Kusitishwa Mradi wa Bagamoyo SEZ kumedhihirisha udhaifu wa Rais Magufuli kwenye Uchumi na Diplomasia

Hata mimi hapo mwanzo nilielewa kama wewe. Sikuwa najua kuwa mradi wa bagamoyo ulikuwa ni zaidi ya bandari. Mradi huu ni zaidi ya bandari ndo maana isingekuwa rahishi kuufanikisha kwa kwa kuboresha bandari zilizopo. Sasa namuunga mkono Mh Nduga nduga na Mh Zitto kuhusiana na mradi huu ambao serikali imeamua kutoutekeleza.
 
Umesema kwamba SGR na STIEGLER'S ikikamilika inaanza kutufaidisha moja kwa moja,uko sawa kwa kiasi fulani lakini nikukumbushe miradi hii miwili ni nusu biashara nusu huduma,sio kama bandari mpya ambayo yenyewe ni biashara kwakwenda mbele.ukitaka kujua umeme ni huduma angalia kuna wengine wanalipa elfu ishirini kufungiwa umeme wakati wengine wanalipa zaidi ya laki moja kufungiwa umeme.kwahiyo stieglers ikiisha ufanisi utategemea na miundombinu ya usafirishaji na uendeshaji wa shirika pia.kuhusu SGR kama bandari haitafanya kazi kwa ufanisi na kuwa lango la biashara linalotegemewa na nchi jirani basi tutegemee SGR kuwa huduma tu maana haitaweza kujiendesha ikitegemea abiria na parcel zao na mizigo kidogo ya kusafirisha,hapa ndipo panaingia mradi wa bagamoyo SEZ.
 
Sina cha kuchangia kwa sababu mradi huu uliitaji zaidi ujadiliwe bungeni kuhusu masharti zaidi ya uendeshaji maana mzigo uliowekwa sio wakitoto lazima masharti yawe straight and clear kabisa
 
Wanasiasa wa nchi hii wakati mwingine muangalie maslahi ya nchi na sio kupinga kila jambo serikali inayoamua, mmekuwa mkituaminisha kuwa deni la taifa linakuwa halafu leo unataka wachina wapewe kipande chetu cha ardhi kujenga bandari yao hapo kwa matrilion yote hayo hivi hayo tutayalipaje? Na kama hayotowalipa wao watafaidika na nini? Yaani humrusu mtu aje kushindana na wewe kwenye biashara na mtaji wake mkubwa unategemea nini.

Kwa kweli sio kila uwekezaji unatija kwa taifa binafsi naunga mkono maamuzi za serikali kwa kuvunja huu mkataba hapo tulikuwa tunapigwa asubuhi kweupe. Hongera Mh. raisi JPM kwa kuweka maslahi ya taifa mbele.
 
Zitto kwenye hili umeingia cha kike. Uharaka wako kuchangia mambo ya kitaifa utakugharimu sana watu kukuamini. Ungetafuta facts kwanza kabla hujakurupuka kuikosoa serikali.
 
kichwa maji kweli wewe unasoma kwa kuruka ruka kukimbilia dirashani kupanga foleni kwa ajili ya buku saba. Huo mradi wa bagamoyo ni uwekezaji sio kwamba nchi inatoa kila kitu toka mfukoni mwake zaid ni hao wachina ndo wanahusika kurun hiyo project
Usiwe mjinga kijana! Huu mradi kipindi cha JK wapinzani waliupigia kelele kwamba tungeboresha kwanza bandari zilizopo, leo nyie manyumbu tena mmegeuka?

Magufuli endelea kuwabana kende hawa kumbe hawajielewi
 
Huyu mh ni tabu sana. Jambo dogo kama hili pia hajachunguza.
Mumielewe zito alichosema,hajamaanisha kutumia magari,amemaanisha wachina ndio wadau wetu wakubwa na wa muda mrefu wa jeshi yaani kuanzia mafunzo mpaka mambo mengine ya kijeshi,maana yake ni kwamba ukiwapanga kwa rank wachina wanaweza kuongoza kwa asilimia nyingi tu kupita misaada na mambo mengine ya kijeshi yanayotoka kwenye nchi alizoziorodhesha mdau.
 
Huu mradi ukianzishwa kipindi cha JK, wakati huo wapinzani walipiga kelele kweli kweli kwamba tuboreshe bandari zilizopo kwanza, leo yamegeuka tena. Ndio maan mm huwa naona hakuna haja ya upinzani Tz maana hawaelewi wanafanya nini
 
Huu ni mradi wa siku nyingi sana ukipigiwa upatu tangu awamu ya nne.... Hauna manufaa kwa taifa kama mtoa hoja anavyojaribu kutuaminisha. Nimemsikia Spika wa bunge leo kwa nafasi yake kama mbunge akijaribu pia kuupigia upatu mradi huu, lakini nagundua tu kuwa na yeye amelishwa matango pori yaliyopakwa cream ya asali. Nchini Kenya wameisha boresha bandari ya Mombasa kwa kiasi kikubwa na wameanza ujenzi wa bandari itakayokuwa na lengo kama hilo la Bagamoyo... Sasa tunakomaa kuijenga bandari ya Bagamoyo kwa ajili ya kuonyesha ushindani?. Kuna upanuzi wa bandari ya Dar es salaam ikihusisha ujenzi wa Economic zones maeneo ya Kurasini na watu wameisha hamishwa, kwa nini tusitekeleze mipango hii badala ya kujenga mji na bandari itakayokuja kushindana na Dar es salaam?.

Naaunga mkono kusitishwa kwa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na badala yake tuboreshe zilizopo kwani hazija endelezwa kiasi cha kushindana na Mombasa ambayo kwa mwambao wa EAC ndio kinara. Tanzania imo kwenye ubia na China kwenye miradi ambayo haijafanya vizuri,.... mifano iko mingi ila nataja hapa TAZARA, mradi wa meli za ushirikiano na China :: SINOTASHIP, miradi hiyo inasuasua muda wote, iweje leo Bagamoyo ije ijengwe kushindana na miradi mikubwa ya Dunia?... Hata kama lengo linaonekana zuri kiasi gani mwisho wa siku masharti yake yataleta matokeo kama yale yaliyoikuta Hong kong na Sri lanka.... Tangu awali niliisha jiwekea nadhiri kuwa nitashika Shilling moja kwenye mradi huo kama utapitishwa.
 
MNAONGEA KAMA TUNATUMIA PESA ZA KUBETIA HAHAAAA EMBU WAENDEEE KUPUMZISHA TU MIRADI ISIOENDEKA WELLDONE MAPRESIDENT
 
Hoja yako ina mashiko kiasi kikubwa, nimeipenda.

Nimeipenda zaidi sababu inaturejesha kwa swali la miaka yote "kati ya kuku na yai kipi ni cha kwanza?" au "fedha na elimu nini kitangulie?".

Hoja ya SGR kuwa huduma badala ya biashara kama bandari isipokuwa fanisi (mizigo michache) hili ni kweli.
Lakini kama hatuwezi kujenga vyote kwa pamoja ni lazima tuchague kimoja, nafikiri SGR ni cha kuanza nacho sababu tayari tunayo bandari inayo fanywa upanuzi, SGR itakuwa inatoa huduma kama ulivyosema wakati tunasubiri mradi wa Bagamoyo ESZ.

Tukiangalia suala la umeme ni kweli itakuwa huduma na biashara lakini uangalie umeme kama kichocheo cha ujenzi wa viwanda vingi vitakavyo hitaji malighafi mengine toka nje hivyo zitapitia bandari na kuingiza pesa, hivyo viwanda pia vingi vitajengwa na wawekezaji toka nje ambao wataleta fedha za kigeni.

Usisahu uzalishaji wetu viwandani ukiwa mkubwa tutahitaji kuunza nje bidhaa zetu, tutahitaji bandari kubwa.

Kwa mtindo kama wa mikataba yetu ya madini, gesi na hoteli tulizo karibisha wawekezaji utaona heri umeme au SGR itakayo kuwa chini ya usimamizi wetu vitaleta pesa kuliko mradi wa wawekezaji tunaosubiria mrahaba sijui mrabaha. Hakuna kitu kabisa tubaishia na vurugu kama za makinikia n.k.
 
Zitto kwenye hili umeingia cha kike. Uharaka wako kuchangia mambo ya kitaifa utakugharimu sana watu kukuamini. Ungetafuta facts kwanza kabla hujakurupuka kuikosoa serikali.
Mkuu elezea kwa vipi ataingia cha kike kama unazo taarifa muhimu za kutosha.
 

Mradi huu sio mzuri kwanza hatuna shida ya bandari nyingine Dar. Pili invetakiwa kuwa Tanga au Mtwara na sio Dar maana kuna mafuta ya uganda Tanga na Mtwara kuna gas sasa Dar kuna nini. Vilevile hatuna pesa uwekezaji unatakiwa kuwa kwenye airport na utalii kwanza mfano hatuna airport nzuri Kia wakati watalii wengi wanashikia pale tungeweka airport ya kisasa watalii wangeongezeka sana. Vilevile wangeweza kugawa hayo maeneo watu wajenge wenyewe. Sasa hivyo viwanda malighafi zingetoka wapi? Serikali kwa namna hii Vilevile wanatakiwa kujenga miundominu kwenye mashamba makubwa ili tuwe na strategic family na masoko ya mazao ya kisasa yenye technology badala ya hii miradi ya kisifa zaidi. Kwenye hili serikali naiunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…