Kifutu, wacha tu usitishwe.
 
Hela inatoa China na Oman, acha ushabiki maandazi...
 
terms and conditions zake zipo beneficial kwa nchi au ndio kama mkataba TICTS na wa KADCO (kilimanjaro airport development co.?)na mikatabamingine kama wa gas nk
 
terms and conditions zake zipo beneficial kwa nchi au ndio kama mkataba TICTS na wa KADCO (kilimanjaro airport development co.?)na mikatabamingine kama wa gas nk
Nadhan ni beneficil afadhali kuliko chatu intenesino
 
Si kila mada kila mtu anaweza kuijadili kwa hoja! Kuna baadhi ya mada nadhani huwa zinakuwa juu ya wachangiaji wengine! Wasamehe buree
Naona hujasoma hapo juu kuwa huo mradi ni uwekezaji wa nchi tatu, China kwa ujenzi na pesa zao, Oman kwa pesa zao na Tanzania kwa eneo tu.

Hivi mnachokisoma huwa hamuelewi au ni upunguani tu?
 
Wanasiasa ni wa ovyo Sana leo anasema haya lakini serikali wangekubaliana na mwekezaji wangekuja na hayo masharti magumu
Nakumbuka mwanzo ni hao hao waliopiga Vita bandari hiyo walisema kwa nini tusiboresha bandari ya Dar ? Leo hii wanasema tofauti duuuuuu Zito kuwa na aibu hata kidogo ukiendelea hivyo sidhani hata jimboni kwako utachaguliwa tena
 

Nani anaekusanya kodi jimboni mwake!,Mlishasenma ampeleki maendeleo majimbo ya upinzani, hata wabunge wahamaji wameyathibitisha hayo kwann muwalaum wapinzani kushindwa kutimiza ahadi zao waachieni wakusanye kodi za majimbo yao then muone.
 
Zito Unaongea Pumba Sana Kwann Wasingeboresha Kwanza Bandari Hizi Tatu Mtwara Dar Na Tanga Pia Uwoni Kwamba Hiyo Bandari Mpya Ya Bagamoyo Ingetengenezwa Ingeasiri Bandari Hizi Mbili Mtwara Na Tanga Tena Zingekufa Kabisa Na Port Ya Dar Nayo Ingekuwa Tia Maji Tia Maji Ingepumuria Gesi Nakingine Hata Iyo Bandari Ingewepo Ingewanufaisha Sana Wachina Na Warabu Sisi Tungeamburia Ajira Ambazo Hata Hizi Bandari Tatu Zingeboreshwa Ajira Zitakuwepo Hasa Kama Ya Mtwara Pia Kuna Utajiri Wa Gesi Pato Kubwa La Taifa Litaingia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…